Kundi la Kakau kutoka mkoani Kagera likiwajibika ipasavyo katika mashindano hayo,kundi hili ndilo lililoibuka na ubingwa kwa mwaka huu ikiwa ni mara ya pili mfulilizo.
Kundi la Bujora ambao walishika nafasi ya pili ya mashindano hayo.
Kundi La Kakau likiwa katika picha ya pamoja baada ya kutwaa Ubingwa


Mashidano ya ngoma za asili katika kanda ya ziwa yanayodhaminiwa na bia ya BALIMI EXTRA LAGER ,yamefikia tamati katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na Kundi la ngoma toka Kagera - KAKAU GROUP wameibuka na ushindi wa kwanza. Kundi la Kakau ndilo lililokuwa likishikilia nafasi hiyo baada ya kuongoza katika mashidano ya mwaka jana.

Mashindano ya ngoma za asili kwa kanda ya ziwa 2010, yalianza tarehe 17 Julai 2010 na kushirikisha mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga na Tabora katika ngazi ya mikoa na vikundi viwili vilyoshika nafasi za juu kila mkoa viliingia katika fainali kuu ya kanda iliyofanyika August 7 jijini Mwanza.

Lengo la mashindano haya yanayodhaminiwa na TBL kupitia bia ya BALIMI EXTRA LAGER ni kuenzi na kudumisha mila desturi za makabila ya kanda ya Ziwa, na pia kuongeza mshikamano wa makabila haya kupitia utamaduni wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nice! Pongezi kwa washindi... Asante TBL!!

    ReplyDelete
  2. Hakuna tube tukajionea ngoma za kwetu???Hebu tupeni link basi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...