KOCHA mpya wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Jan Poulsen, leo ameanza kazi yake kwa kutangaza kikosi cha timu hiyo huku akimrejesha kipa namba moja, Juma Kaseja aliyekuwa achwa kwa muda mrefu na kocha aliyemtangulia Marcio Maximo kwa utovu wa nidhamu.

Nyota wengine walionufaika na ujio wa Paulsen aliyechukua nafasi ya Mbrazil, Marcio Maximo, ni Haruna Moshi ‘Boban’ na Athumani Idd ‘Chuji’ ambao pia walitoswa kwa utovu wa nidhamu.

Akitangaza kikosi hicho chenye wachezaji 27, jana, Paulsen alisema ameamua kuwaita nyota hao ili kuamsha ari na mshikamano miongoni mwa wachezaji na wadau kwa ujumla. listi kamili ya Stars hii hapa chini.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. timu tatu tu ndio zinatoa wachezaji kwenye timu ya taifa ,azam,yanga na simba.


    timu zamikoani inabidi zisaidiwe nazo hili kuweza kutoa upinzani kwa wachezaji wa timu za dar.


    hivi michuzi kulikuwa na ugumu gani ku-type hayo majina ya wachezaji hili yaonekane vizuri kwa wasomaji wako?

    ReplyDelete
  2. hii ndio maana kila siku tutafungwa! kwa majungu tu sasa huyu ni kocha mpya hana hata mwezi hapo TZ amewaonaje hao wachezaji wengine kwa kipindi kifupi hiki? Inamaanisha tayari keshatiwa maneno.michuzi usiibane hii

    ReplyDelete
  3. Kweli Mikoani Nimeona Club Moja tu Mtibwa. Zilizobaki Dar-es-salaam na za Nchi za Nje. Kweli Mikoani na Kisiwani kwenye Club zao wachezai wapo ila wanatengwa Ila simlaumu sana Manager Bado anamuda atakuja kuwajuwa tu. Tusihukumu mapema tusubiri azoee na tuone atafanya lipi zaidi au Pungufu? MZ.

    ReplyDelete
  4. Hii ndiyo timu sasa, sio ule upuuzi wa MAXIMO kuchagua wachezaji wa mchangani anajidai eti kujenga vipaji. Timu yetu ilikuwa inafungwa sio kwa sababu wachezaji walikuwa hawajui mpira bali ilikuwa na kocha asiyejua mpira. Sasa mimi nina matumaini makubwa na timu hii. MAXIMO atapata habari zake na ataisikia TAIFA STARS ktk bomba, kocha gani hata timu aliyokuwa anaifundisha Brazil haijulikani!! Tunamtakia mafanikio mema kocha mpya sasa Rwanda itatukoma.

    ReplyDelete
  5. huyu kocha si kaja jana tu sasa amewezaje kutaja kikosi hicho ama amechaguliwa?? naombeni maelezo jamani tusidanganyane !

    ReplyDelete
  6. yaani kocha kawasili jana tu toka ulaya, leo anataja kikosi cha Taifa Stars! kweli U-Simba na U-Yanga umechagua hii timu na siyo kocha.

    ReplyDelete
  7. Huko England au Brazil timu ya taifa haiweze kuwa na wachezaji waliotoka ktk klabu tatu tu(Yanga, Azam,Simba), haya ni maajabu ya mwaka!

    ReplyDelete
  8. Jameni kwani Vancouver whitecaps wamehamia USA? Au aliyeandika hapo alitaka kusema America? I ca't understand such mistakes these days where information technology is soo advanced!! Besides if one has a little geographical knowledge Vancouver is a city in Canada.Ni sawa na kusema Dar young african of Egypt, wapi na wapi.

    ReplyDelete
  9. TIMU YA TAIFA ama TIMU YA MKOA WA DAR????!!!

    Inawezekana vipi kocha mpya kuanza kazi na kuunda timu kwa muda mfupi hivo?

    Timu hiyo iliandaliwa kabla ajafika, na nia ya aliyeandaa imetimia, Hata Tenga hana wazo alilochangia, sbb anauzoefu wa timu inavotakiwa kuwakilisha kanda zote. Iweje hilo alijafikiriwa?

    Kwanini TZ kila kitu ni kama ndoto za alinacha?

    Huo ni uzembe mkubwa, na itashusha kiwango cha mpira wa miguu mikoa mingine na taifa kwa ujumla

    ReplyDelete
  10. JAMANI:

    1. KUNA NJIA NYINGI ZA KOCHA KUCHAGUA WACHEZAJI, SIYO LAZIMA AKAE HAPA BONGO MWAKA MZIMA.

    2. MCHANGANUO WA TIMU NA WACHEZAJI NI KAMA HIVI:
    YANGA = 8
    SIMBA = 7
    AZAM = 7
    MTIBWA = 1
    KUTOKA NJE 4.

    TUSILAUMU LAKINI TUJIULIZE KWA NINI?

    JIBU NI KWAMBA TANZANIA TIMU ZENYE HELA NDIZO HUCHUKUA WACHEZAJI BORA KWA USHAURI WA MAKOCHA WAO. HIVYO, PANGA PANGUA, TIMU YA TAIFA LAZIMA IWE NA WACHEZAJI KUTOKA KWENYE TIMU TAJIRI ZA TANZANIA, AMBAZO ZOTE NI ZA DAR ES SALAAM. KWA ANAYEFUATILIA LIGI YA TANZANIA MWAKA HADI MWAKA ATAONA HILI NI JAMBO LA WAZI KABISA.

    SUALA HAPA NI JE, TUFANYEJE ILI TATIZO KAMA HILI LIISHE?

    AIDHA, TUFAHAMU KUWA KWA SASA TABIA YA KUCHUKUA WACHEZAJI WAKALI KUTOKA NJE NDIYO ITAUA KABISA VIPAJI VYA WACHEZAJI WA TANZANIA.

    HILI NALO LINAKUJA.

    MICHUZI, HAWA VIJANA WASIOCHAMBUA ISHU HATA KWA JUU JUU TU UWE UNAWAWEKA KAPUNI. DEMOKRASIA YAKO KALI ANKAL, HUWAACHI TU?

    ReplyDelete
  11. Wadau muangalieni kocha wa liverpool ametaja kikosi chake kamili hajatimiza miezi huyu kuna kumbu kumbu jamani ninyi muko tu na majungu, wacheni majungu tujenge team ila kocha namshauri apite na visiwani zenji kuna vipaji kule kina canavaro, abdi kasiim aliefunga goli zuri na la kwanza kwa uwanja wetu pamoja na abdulhalim wte ni wachezaji wa kutegemewa team ya taifa wanatoka kule.

    ReplyDelete
  12. Kocha kaingizwa mkenge. Lazima. Lakini uzuri wa tabia huwa haijifichi. Wale wale tunaowajua wana tabia ya ajabu haumalizi mwaka, watakuwa nje. sababu ni ukosefu wa nidhamu

    ReplyDelete
  13. Sasa huyu coach, hawa wachezaji kawaona wapi?

    ReplyDelete
  14. Sasa huyo jamaa mmemuokota wapi?mbona hatujawahi kumsikia au ndio...buy one ,get one free!!!!

    ReplyDelete
  15. UKITAKA KUYAONA HAYO MAJINA KWA URAHISI AU KWA KUSOMEKA WEKA CASOR YAKO KWENYE MAJINA NA DOUBLE CLICK =CLICK MARAMILI KWA SPEED YATAKUWA A KUSOMEKA. KUHUSU VANCOUVER WHITECAPS KUANDIKWA KUWA NI USA NIA SAWA PAMOJA NA KUWA IPO CANADA KATIKA JIMBO LA BRITISH COLUMBIA WEST OF CANADA JIRANI AU JUU YA JIMBO LA WASHINGTON (SEATTLE)LA USA LAKINI ITAANZA KUCHEZA LIGI YA USA INAYOITWA MAJOR SOCCER LEAGUE NI TIMU MBILI ZA CANADA ZITAINGIA KATIKA LEAGUE HIYO NAYO NI PORTLAND NA HIYO VANCOUVER WHITECAPS ZIMESHAORODHESHWA KATIKA MLS

    ReplyDelete
  16. Unkali, Hebu Acha Kutuuumiza Macho!! Tuwekee Hiyo List iwe inasomeka vizuri au wewe unaona inasomeka maana isije ikawa sisi ni vipofu watarajiwa!!!!!

    ReplyDelete
  17. Mdau Mon Aug 02, 09:07:00 PM
    Mabingwa wa dunia Spain ilikuwa na mchezaji mmoja tuu ambaye alikuwa achezei barcelona au real madrid katika mechi ya fainali na uholanzi.
    Barcelona= 7
    Real Madrid= 3
    Villareal = 1

    sasa unapokuja kwetu apa nyumbani Barcelona na Madrid ndo kama Simba na yanga kwa ubora na ubora unaletwa na wachezaji waliopo humo ndani.

    ReplyDelete
  18. Vancouver whitecaps iko vancouver canada. Major league soccer(MLS) inaundwa na timu za canada na usa,ni kama vile NBA ilivyo na toronto raptors ya toronto canada.
    by the way,portland sio ya canada,ni timu ya oregon usa.

    ReplyDelete
  19. nyie mnao lalamika hamuoni list ya wachezaji sijuhi mnaumia macho rudini shule hata basic knowledge ya computer hamana !! vingine silazima muulize kuweni wabunifu !! mnachua kucheza karata tu na kusikiliza bbc on line !!

    ReplyDelete
  20. watanzania awawezi fika popote siku zote na wanao jua hilo huwa hawajihusishi na chochote made in tanzania !! watanzania walisha laaniwa . hata vitu simple zero kabisa. Sasa hata waandishi wa habari awawezi kuwaoji hao TFF si wanaalikwagwa kwenye press conference !!

    ReplyDelete
  21. Jamani hili sio bunge kwamba kila jimbo lazima liwe na mwakilishi, wote tunajua kwamba wachezaji wazuri hawawezi kukaa mikoani maana kule hakuna fedha na hata wakichaguliwa lazima watahamia vilabu vya DSM maana mpira ndio ajira yao. Kuhusu uchaguzi, kocha yeyote mgeni lazima apate sehemu ya kuanzia hatuna muda wa kungojea ili awaone wachezaji mwenyewe maana mashindano hayatungojei na mwezi huu tunacheza na Egypt. Kitu ambacho sikupenda ni kuelezwa kwamba wachezaji fulani hawana nidhamu hasa kwa kuwa Maximo hakusema walifanya nini. Kocha mpya ataanza kwa mawazo hasi kuhusu wachezaji hao tofauti na wenzao, nilitegemea baada ya kumsaidia kuchagua angeachwa aone mwenyewe kama hawana nidhamu.

    ReplyDelete
  22. MICHU ULIBANA COMET YANGU LAKINI KOCHA WA JANA AMEJUAJE KIKOSI KAMILI? HAYA SAIVI MNASEMA NDIO TIMUNGOJA IBORONGE TENA MSEME SERIKALI INAPOTEZA HELA

    ReplyDelete
  23. Nyie wooote mnaosema u simba na u yanga hamjui mprira chagueni fani nyingine, kwani hamjui katika world cup 1st 11 ya spain ilikuwa na wachezaji 7 wa Barcelona 3 Real madrid na 1 others? pia jifunzeni ki english maana alisema jana kwakuwa hana muda atatumia zaidi timu iliyopo na kuongeza wachache waliofungiwa ili uleta mshikamano.Tafakarini kwnza kabla ya kupoteza muda kuandika tu

    ReplyDelete
  24. Wadau bwana wakipata nafasi ya kuongea basi wanaongea tuuu! Sasa kosa liko wapi?? mlitaka aseme nipeni miezi mitatu nichaguee kikosi???? hapa hata angesema hivyo wangeanza..ohhh kocha gani anataka muda wote huo! ahhhh bongo tambarare!

    ReplyDelete
  25. his selection of players was based on advice from a section of local coaches and the technical committee of the Tanzania Football Federation (TFF).

    ReplyDelete
  26. Inawezekana kawaona hao wachezaji kwenye DVD au kumbukumbu za TFF. Cha ajabu hapa ni kwanini TFF hawakuwa na mipango ya muda mrefu ya kumuandalia ziara ya kuangalia mazoezi ya vilabu vyenye wachezaji husika, huku jukumu la kuifundisha timu kwa mchezo na misri liachiwe Mwl msaidizi wa uongozi uliopita huku yeye akikaa jukwaani.
    Kwa kawaida meneja anaanza kutaja kikosi cha ufundi(back room staff) kisha wachezaji husika. Sasa kwa hili sina uhakika kama limefanyika kiufundi.Nangoja kwa hamu kusoma makala ya super coach Mziray juu ya hili suala.

    ReplyDelete
  27. Anonymous wa Tue Aug 03, 12:34:00PM

    Jiulize Spain ni ya ngapi ktk FIFA ranking na Barcelona na Real Madrid ina mafanikio gani ktk viwanja vya nje ya Spain.

    Hapa Simba haikufungwa hata game moja ya local league, ktk mechi nne za Kagame cup Ilifungwa mara tatu tena na timu za EA, Yanga ndio hivyo wewe unajua.

    kucheza Simba au Yanga haimaanishi wachezaji wa viwango vizuri zaidi ya kusaidiwa na waamuzi na TFF katika ligi ya Vodacom.

    Hapa hakuna ushindani wa kutosha.......Maamuzi utata mtupu.....Timu za mikoani hazipewi support..hata makampuni mengine yadhamini timu mbili tu.

    kihistoria upcountry ndiko kuna mhimili wa mpira wa Tanzania.

    TFF lazima wawajibike katika hilo, Hapo sio sehemu ya kutafuta umaarufu au mlango wa kwenda kwe siasa. Tafuteni watendaji wa kweli...sio waganga njaa.

    Najua wewe Michuzi hutaiweka hii comment....hata usipoiweka mradi wewe mwenyewe uisome inatosha.

    ReplyDelete
  28. WADAU MSILALAMIKE.

    TULICHOKIFANYA KWA MARA HII NI KUMCHAGULIA WACHEZAJI AMBAO KWA MTAZAMO WETU TUNAONA WAKO JUU ILI AANZE NAO KWANZA.

    HALAFU AKISHA KUWA MZOEFU NA KUWEZA KWENDA MIKOANI ACHAGUE WACHEZAJI AMBAO YEYE ATAONA WANAFAA KUWA KATIKA KIKOSI ATAKACHOUNDA.

    ReplyDelete
  29. MAXIMO YUPI TENA?

    ReplyDelete
  30. Acheni ubishi ambao hauna kichwa. Alisema amechagua team toka kwenye kikosi kilichocheza na Brazil. Fanyeni utafiti na si kuongea tu. Mlitaka asubiri lini ndo achague timu??
    Wachezaji wote wazuri walioko mikoani wakishacheza msimu mmoja wa ligi msimu unaofuatia wanahamia kati ya Simba ,Yanga ama Azam.

    ReplyDelete
  31. UNAJUA WATU WENGI HAWAJUI MPIRA,WANALALAMIKA KWA NINI AMECHAGUA YANGA,SIMBA NA AZAM.
    MARCIO MAXIMO ALISHAULIZWA HILO SUALA NA AKAJIBU KUWA HATA UKICHAGUA WACHEZAJI KUTOKA JAMHURI YA PEMBA ,MAJIMAJI YA SONGEA,KARIAKOO YA LINDI HUYO MCHEZAJI AKIWIKA TIMU YA TAIFA MSIMU UNAOFUATA ,SIMBA,YANGA NA AZAM WATAMSAJILI NA KOCHA HAWEZI KUMUACHA TIMU YA TAIFA KWA KUWA TU AMEHAMIA SIMBA.

    MKUMBUKE WACHEZAJI WAFUATAO WALICHAGULIWA TAIFA STARS NA MAXIMO WALIPOKUWA NA TIMU ZIFUATAZO:
    JACKSON CHOVE - JKT RUVU(PWANI)
    STEPHONO MWASIKA - PRISONS(MBEYA)
    ABDURAHAMAN HOMOUD-MNZANZIBARI
    NIZAR KHALFAN-MTIBWA
    UHURU SELEMANI-MTIBWA

    SUALA LA TIMU YA SASA KUJAA SIMBA,AZAM NA YANGA NI SABABU ZILE ZILE HATA PAULSEN AKIENDA PEMBA AKACHUKUA WACHEZAJI WAWILI TOKA TIMU YA JAMUHURI WAKAWIKA TAIFA STARS HAO WACHEZAJI HAWATAWEZA KUENDELEA KUCHEZEA TIMU YA HUKO PEMBA KWA SABABU YA UMASKINI BALI WATASAJILIWA SIMBA,YANGA,AZAM AU MTIBWA, NA KOCHA HAWEZI KUMUACHA KWA KUWA ANATOKA DSM AU WENGI WATATOKA TIMU ZA DSM KOCHA ANACHOANGALIA NI NIDHAMU,KIPAJI NA UWEZO WA MCHEZAJI HUSIKA.SUALA LA KUWA NA TIMU YA KITAIFA HUO SASA NI UKABILA KWA KUWA HATA UKIFANYA UKABILA WACHEZAJI WOTE WANAOCHEZA TIMU ZA DSM SI WAZARAMO.

    MPIRA SI SIASA KWAMBA RAIS AKIWA M-BARA BASI MAKAMO AWE MPEMBA NA RAIS WA ZANZIBAR AWE MUUNGUJA.MPIRA NI PROFESSIONAL.

    KOCHA WA TIMU YA TAIFA HAFANYI KAZI PEKE YAKE YA KUCHAGUA NATIONAL TEAM BALI HUSHIRIKIANA NA KAMATI YA UFUNDI YA T.F.F AMBAYO HUWA NA WATAALAM WA SOKA WAKIWEMO MAKOCHA WA KIZALENDO NA TAFCA.HAO WANAHUSIKA KATIKA KUCHAGUA TIMU YA TAIFA AU KUMSHAURI KOCHA.KOCHA MGENI ANAYEKUJA TOKA NJE YA NCHI MWENYE WIKI TATU KABLA YA MECHI YA KIMATAIFA HUANZA NA TIMU YA TAIFA ILIYOPO NA BAADAE HUIBORESHA TARATIBU NA TIMU HII NI ILE ILIYOACHWA NA KOCHA ALIYEMTANGULIA KOCHA MPYA AMBAYO HUONGEZEWA WACHEZAJI WACHACHE KWA KUSHAURIANA NA KAMATI YA UFUNDI YA CHAMA CHA SOKA(T.F.F).

    KAMA PAULSEN ANGEKUJA MAPEMA MWEZI JANUARI ANGEWEZA KUCHAGUA MWENYEWE TIMU YAKE LAKINI SASA MUDA HUO HAUPO NA HAKUNA LIGI.

    MKUMBUKE KUWA MCHEZAJI HAJIFUNZI MPIRA TIMU YA TAIFA,HUWEZI UKATOA WACHEZAJI SABA LEO TOKA WASIO NA UZOEFU WOWOTE HALAFU UKAWAPAMBANISHA NA MISRI AU ALGERIA,MKUMBUKE MAXIMO ALIVYOCHUKUA TIMU YA TAIFA ILIYOCHAGULIWA NA MSHINDO MSOLLA TIMU ILIFANYA VIZURI ,LAKINI BAADA YA KUWAINGIZA YOSSO WENGI TIMU IKAANZA KUFUNGWA FUNGWA NA HATA CHALLENGE CUP TULISHINDWA KUPATA MATOKEO MAZURI.

    KATIKA TIMU HII YA TAIFA WACHEZAJI WAMECHAGULIWA TOKA TIMU NANE TOFAUTI:
    SIMBA,YANGA,MTIBWA,AZAM,DT LONG AN,VANCOUVER WHITECAPS,KONGVISNGER NA SOFAPAKA.

    WACHEZAJI WOTE NI WATANZANIA KWA HIYO HAKUNA KOSA LOLOTE HAPO,MPIRA SI SIASA!

    END

    ReplyDelete
  32. GP W L T GF GA PTS
    Milltown FC
    13 7 2 4 21 15 25
    York Region Shooters
    13 7 3 3 20 14 24
    Serbian White Eagles
    10 6 1 3 21 6 21
    TFC Academy
    12 6 3 3 18 14 21
    FC Hamilton Croatia
    13 5 3 5 27 17 20
    Brantford Galaxy
    11 5 3 3 26 23 18
    Portugal FC
    12 5 5 2 23 23 17
    Montreal Impact Academy
    14 4 6 4 19 15 16
    North York Astros
    13 4 7 2 21 27 14
    Toronto Croatia
    9 2 2 5 15 16 11
    Brampton Lions
    13 3 8 2 15 24 11
    St. Catharines Wolves
    12 2 8 2 13 28 8
    London City
    11 1 6 4 13 30 7

    CANADA WANA LEAGUE YAO INAITWA CANADA SOCCER LEAGUE HIVYO SI TIMU ZOTE ZA CANADA ZINAZOCHEZA LEAGUE YA U.S.A = MAJOR SOCCER LEAGUE HADI SASA NI TIMU MOJA TU YA CANADA INAYOCHEZA MSL YA U.S.A. NAYO NI TORONTO FC ILIYOINGIE LEAGUE YA U.S.A. MWAKA 2006 VANCOUVER WHITECAPS IMEJIANDIKISHA MWAKA HUU NA ITANZA KUCHEZA LEAGUE YA U.S.A 2011 MARCH, NA TIMU INGINE YA MONTREAL IMPACT IMEJIANDIKISHA MAJOR SOCCER LEAGUE YA U.S.A LAKINI ITAANZA KUCHEZA MWAKA 2012 TIMU HIZI ZIMEHAMIA HUKO KWA AJILI YA COMPTITIVENESS YA SOKA YA USA NA BIASHARA PIA I MEAN PESA KWA KUWA HIZI TIMU NI PROFESSIONALS NA NI BIASHARA NI MAKAMPUNI KAMA VILE YANGA ILIVYOTAKA KUWA KAMPUNI AU KAMA MANCHESTER UNITED ILIVYO. THAT IS KOCHA WA TANZANIA AMEANDIKA VANCOUVER WHITECAPS KUWA NI USA KWA VILE IKO KWENYE LIGI HIYO. HAPO JUU KABISA NI LEAGUE YA CANADA NA MSIMAMO WAKE HADI WEEK JANA. INAITWA CANAA SOCCER LEAGUE. PIA CANADA KILA JIMBO INA CHAMA CHAKE CHA MPIRA NA LEAGUE YAO PIA NA AMBAO WANAKUJA KUCHEZA LIGI YA CANADA NZIMA

    ReplyDelete
  33. Kocha kuna Kipa mwingine hapa Helsinki wa Bongo FC Mr kipara ka vipi wasiliana na scorali ezza. aweza kutusaidia huko Egypt.

    ReplyDelete
  34. Timu ya Spain haikuwa na wchezaji 11(7+3+1) kama unavyodai, lazima ilikuwa na wachezaji zaidi ya 23 pia Torres wa liverpool hukumtaja ktk kikosi kizima cha Spain, yaani hatuzungumzii first eleven!

    Miaka ya zamani kina Leopald Tasso , Sululu, Shiwa Liambiko, Chuma n.k walitokea mikoani na ndio maana Taifa stars ilikuwa tishio, ilitakiwa angalau vipaji tulivyoona ktk kombe la Taifa kama toka Lindi n.k wangekuwemo.

    Hapa hakuna kitu, tuambiwe tu kuwa kamati ya ufundi ya TFF ndiyo iliyomchagulia Kocha wachezaji hawa, baada ya kamati kubanwa na U-Yanga, U-Simba na pochi la Azam, lakini hapo hakuna viwango.
    Mdau
    Cairo.

    ReplyDelete
  35. Timu ya taifa haichaguliwi kidemokrasia. Mnataka kocha wa taifa achukue wachezaji wa mikoani wakati hajawaona? Achukue wachezaji ambao hawana hata uzoefu wa ligi kuu ya Tanzania? Pandisheni viwango vya timu za mikoani ndio mseme achukue wachezaji wa mikoani.
    Tushukuru kwamba Wamisri wametuchomolea mechi. Kama ingetokea Kaseja akadunguliwa mabao matano tena na Wamisri sijui tungesemaje...

    ReplyDelete
  36. WEWE wacha Kelele Kocha wa Liverpool kwanza ile timu ya Club la Pili bado hajapanga kikosi bwana.

    La hapa ni timu ya Taifa aliyesema wachezaji wa Kisiwani hakuna aliyelalamika hilo watu wamelalamika wachezaji wengi wanatoka Dar-es-salaam na Sio Mikoa mengine au Kisiwani kwenye vilabu vya huko huwa hawatizami tukianza Kuiga Spain hatutofika leo.

    ReplyDelete
  37. nani kakwambia kiwango cha Simba na Yanga kipo juu?

    Timu zinanunua wachezaji kwa mamilioni na ligi ikianza inabidi wachezaji hao hao wanunuliwe magoli kwa marefa.

    Hushangai watu hao hao wanaongoza kwa magoli hapa wanarudi bila hata goli la off side kwenye international games.

    ReplyDelete
  38. we anonn wa kwanza nikuulize timu ya taifa ya hispania kombe la dunia 2010 ilikuwa na wachezaji wa barca wangapi na real madrid wangapi? bje hispania hakuna timmu nyingine kama bongo?

    usiwe mshamba kama jamaa fulani ambao huwa wanakomaa kocha msaidizi atoke kwao eti ndo usawa.

    swala si wametoka timu gani, la msingi wanaweza?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...