Home
Unlabelled
miss TZ 2007 Richa adhia katika CNN
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Tanzania urangi upo miaka nenda na dahari. Tunabaguana na kudharauliana sana tu.
ReplyDeletecomments nyingi za waliohojiwa zinafanana na mawazo ya watanzania wengi, la ajabu ni kuwa comments kama hizo kama angelisema mzungu basi akngeliitwa racist, lakini kwa kuwa kasema mwafrika basi ni sawa. ukweli sio sawa, racist ni nja mbili.
Watanzania ni wabaguzi mno!
Binafsi, siwezi kuwalaamu Watanzania kwa hilo, uhuru wa kujieleza kila mtu
ReplyDeleteanao na hasa katika dunia ya leo ambapo freedom of speech imeshika kasi. Suala la racism ipo kote duniani, hata mataifa makubwa kama ya Israeli wamejikuta wakiyafanya madudu ya wazi wazi kwa watoto wadogo waliozaliwa kwenye ardhi yao na wazazi ambao si wayahudi. Kwa bahati nzuri nimeshafanya kazi na wahindi, hivyo ninawaelewa fika jinsi wanavyomchukulia mtu mweusi, lakini pamoja na hayo pia nimeshakutana matukio ya udhalishashaji mkubwa tena kwa wazawa. Wahindi hubagua na kuwanyanyasha wafanyakazi wa ndani kama vile mbwa.Siyo hili tu, bali kuna mambo mengine kadha wa kadha ambayo nitashindwa kuyazungumzia hapa.
Unajua maisha yangu yote niliyoishi Tanzania sijawahi kusikia ndoa kati ya wanaume wa kimakonde na hawa dada zetu wenye asili ya kihindi, je huu si ubaguzi wa rangi jamani?
Nimesoma india nimeishi india hawa jamaa hata ukizaliwa india huwezi kuwa muhindi ni wabaguzi sana! tuache hayo kwanza wa hindi wa tz wanaishi kwetu lakini awaeshimu tamaduni zetu wana tunyanyasa wanatubagua ndani ya nchi yetu !! mimi nikiwa rahisi wa hindi wazaliane na wa tanzania weusi lasivyo wajikate pia wewe mtanzania gani hata kiswahili hajuhi ,history ya nchi yetu hajuhi , Nimeishi KISUTU so nawajua sana hawa wa bagachori !!
ReplyDeletewa hindi wa bara wanatakiwa wafanywe kama wale wa zanzibar ndo hadamu hitakuwepo!!
ReplyDeleteWell and neutralised balanced story.
ReplyDeletewaarabu na ujinga wao wote basi nawapa hongerakwa kuwaweza hawa jamaa. lakini tufahamu ya kuwa mambo haya sio yeye huyo dada wakusemwa hivi hakuna njia ya watu kuweza kujuwa wapi huyo ametokea???au serekali inauwezo wakuchunguza magaidi tu na wanasiasa wasiowapenda????na tujue kila jamii inawazuri na wabaya...
ReplyDeleteHawa wahindi ni wabaguzi sana, wengi wa wanaoomba uraia Tanzania msizanie wanaipenda nchi la hasha wanacho fanya ni kuja Tanzania kukusanya pesa kwa biashara za ukwepaji kodi na kutumiwa na viongozi kuiibia serikali baada ya hapo wanaomba visa za UK (hebu nenda ubalozini uone wanaoongoza kuomba visa ni watu gani) au Canada na USA kwani kule kwao India ni vigumu sana kupewa visa za nchi hizi.
ReplyDeleteNiliwahi safiri na dada mmoja wa kihindi anatokea Canada alipokuwa ameolewa, dada huyu aliniambia anatokea morogoro na mama yake anafanya kazi Bank ya CRDB morogoro. Tulikuwa siti moja kama lisaa zima alikuwa analia na kufuta machozi mimi ubinadamu ukanijia nikamsalimia na kumuuliza kama anaumwa niite attendant akaniambia hapana; alikuwa anarudi Morgoro baada ya kuolewa na jamaa wa kihindi ambaye mama yake alimlazimisha na muhindi mmoja aliyewahi kuishii akapate TZ kisha akapata uraia wa Canada na baadae kuwachukua ndugu zake wote kutoka TZ ili nae akikaa kwa miaka mitatu(kama sijasahau) kule apate uraia. Akaniambia jamaa yule alikuwa hawezi tendo la ndoa(jongoo halipandi mtungi)ila akavumilia huku ndugu wa yule mwanamume wakimchunga; akapata deppression baada ya mwaka akarudi TZ; kufika mama yake akamwambia asipoteze muda kwani yeye anamtegemea yeye apate uraia ili aje amchukue, baada ya wiki mbili za kujirusha na boy friend wake wa bongo akanda pipa anasema alipotu tu Canada akaanza kuwa analia tu kila wakati, baada ya wiki moja ikabidi arudi kwani mama mkwe alikuwa anamsimanga sana kuhusu mwanae na kwamba mtu hawezi kufanya kitu ila yeye anang'ang'ania ili apate uraia tu; basi katika safari ile kilio chote kilikuwa ni kwamba hawezi kaa Canada bila kufanyab"mambo yetu" na bongo mama yake anataka avumilie tu.
Nilimuonea huruma sana yule dada lakini pia nikapata picha mtu anafanya kazi bank nchini Tanzani a preveledge goes to the few bado anataka kuikikbia nchi kweli huyu mzalendo kweli?
Baniani mbaya kiatu chake dawa. Mbantu akiwa na shida haendi kwa ndugu yake kwa msaada ila ankwenda kwa hao wanaoitwa magabachori.
ReplyDeleteWatanzania ni waguzi mno tena sana. Inabidi tubadilike hata wamerakini wenyewe wanaongozwa na mnya nje. Tubadilike jamani acheni ubaguzi.
Bora Rita changanya supu ishi na watu wenye akili na wanaofanana na wewe. Achana na mijitu iso na akili
Hayo ni maoni ya mtu binafsi, kuna wabunge watanzania wenye asili ya kiasia wanachaguliwa kwa vishindo, mimi mgozigozi kuanzia shule ya msingi DSM mpaka Sekondari DSM nilifundishwa masomo ya siasa na kiswahili na waalimu wa kiasia mpaka nimekuwa mzalendo kwa ajili ya siasa na kwa upande wa kiswahili ndiyo usiseme walinipa hamu ya kusoma KULI na Vitabu vya Shaaban Robert.Kuna mwalimu mmoja wa kike wakihindi ni mke wa jamaa mmoja wa mikoa ya kaskazini, mama huyo wa Kihindi alikuwa mwalimu wetu sekondari miaka ya 1980 Darisalama.
ReplyDeletekuna mifano mingi tu hata huku Uingereza barabarani utawasikia ndugu zetu watanzania wa kiasia wanaongea kiswahili swafi cha Kariakoo baina yao hapa jijini London na ukijiunga ktk gumzo yaani mpaka raha, wazungu wanajiuliza hivi hiki kiwingu cha mchina, mwafrika,mwarabu, wahindi wawili na mmatumbi wanaongea lugha gani hiyo- hawajui ni kiswahili.Sasa ukiona mhindi- mtanzania anaongea kiswahili nyumbani kwake hapa London(maana gujarati/urdu inampiga chenga), je huyo si mtanzania?
Ila maoni ya mtu binafsi naona yanachangiwa sana na maisha mtu aliyopitia. Mimi mswahili nimepitia maisha tofauti, hivyo nina mtizamo kuwa ubaguzi ni sumu, ila siwezi kuwatuhumu jamii fulani mzima kuwa ni wabaguzi.
Mdau
Mtoto wa Mjini
Acheni Kiswahili cha Kikenya hapa....siyo katika CNN bali ni "kwenye CNN."
ReplyDeletemimi na shanga sana, as to why would Issa Michuzi the champion of Human rights decide to post this OLD video at this time? Pengine ana taka kuchokoza Peacefulness that prevails the people of TZ...
ReplyDeleteI challenge you Mr. Michuzi, your blog, which I visit daily for the last 3 years, is a showcase for paiting watanzania wenzako-wahindis in bad news only. Hii ni wazi kabisa, go back and check your old blogs...wafrika and wazungus are always in positive spin...missing in your blogs are Arabs...I am not sure why...so you your self unabagua despite your claim otherwise...na hii ni wazi katika blogu zako...BTW I still will always visit your blog...and love it...Mungu Ibairiki Tanzania...local mdau
Richa Adhia should be ashamed of herself for trying to brand Tanzania as a xenophobic nation. Many Tanzanians rooted and even cheered for her when she was contesting in the Miss World Pageant, it's only the few who were against her. It is utterly despicable to use these outliers to generalize the entire nation.
ReplyDeleteOn the other hand, Indian community in Tanzania shares part of the blame also for being reluctant in assimilating into Tanzanian's culture. It is sad, but true, that these people have shun Tanzanian’s culture simply because they perceive it to be inferior compared to Indian’s culture. It is superiority complex, which is engrained in their DNA, that have bamboozle our brother and sisters of Indian decent that is reason they are still embracing Indian culture in lieu of Tanzania's culture.
Mbona haya mambo ya kawaida tu. Ndivyo tulivyo watz. wahindi, waarabu ni miongoni mwa makabila yetu.
ReplyDeleteTunaishi kiutani zaidi, wengine tumezoea. Utasikia duka la mchaga, saluni ya mhaya, bucha ya mkurya, shamba la msukuma, baa ya mkwere na mifano mingine mingi na mtu anafanya hivyo hana hata ile hisia ya kubagua.
No matter what we al comments, prejudice is not easy thing to get rid off in any country of the world, talking about Indian-Tanzania not to be fully integrate in our society is just like talking about telling wahaya not to prefer they are own. What we need to look is goverment involvement in producing kind of leafleats which will encourage the acceptance of multicultural and diversity into our country. Rachida is a Tanzanian of Indian original. Lets us not live at zama za Mirambo.
ReplyDeleteWhen there is nothing to discuss it is time to make wahindis the scape goats.It is no surprise,it is happening always not only in Tanzania but many countries in the west also.When we see somebody successful we dont ask how they did it but we ask why he did it.ALUTA CONTINUA.
ReplyDeleteWatanzania sijuio lini tutaacha ubaguzi. Mpaka SA ambako mpaka juzi kulikuwa na apartheid ya hali ya juu basi wamekazana kuacha tofauti zao na kujiita rainbow nation. Sisi tunawatukana wahindi kuwa ni wabaguzi basi kama ni hivyo basi mbona SA na nchi nyingi sana wanashiriki katika mashindao kama hayo na wanakubalika na watu wanawasupport. Sisi uwelwewa mdogo, elimu ndogo, chuki na hasama. Sasa ikiwa kama wanachapa kazi na kuwa na maisha mazuri basi na sisi tuwaige sio tuwachukie. maan yule aliyesema baniani mbaya kiatu chake dawa haku kosea. Tukiwa na matatizo basi mara tunamfuata mhindi tu wakati huo tunamwita 'wangu' ili tupate pesa. Sasa unafikiri wahindi wajinga hawajui kwamba tunawafuata kwa shida tu na wakati wa ushirikiano na support tunawaita wabaguzi? sasa kama hivyo nawo watatukimbia - unafikiri nani anapenda kuombwa ovyo?
ReplyDeleteKwa wale wahindi kama MO, zakia meghji na wengine ambao wanachangia mbona hatuwapongezi na tunageneralise tu?
Kwa hali hii maendeleo Africa ndoto kweli...
Jamani watanzania siyo wabaguzi hata kidogo. Hivi kuna watu wabaguzi kama wahindi achilia mbali wajerumani? Wahindi wenyewe kwa wenyewe wanabaguana tena sana ndio maana wamekuwa na matabaka. Sasa kwa hapa TZ wapo wahindi ni ma MP etc wanafanya kazi zao bila usumbufu. Nenda kule India uone balaa litakalokukuta kama wewe ni mtu mweusi,utabaguliwa mpaka ukome,kwanza huna haki kwa kitu chochote ukiwa kwao. Sasa leo hii wanaishi kwa amani hadi wanapewa nafasi za kutuwakilisha kama mamiss,wengine wameoa hadi dada zetu,ni amani tu,jaribu kule kwao kuoa kama hujakatwa kichwa,then mseme sisi ni wabaguzi. Jaribuni kufuatilia asili yenu(uhindi) mtaogopa hata kutulaumu!!
ReplyDeleteHiyo mijitu mibaguzi inayosema kwamba et wahindi wanajali utamaduni wao kuliko ule wa tanzania. Kwani utamaduni wa tanzania ni upi? tanzania ni multicultural na humu kuna makabila mengi. Leo utamwambia mmasai asijali utamaduni wake? na yeye ni mtanzania... mhaya, mmakonde, mpemba wote wana tamaduni zao sasa kwanini mhindi asijali wao? Tatizo ni chuki hatupendi kuwaona wahindi wakija mbele kwa sababu wanajitahidi.. na nyinyi si mjitahidi mpate maendeleo? siku zote njaa tupu na kuwafuata hao wahindi mkiwa na shida na ndio maana mnadharauliwa siku zote... hebu chapa kazi na wewe upate kuendelea basi uone kama utadharauliwa.. mbona wahindi wanaoishi uzunguni hawaitwi wabaguzi??? hawaombwi ovyo eti..
ReplyDeleteacheni UBAGUZI - tafuteni maendeleo.. kazi kukaa mitaani tuuu
comments nyingi zilizotumwa hapa zimeprove kuwa kweli watanzania ni ma-racist. Tatizo ni kuwa hawajijui au wanataka ku-justify u-racism wao kwa vitendo wanavyofanya wahindi nchini tanzania. Jambo ambalo sio sahihi, ni sawa na kuwa muingereza aanze kuleta maneno yake ya chuki kwa mtu mweusi na a-justify kwa kuwa wauza unga wengi ni weusi au jela zimejaa watu weusi.
ReplyDeleteHivi nyie wengine vipi lakini? Huyo ni raia wa Tanzania ana haki za kimsingi kufanya lolote, kushiriki katika mashindano yeyote yale kama Mtanzania mwingine yeyote, maswala ya kuwa eti yeye anajamii ya Kihindi ni nonsense, mbona Miss England mwaka 2006 Hammasa Kohistani alikuwa na asili ya Kiarabu tena hata hakuzaliwa UK wala nini lakini kwa kuwa wazazi wake walipata uraia wa UK na yeye akaweza kushiriki bila ya kipingamizi chochote, nachukia sana kuona eti mtu aweza baguliwa sababu ya asili yake, kwa ufupi huyo ni Mtanzania mwenye asili ya Kihindi inatakiwa apewe haki zake za msingi kama raia mwingine yeyote yule, ACHENI MITIMA NYONGO.
ReplyDeleteHuu si ubaguzi pekee uliopo.
ReplyDelete2015 tutapata rais muhindi toka ccm.
ReplyDeletemtasemje.obama oyee ccm ju
Tunawabagua wahindi kwa sababu ya rangi yao. Sasa unafikiri na wao watafanyaje? Yaliyotokea Uganda na baadae kenya kuwafukuza wahindi basi inawafanya wawe na wasi wasi siku zote na hivyo mali wanaipeleka nje. Leo mlalahoi akiwa na shida basi anafuata mhindi hata kama hamjui na kumomba pesa. Kwa sababu wanazo hizo pesa. Lakini shida ikimaliza tu basi tayari tunaanza kuwasema. Sasa jaribuni na nyinyi kutafuta hizo pesa sio mnawachukia kwa sababu wachapa kazi. Leo mnasema eti kwa kuwa anaonekana mhindi basi richa hawezi kutuwakilisha watanzania.. basi ajipake mashizi ndio ataweza kutuwakilisha? basi na hao wabunge wakindi nao pia wache wajipake mashizi ili tupate kuwaamini...
ReplyDeleteTanzania tunasifika lakini ubaguzi umejaaaaa --- na katika mazingira kama haya basi maendeleo NDOTO kweli...
MLIKUWA MNAWAITA GABACHOLI AU PONJOLI.
ReplyDeleteNYINYI WAKISEMA MAFALA MNAKUJA JUU LAKINI WAO WAKO KIMYA HAWAJALALAMA.
mimi ni mwarabu na ni mtanzania nimezaliwa hapa tz na wazazi wangu wote wamezaliwa tz , babu yangu ndo hakuzaliwa hapa pamoja na bibi yangu ambao wote ni marehemu sasa walikuja zamani sana wakiwa vijana na mashua ,kulikuwa hamna ndege wa meli siku hizo , wakapata na uraia hapa , sasa mimi na wazazi wangu hatujawahi kuenda huko alikutoka babu , wala hatupajui , sasa utaniambia mimi pia si mtanzania ? na ikiwa mimi sio mtanzania kwa sababu rangi yangu nyeupe je na nyinyi wabeba maboksi huko UK na nchi zingine mnaoomba uraia wa nchi za kizungu then baadae mnajiita kuwa raia wa huko inakuwaje hapo ? au na OBAMA mweusi kuwa rais wa USA inakuwaje hapo ? au kitu akifanya mtu mweusi ni sawa ila akifanya mweupe sio sawa ?
ReplyDeletenimewaoona wengi mliotoa maoni humu elimu zenu ndogo na pamoja na akili zenu , mnahitaji elimu zaidi.. mungu atuepushe na akili zenu finyu ..
asanteni
mdau mwarabu DAR
kwa hiyoo ndo alienda kushtaki???
ReplyDeletendio sio mtanzania na HAKUSTAHILI kuwa miss Tz,ni sawa na mtanzania mmatumbi aliyezaliwa india HAWEZI kuwa miss india hasilani!!!mara miss india amerika tumueleweje
na ili jambo adi leo limetutia doa la kumweka mhindi kuwa miss Tz...na wasirudie tena maana tutaifunga iyo kamati yao,,nyambaf
na habari ndo iyo
kwa taarifa yako USA si nchi ya wazungu upo hapo?
ReplyDeleteni nchi ya wahindi wekundu,watumwa waliopelekwa kulima na settlers
so mtoe obama hapo!
kwa nafasi za kuiwakilisha nchi wahindi/na wengineo no plizz,,,
tit for tat...u accept us we accept yu,yu dont we never!!
michu si unarudia kutuchokoa?acha tumwage radhi hapa!!
HATUMTAKIIII 2007 tunahesbau hatukuwa na miss Tz
Mdau wa 9:47 a.m nakupongeza kwa upeo wako na mawazo yako - hapa hakuna ubishani... lakini wabaguzi watakuja na hoja za kijinga bado.. kweli elimu ndogo upeo mdogo, uelewa mdogo na ndio maana hamna maendeleo...
ReplyDeletehawajui kama tunaumia wenyewe wakati wenzetu washafika mwezini na wamerudi.. sisi tumebaki kubagua tuu.. hao wahindi ambao tunawabagua basi ndio wako mbele kiuchumi - maana wamekaa kimya na kujali maendeleo.. wakati wengine wamejaa chuki na hasama
haya maendeleo yatakuja labda baada ya miaka 100