UHALALI WA “TITLES” NI NINI?
Kuna aina nyingi za “title” lakini si kweli kwamba mtu yeyote ama bodi yoyote inaweza kuibuka na “title” na kuwapachika watu. Kinachofanyika huwa ni kuwapa watu “sifa za kifani au kitaaluma” yaani “professional credentials” ama ‘academic credentials” na pia vyeo (kama vya kwenye majeshi) na hata heshima tu. Hizi “titles” hazitoki tu kuzimu na kutua kwenye vichwa vya watu. Kwa ufupi kabisa, HAKUNA “TITLES” INAYOTOKANA NA USAJILI wowote ule popote pale, hata kama Wachina, Wajapani na Wajerumani wanafanya vioja hivyo. Kuna “TITLE” moja tu inayozaliwa na shahada moja ya utabibu, “DAKTARI.” Haya tuchambue.
1. Taaluma kama wahasibu, huchukua shahada, kufanya kazi na kisha kufaulu mitihani ya bodi na kupewa kitu kiitwacho CPA (Chartered Public Accountant) ama ACCA huko Uingereza. Watu hawa hawajikwezi na kutanguliza kabla ya jina eti Mhasibu au Accountant. Watu hawa pia huwa wakaguzi wa hesabu, yaani auditors kwa Kingereza. Wahasibu huweka CPA au ACCA kwenye kadi zao na barua/nyaraka za kikazi/kifani na matangazo ya biashara. Pia wapo Chartered Financial Analysts (CFA) ambao huweka kisifa chao, mbele ya jina lakini kamwe hawawezi kuitwa chochote kabla ya jina.
2. Aidha, taaluma nyingi zina usajili, mathalani wasanifu majengo (architects), wachumi wa ujenzi (quantity surveyors ama building economists), marubani, wauguzi, mawakili, na wengineo walimu wa chekechea hapa Marekani, madalali wa nyumba, watunza wagonjwa na vikongwe, washauri binafsi wa fedha, mafundi wa kompyuta, watoa mitihani ya lugha za kigeni, wakaanga nyama, n.k. Wote hawa hawana hiki kioja cha kujiita Pilot Kweche Kwichi ama Architect Kuja Kuondoka. Kulikoni wahandisi?
3. ENGINEER (MHANDISI): Hii ni sifa anayopata mtu mwenye shahada ya kwanza ya uhandisi ambaye baada ya kufanya kazi ya uhandisi chini ya usimamizi kwa muda fulani na kufaulu mitihani ya bodi ya usajili, hupewa HAKI ya KUTAMBULIWA kama mhandisi (engineer). Anaweza kuandika kisifa hicho mbele ya jina lake kwenye kadi (business card), barua za kikazi na nyaraka za kifani. Hiki si kitangulizi kabla ya jina. Huenda wapo watu kwenye nchi zingine ambao hufanya hivi, hao wamo kwenye kundi moja na Watanzania wetu wanaofanya hivyo. Ni UJUHA na USHAMBA tu. Mhandisi si “title,” bali ni professional qualification na haiwezi kutangulia kabla ya jina, FULL STOP.
“TITLES” ZINGINE ZINAZOKUBALIKA
4. Kuna watu kama Reverend au Pastor (Mchungaji) kwa Wakristo ambao kazi zao zinawapa “titles” na pia Sheikh kwa Waislamu na Rabi kwa Wayahudi. Hawa RUKSA hata kama hatuwapendi.
5. Kuna JUSTICE kwa majaji, hii iko wazi na inakubalika, lakini hakimu hata kama amesoma sana na kufanya kazi kwa miaka 100, hapati kitu. Hii kitu hutolewa na Mkuu wa Nchi.
6. SENETA ama LORD au LADY ni hadhi za wanasiasa wanaofanya kazi kwenye mabunge ya juu (upper chamberof the House) kwenye nchi zao. Hizi zinatumika kabla ya jina, lakini MBUNGE haina fursa hii, bali inaweza kuwekwa mbele ya jina (suffix) kama MB au MP.
7. Kuna PROFESA. Hiki ni cheo cha kitaaluma kwenye chuo kikuu ambacho mtu hufikia kutokana na kufundisha, kufanya utafiti, kuchapisha na kufanya kazi kwa muda mrefu huku akipanda vyeo kuanzia uhadhiri usaidizi hadi uprofesa mshiriki ama uprofesa msaidizi na kisha PROFESA. Cheo hiki hakipaswi kuchanganywa na jina la kijumla wapewalo walimu wa vyuo Marekani la PROFESA, kama alivyokuwa Rais Barack Obama. Huyu hakuwa profesa wa cheo bali profesa kumaanisha mwalimu tu, kama ilivyo kwenye Kihispania ambapo mwalimu yoyote hata wa darasa la kwanza ni PROFESOR (“s” moja).
“TITLES” ZA HESHIMA
Tunaweza kutofautiana kuhusu uhalali wa “titles” za heshima lakini ukweli ni kwamba watu wamepewa na wanazitumia na hizi hazimsaidii mhandishi yeyote kutanguliza kidokezo MHANDISI kabla ya jina lake.
1. Kuna watu kama Mwalimu Julius Nyerere ambao walikubalika na “titles” za heshima ambazo hazipatikani kwenye jambo lolote lile. MWALIMU si “title” katika hali ya kawaida, bali ni heshima tu na anaweza kupewa binadamu mwingine.
2. MAALIM Seif Shariff Hamad amezoeleka kwa kisifa za MAALIM na sina maelezo alikipataje. Naamini ni heshima yake sasa.
3. Pia kuna watu kama DKT. Kenneth Kaunda ama DKT. Milton Apollo Obote ambao waliitwa hivyo kwa heshima tu lakini hawana sifa hiyo kifani wala kitaaluma. Viongozi hawa bahati mbaya hawakufanikiwa hata kupata shahada moja ya chuo kikuu katika maisha yao.
4. Mtanzania mwenye heshima ya kuitwa “DOCTOR” lakini bila kuwa na PhD ya darasani, ni SALIM AHMED SALIM ambaye ana shahada ya kwanza ya India na shahada ya uzamili ya Marekani. Ingawa ana shahada za udaktari wa heshima SITA, lakini hiyo si sababu ya kuitwa “DAKTARI” bali ni heshima aliyopewa duniani.
5. ALHAJ pia ni “title” ya kidini kwa mtu aliyekwenda Mecca kuhiji lakini sifahamu kwa nini wanaokwenda kuhiji Vatican ama Israel huwa hawana “title” hii.
6. MHESHIMIWA kwa wabunge, MTUKUFU kwa marais, MSTAHIKI kwa mameya, MWASHAMU mwa makadinari, na vingine vya Kiingereza, kama His Highness, au Prince of Wales, au her Majesty, na nyingine nyingi zinaingia katika kundi moja – HESHIMA kutokana madaraka. Hizi haziwasaidii wahandisi kuibua cha kwao.
7. NDUGU au COMRADE ni kundi moja na BW., BIBI, na BI au MR au MESSRS kwa wingi, MRS., MISS au MS, MDM kwa MADAM, n.k. zote hizi ni heshima kwa mshikaji yeyote. Nawashauri wahandisi wazichangmkie hizi kabla hazijaisha.
“TITLES” ZA UTANI NA MIZAHA
1. SIR GEORGE KAHAMA: Kwa utani tu, Mwalimu Nyerere alimpachika jina hili na hatimaye likashika hadi leo lakini ya kudumu. Ili uwe SIR kuna taratibu zake nchini Uingereza mpaka Malkia ama Mfalme akutunukie. Kahama wetu hakupitia humo.
2. PROFSA MAJI MAREFU: Na waganga wengine wengi wa kienyeji hujiita hivi kama mzaha wa kuvutia biashara na kila mtu anajua hili.
3. DOCTOR REMMY ONGARA: Ni jina alilojipa kimzaha kwa utani wake kwenye muziki na limeshika hivyo kama lilivyo.
4. JENERALI HEZEKIAH OCHUKA: Huyu alikuwa mwanajeshi wa Jeshi la Anga la Kenya asiye na cheo aliyeandaa na kufanya jaribio la kumpindia Rais Daniel arap Moi Agosti 1, 1982. Askari wenzake walimpenda na kumwita Jenerali hata kabla hajaleta zahma na kukimbilia Tanzania kwa ndege na mwenzake mmoja.
5. HIS EXCELLENCY, PRESIDENT FOR LIFE, FEILD MARSHAL, AL HADJI, DOCTOR IDI AMIN DADA, VC, DSO, MC, Conqueror of the British Empire in Africa in General and Uganda in Particular.Pamoja na vibweka vyake na kujipa majina haya, lakini Idi Amin alijua maana ya visifa vya baada ya jina (suffix) kuliko WAHANDISI wetu.
UHALALI WA “TITLES” YA “DOCTOR”
Ukiondoa watu waliogushi shahada zao za uzamifu, na kubakiza watu safi, bado mjadala wa nani ni “doctor”unabaki na pia iwapo “titles” hii inaweza kulinganishwa na “title” zingine. Chambua.
“TITLE” ITOKANAYO NA SHAHADA YA KWANZA
1. Kuna shahada mbili tu za kwanza duniani kote ambazo humpa mtu “title.” Bahati “title” hiyo ni moja tu: DAKTARI (Dkt) au DOCTOR (Dr) kwa Kiingereza. Nazo ni:
(a) Shahada ya Udaktari wa Utabibu, yaani Doctor of Medicine kwa Kiingereza au kwa Kilatini Medicinæ Doctor (MD), na hutolewa Tanzania huku Chuo Kikuu cha Colombia, Marekani, kikiwa kilianza kuitoa mwaka 1767. Shahada hii zamani kidogo nchini Tanzania ilijulikana kama MBBS ambayo ni kifupi cha Bachelor of Medicine & Bachelor of Surgery zote kwa pamoja. Jina jingine ni MBBCh, ambayo ni kifupi cha Kilatini kitupu,MedicinaeBaccalaureus, Baccalaureus Chirurgiae.
(b) Shahada ya Udaktari wa Meno, kwa Kiingereza, Doctor of Dental Surgery (DDS) kama kwetu Tanzania, au kwa jina jingine lolote kitakachoamua chuo husika, mathalani Bachelor of Dentistry (BDent) katika vyuo fulani Marekani.
2. Shahada za kwanzazifuatazo pamoja na kubeba kidokezo cha neno “utabibu” au “daktari” lakini haziwezi kumpa mtu hadhi ya kuitwa “Daktari.” Hizi ni:
(a) Bachelor Veterinary Medicine (BVM), mathalani ya Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Chuo Kikuu cha Cambridge, Uingereza. Ina majina mengine pia. Huchukua miaka mitano katika nchi nyingi kama si zote.
(b) Juris Doctor (JD) ambayo ni shahada ya kwanza ya sheria katika nchi kama Marekani ambako ni lazima kwanza uchukue shahada nyingine yoyote kabla ya kusomea JD Wamarekani wanaiita JD kuwa ni professional degree, yaani shahada ya fani. Katika nchi zingine kama Tanzania zinazofuata mfumo wa elimu wa Uingereza, shahada ya kwanza ya sheria huitwa LL.B, yaani Legum Baccalaureus, ambayo si lazima isindikwe na shahada nyingine kwanza, kama ilivyo India. Lakini zote huchukua miaka mitatu.
3. Swali linakuja, je, “daktari” maana yake ni nini? Neno hili la Kiswahili limetoka kwenye neno la Kiingereza “doctor’ ambalo nalo limetoka kwenye neno la Kilatini “doctoris” maana yake ikiwa ni “mwalimu.” Asili ya neno hili si utabibu bali ni ualimu. Kama ungalitafsiri cheo alichojipa Julius Nyerere cha “Mwalimu” kwa kutumia Kilatini, basi ungalimwita “Daktari.” Mjadala wa kwa nini watabibu huitwa madaktari huo siku nyingine.
4. Jambo la kuzingatia ama kufahamu hapa ni kwamba: HAKUNA ‘TITILE” YOYOTE NYINGINE DUNIANI INAYOZALIWA NA SHAHADA YA KWANZA.
“TITLE” ITOKANAYO NA SHAHADA YA UZAMIFU
Kuna shahada za aina mbili au tatu hiviza udaktari usiokuwa wa utabibu, yaani shahada za uzamifu, ambazo humpa mtu haki ya ‘title” ya kuitwa ‘Daktari” au “Doctor.” Nazo ni:
1. Shahada ya Uzamifu, yaani Udaktari wa Falsafa, au kwa Kiingereza Doctor of Philosophy au kwa Kilatini, Philosophiæ Doctor. Kwa kifupi ni Ph.D. Hii ni shahada ya kitaaluma, kwamba imebebwa na UTAFITI WA KITAALUMA (pure academic research) ikiambatana na UALIMU WA CHUO KIKU. Shahada hizi huweza kuwa katika fani mbalimbali, mathalani kwenye Kemia, Fizikia, Historia, Thiolojia, n.k.
2. Shahada ya Uzamifu, iitwayo Udaktari wa taaluma iliyosomewa. Mathalani, Udaktari wa Elimu, yaani Doctor of Education na kifupi chake cha EdD, au Udaktari wa Utawala wa Biashara, yaani Doctor of Business Administration au DBA. Hii ni shahada ya kifani (professional doctorate), kwamba imebebwa na UTAFITI WA FANI na haina shabaha ya kumwandaa mhitimu kuwa mwalimu wa chuo kikuu, bali kuwa mtaalamu kwenye fani husika. Shahada za utabibu wa binadamu pia zina heshima hii.
3. Hata hivyo, kuna shahada za udaktari chache ambazo ni za kitaaluma na si kifani lakini haziitwi PhD. Mfano ni Udaktari wa Sheria (Doctor of Laws) ambayo pia huitwa Doctor of Juridical Science, au kwa Kilatini Scientiae juridicae Doctor, SJD. Shahada hii ni lazima ije baada ya mhusika kuhitimu LLB au JD, na kisha LLM (shahada ya uzamili ya sheria, kwa Kilatini Legum Magistra).Lakini pia iwapo chuo kikuu kitaamua kuita Shahada ya Udaktari wa Falsafa katika Sheria (PhD in Law), hiyo itakuwa ni halali yake.Pia kuna Udaktari wa Sheria za Kanisa, yaani Doctor of Canon Law, kwa Kilatini Juris Canonici Doctor, JCD ambazo hutolewa kwa mapadri na sidhani kama wao hujiita madaktari lakini kitaaluma wanayo haki hiyo.
4. Jambo la kuzingatia hapa ni kwamba, wahitimu hawa wana HAKI ya kuitwa “DOCTOR” ama “DAKTARI,” mfano Dkt. John Pombe Magufuli. Lakini pia wengine hawatakimtindo huu, mfano, Marekani watu wengi wenye PhD, haundika majina yao bila kitangulizi (prefix) cha “DR” na kisha kuweka kihitimisho (suffix) mbele ya jina cha “PHD” kama hivi, Condoleezza Rice, PhD. Wengine hawafanyi chochote na hatuwezi kuwalazimisha. Kimsingi hata madaktari wa utabibu Marekani, tena wengi tu, huandika majina na kuweka “MD” mbele yake, mfano Sanjay Gupta, MD. Suala hapa ni HAKI ya “TITLE”
HAKUNA “TITLE” ITOKANAYO NA SHAHADA YA HESHIMA
Kuna shahada zitolewazo na vyuo vikuu duniani zijulikanazo kama Daktari wa Falsafa wa Heshima au Daktari wa Heshima, maarufu kamaHonoris Causa kwa Kilatini kumaanisha “for the sake of the honor.” Ziko katika makundi mawili. Hizi hazimpi mtu heshima ya kuitwa “DOCTOR” ama “DAKTARI.” Nazo ni:
1. Udaktari wa Heshima kutokana na mchango MKUBWA wa kitaaluma ama kifani. Hii pia huitwa Higher Doctorate na hutolewa baada ya mtu kuwa na shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) au ya Udaktari (Doctor of) kwenye fani husika. Shahada hii hutolewa kwa watu mahiri kwenye utafiti na uchapishaji kwenye majarida ya kitaaluma ambao kwa kweli hawapatikani kirahisi. Mfano wake ni Daktari wa Sayansi au Doctor of Science (SD au D.Sc) kwenye taaluma za sayansi asilia kama uhandisi, fizikia, kemia, utabibu, n.k. Pia Doctor of Humanities, au D.Hum kwenye taaluma nyingi zenye mchepuo wa sayansi ya jamii, bahati sina Kiswahili chake. Hali kadhalika, Doctor of Letters, au kwa Kilatini Litterarum Doctor, au D.Litt. kwenye taaluma zisizokuwa za sayansi asilia, ila nasikitika sina Kiswahili chake.
2. Udaktari wa Heshima kutoka na HESHIMA. Hizi ni maarufu kwa viongozi wa kisiasa kama marais, na watu wengine maarufu na zote ni za udaktari wowote kadri chuo kitakavyoamua. Zinaweza kuwa Doctor of ... mathalani aliyopata Rais Jakaya Kikwete hapa Marekani mwaka 2006 ya Doctor of Law; au PhD in ... mathalani aliyopata John Malecela mwka 1977 kutoka Chuo Kikuu cha Texas iliyoitwa PhD in Humanities.
3. Jambo la msingi hapa ni kwamba, hawa hawaitwi madaktari, hata wakihonga, hakuna hiyo. Utamaduni wetu Tanzania wa kuwaita wanasiasa wenye nazo eti “madaktari” ni ujuha ama ni kufanya mzaha.
Mdau, Washington DC.

unapoteza muda wewe NGWINI, ebo?
ReplyDeleteTutaendelea kuviweka hivyo visalamu Eng. Makau Bwao.
Michuzi,
ReplyDeleteMwambie mdau wako wa Washington kuwa title ya engineer ni halali na inajulikana kimataifa. Najua kuwa wamarekani huwa hawatumii title sana isipokuwa zile za kijeshi na za kisiasa kama Senator, President, Congressman, General, n.k.; ni mara chache sana wanatumia title za usomi za Dr. kama ilivyokuwa kwa Dr. Henry Kissinger lakini dada Condoleeza Rais akaitwa Secretary Condoleeza Rice badala ya Dr. Condoleeza Rice. Hivyo kwa huenda mdau wako wa marekani anadhani kwa vile kwao huko Injinia hatumii title ya Eng. basi ndiyo hivyo duniani kote, hapana, siyo hivyo.
Ingawa nakubaliana naye kwa mengine mengi lakini kwa hiyo ya injinia nadhani anawachukia mainjia kwa sababu zake tu. Hebu mwambie asome hii hii.
Pre-nominal letters are a title which is placed before the name of a person as distinct from a post-nominal title which is placed after the name. Examples of pre-nominal titles, for instance professional titles include: Doctor, Captain, Eur Ing (European Engineer), Ir (Ingenieur) and Professor; whilst other common social titles are Mr., Master, The Honorable, Ms., Mrs. and Miss. Pre-nominal letters are generally social, but can be professional in nature (e.g. Eur Ing).
Tunashukuru kwa upembuzi yakinifu... Lakini umemsahau dr Kikwete
ReplyDeleteHAHAHAHAH, SASA MA-ENGINEER UNATAKA KUWA-FRUSTRATE. WENZAKO WANAJENGA HESHIMA MTAANI WEWE UNAWAHARIBIA TENA!
ReplyDeleteDah we mkali, nahis ni mmoja wa wadhamili wa vyuo vikuu vya Marekani, swali langu moja tu kwako inaonekana ni msomi mwenye uelewa wa kueleweka kwanini usirudi nyumbani na kuisaidia nchi yako kwa hayo uliyonayo?. Hao marekani waliishaendelea miaka mingi iliyopita kwanin mnapenda kumlazimisha aliyeshiba wakati mwenye njaa yupo
ReplyDeleteRudi nyumbani uokoe jahaz la nchi yako
wahapa-hapa
Salamu kwa ma-injinia:
ReplyDeleteShowing off is the fool's idea of glory - Bruce Lee.
Nimetoka kusoma habari sasa hivi na imenichefua: eti Injinia Stella Manyanya kadakwa na Takukuru. Yaani hata kuandika Mhandisi inaonekana kama ni kuwashushia heshima hawa majuha?
ReplyDeleteHakuna cha injinia wala mhandisi, ni Bwana na Bibi na Bi. kama wakitaka Kimombo sawa, Mr, Mrs na Miss.
Waishie zao huko ni vijipembe mbuzi.
Haya mambo yako Tanzania tu. Sijasikia hata siku moja mhandisi eti imekuwa "title."
ReplyDeleteKwanza, nashangaa, kila mradi wa ujenzi Tanzania tunachukua wataalam kutoka nje. Hawa jamaa wako wapi kama wana utaalam huo basi?
Wengi wao ni washamba tu.
DAWA YA ENGINEER YOYOTE, MPE KAZI YA KUJIELEZA, TENA KWA WABONGO KAMA KUNA UNG'ENG'E NDIO UMESHAWAUA.
ReplyDeleteTUNAOMBA ENGINEER YEYOTE AJIBU SASA. HAKI HIIYA KUITWA KWA TAALUMA ZETU TUNAYO WACHACHE JAMANI.
DOCTOR.
Bwaba Matinyi,
ReplyDeleteKaka you killed it and you made my day na sina cha kuongeza. Ngoja niende jikoni kwenye fridge Nikachukue Heineken ya baridi nishushie huu ujumbe muruwa.
Mdau Green Belt, Maryland
Mie naenda kulala nikirudi hapa kesho patakua pamechimbika, hao kina Injinia Stella Manyanya na DK Salmin Amour watakumeza na mimi simoo!!
ReplyDeleteMdau DR Matunge, PhD in miziziology(Gamboshi-Mwanza)
Nawe ulikua na muda mwingi sana lakini naona unajikanyaga tena.
ReplyDeleteWameshasema ukiwa unaandika sio vibaya kama mtu unataka kutupa tittle zako zote ulizonazo, onyesha tu sio vibaya.. Lakini ikiwa kama ni salutation??!!!!! Mbona kazi ipo?????......"hello nurse Betty", "hey engineer Sherry", "vipi mambo police marwa", "hujambo mwalimu mkindi", "umelalaje advocate haule", "vipi mambo architecture William", "habari za kushinda messenger john", "tutaonana kesho secretary helena", "ulale salama train conductor Kimu", ", vipi mambo basi driver Edward", "huyu ni rafiki yangu mkulima Hassan", ..... heheheheh mbona kazi???Kutapitika huko mitaani kweli...???
Na mimi nataka mniite computer programmer Maggie au sijui niitwe computer engineer Maggie. Nilisoma watu wamesema kama una masters ya hiyo degree ndio unaweza kutumia hiyo title... Lahaula mbona kazi huko....
watu mnataka muitwe ma engineer wakati miundo mbinu choka sana. fanyeni kazi tuone...majumba ya kusisimua ya Frank Lloyd Wright tunayaona kila siku lakini huoni hata kitabu kimoja kinaweka sijui architecture Lloyd Wright .....Wanasema Frank Lloyd Wright was an architecture. Siye twapenda sifa kazi hatuwezi...
Ni kweli wabongo tunapenda sana ujiko na titles wakati upstairs (kichwani) ni sifuri. Mie huwa najiuliza hivi hizo titles zina nini hadi watu waghushi vyeti ili kuwa nazo.? Pia kwa mtazamo wangu hiyo title ni suffix na sio prefix na kamwe haibadili jina lako halisi kwa sababu ni kijisifa ulichopata ukubwani baada ya kufikia kiwango cha juu cha fani fulani na si vinginevyo.
ReplyDeleteAsante mdau wa Washington kwa uchambuzi yakinifu, wabongo tujifunze na tusipende sifa tusizostahihi!
Maelezo mreeeefuuuu, hadi yanachosha kusoma. Binafsi sijamalizia hadi mwisho kusoma maelezo yako, nimeishia kati tu.
ReplyDeleteYaelekea huwa unafeli sana mitihani wewe, coz hata kama mimi ndio ningekuwa mwalimu, nisingekuwa na muda wa kusoma hayo yote, tena ukizingatia kuwa uandikaji wako hauna mvuto.
Next time be short and precise.
YAWN, YAWN.
Umegonga mwake baba, mwenye masikio na asikie mwenye macho na ajionee. MAINJINIA WETU UCHWARA WATAKUMEZA OHOO shaurilo! Unajua kwanini nimesema mainjinia uchwara?
ReplyDeleteKwa sababu mbali ya kujivumbulia kamchezo kakujipa titles, hakuna LOLOTE LA MAANA WALILOKWISHAFANYA TANGU UDSM IUMBWE mpaka leo. Hebu watuonyeshe HIKI NDICHO KINACHOTUPA KIBURI YA SISI KUITWA MAINJINIA! TUONYESHENI UINJINIA WENU JAMANI JAPO KWA KUUNDA KIBAJAJI TUU! sio kazi kudesa tu na kujipa matitle!
Na huyo Injinia Manyanya si bora anyamaze tu maana huko Tanesco alikotoka kuko CHOPI! Hakuna jipya, tena basi wengi wanaopenda kujikweza ni Mainjinia walioko Tanesco!
Heri ya mimi fundi mchundo kazi yangu inaonekana!
Fundi Mchundo
Kweli nyie ni mangwini na wapiga domo. Yaani mnatumia nguvu kuuuuuuuuuuuuuubwa na maneno meeeeeeeeeeeeengi, kisa watu kujiita Eng. Fulani.
ReplyDeleteFuatilieni fani zenu kwanza za mapishi na wizi wa kura, ndo mje kwa wanaoijenga dunia.
Sasa, nawaambia hivi itawauma sana tena sana, sisi tunaendelea kujiita hivyo na hamna uwezo wa kuzuia hata muende wapi.
Nawe, wa ughaibuni nikuulize titles zingine kazileta Mungu??? Au ni makubaliano ya binadamu.
Nendeni mkachemshe chai mnywe acheni uvivu wa kufikiri; msitupotozee muda hapa. Sisi tuko bize sana, kwani tunakiwa tuhakikishe mnafasiri, mnaangalia TV, mnapiga simu, mnatumia kompyuta, mnapata mwanga n.k.
Tutaendelea kujiita sana, jinyongeni.
ENG. JUMA KAZIMOJA
we juma huna lolote ni injinia koko tu hamjawahivumbua kitu ni hayo majina tuu bure kabisa, hujawahi hata kutengeneza pasi achilia mbali tooth picks, subirini mainjinia wa ukweli wazungu ndo wavumbue ndo mkopi, vinginevyo bado nyie ni majuha dot com, bongo hakuna cha injinia wala akiteki ziro kabisa majengo mtindo wa kizaniiiiiiii no mvuto, uwezo mlio nao ni kujenga nyumba za njiwa juu ya paa la nyumba full stop!
ReplyDeleteMadau Wa Washingon DC,
ReplyDeleteUmeandika maelezo marefu bila vithibitisho (reference) yoyote!!!
Unataka tukuamini wewe kama nani wakati ambapo hata jina elimu/uzoefu au fani yako hujaweka?
Huenda wewe ni Prof/ Dr/ Mwalimu n.k uliyebobea kwenye mambo ya Sayansi ya Jamii n.k kwa nini usijitambulishe ili tuamini kuwa ulichoandika umekifanyia uchunguzi na sio hadithi za vijiweni DC.
Unataka wengine waliosomea fani zao miaka na miaka za Uhandisi wasitumie title bila ya kuwapinga kwa nondo za uhakika kuthibisha madai yako?
Bila ya vithibitisho (references) hiki ulichoandika hakina tofauti na hao unaojitahidi kuwakosoa.
Soames,
Reading, UK.
Jamani waacheni wenzenu wajiite Injinia Chumaulete wafurahishe nafsi zao!
ReplyDeleteENG JUMA KAZIMOJA,
ReplyDeleteNI KWELI WANASAYANSI NA MAINJINIA WA UKWELI WAKO BUSY DUNIANI KUHAKIKISHA DUNIA INAKWENDA MBELE NA HAWANA MUDA WA KUJIVIKA MATITLES ILI KAZI ZAO ZIJULIKANE!
Ila nyie mainjinia wa Bongo mnajua KAZIMOJA TU YA KUJIVIKA MATITLES, hakuna moja la ziada mnalolifanya, hebu tuambieni kazi zetu tulizounda ni hizi! Ama ndio hiyo KAZIMOJA inawatosha?
Tulipokua watoto hata mpishi wetu tulimwita Doctor kwa umahiri wake wa kupika vyakula. Je hii si halali?
ReplyDeleteDah!!, kumbe Matinyi naye ni punga namna hii. Ameandika kwa authority kama vile anajua sana wakati hajui kitu kabisa. Anapotosha sana watu kusema kuwa ni "Ni UJUHA na USHAMBA tu. Mhandisi si “title,” bali ni professional qualification na haiwezi kutangulia kabla ya jina, FULL STOP." bila kuwa amefanya utafiti wowote. Kwanza anasema uwongo kusema kuwa mhandisi ni professional qualification, kwani mhanidisi ni mtu ambaye professional qualification zake ni pamoja na digrii ya uhandisi na kuwa regisitered kwenye mamlaka inayotambulika kisheria.
ReplyDeleteMwandishi wako ameshindwa kutambua kuwa kuwa na elimu ya Engineering tu hakumfanyi mtu kuwa injinia na wala hawezi kujiita injinia hata kama ana digrii ngapi za engineering; ataruhusiwa kuonyesha digrii hizo baada ya jina lake (Post-nominal letters), kwa mfano, Issa Michuzi (B.Eng, M.Eng, M. Sc. Eng) na kadhalika. Mtu anakuwa Injinia tu akishatimiza masharti mengine na kuwa registered. Registration process inatofautiana kutoka sehemu hadi sehemu lakini ni kawaida sana kutambua injinia aliyekuwa registered sehemu yoyote. Baada ya kuwa registered, ndipo anaporuhusiwa kutumia title au Pre-nominal letters kabla ya jina lake. Hizi Pre-nominal letters zinatofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine, na kwa Tanzania wanatumia title ya Eng.
Jamaa yako angefanya utafiti kidogo tu hata pale Wikipedia tu angejua titles za mainjinia zikoje, na wala asikurupuka kuandika utumbo huo hapo juu. Vile vile kama angetaka kujidhihirisha kuwa yeye ni mwandishi makini, na kwa vile yuko Marekani angeulizia kwenye ofisi za bodi na jumuia mbali mbali na kihandisi kama vile ASME, IEEE, ASCE, AIChE, na kadhalika.
Kuruhusu watu wa namna hii kutumia globu yako kuandika vitu ambavyo havikufanyiwa utafiti na vinapotosha kunaweza kupunguza heshima ya globu hii ya jamii na kufanya kama vile ni ya kijiweni au ya kidaku ambapo watu wanatoa pumba zozote.
Ngoja nikutolee sehemu ndogo ya Pre-nominal letters au titles za mainjinia kama zilivyoorodheswa pale Wikipedia:
* Eng. is used for engineers in Egypt.
* Engr is used as a pre-nominal in Nigeria
* Eng is used as a pre-nominal in Uganda for registered engineers.
* Mohandess Payeh 1 and Mohandess Payeh 2 are titles used in Iran
* Ir is used as a pre-nominal in Hong Kong , Malaysia and Indonesia
* P.E.Jp as a pre-nominal in Japan
* Er. is used as a pre-nominal in India , Nepal and Singapore
* P.E. or Professional Engineer is used as a pre-nominal (similar to Dr. or Prof.) in Pakistan
* Mohandes is used as a pre-nominal in Arab countries like iraq ,syria and lebanon
* Eng. or .م as a pre-nominal in Jordan
* Engr. or Engineer is used as a pre-nominal in the Philippines
* Eur Ing, (EUR ING) (European Engineer) in Europe, used as a pre-nominal (similar to Dr. or Prof).
* Ing.P.Eur (European Professional Engineer) in Europe, used as a pre-nominal
* Ing. (Ingeniero) in Spain, used as a pre-nominal,
* Eng. (Engenheiro) in Portugal, used as a pre-nominal.
* Ing. EurEta - used as a pre-nominal (similar to Dr. or Prof).
* Ir. or Ing. in the Netherlands (pre-nominal letters)
* Ir. or Ing. in Belgium (pre-nominal letters)
* Ing. or Ing.jr in Italy (pre-nominal letters)
* Ing. in Romania, used as a pre-nominal (similar to Dr. or Prof.).
* Ing. for engineers in Czech Republic and Slovak republic, used as a pre-nominal (similar to Dr. or Prof.).
* inż. and mgr inż in Poland, (pre-nominal letters)
* маг. инж. (Mag. Inzh. from Magister (Master) Engineer) in Bulgaria (pre-nominal letters)
* "Inġ." in Malta
SIR GEORGE KAHAMA KWELI NI SIR. MI NILIBISHA KAMA WEWE BAADA YA KUSOMA KITABU KILICHOANDIKWA NA MWANAE NDIO UTAJUA KUWA KWELI NI SIR, MPAKA PICHA ZIMEWEKWA ZA SIKU ALIYOPATA HIYO TITLE. KWA HIYO NYERERE SI SABABU YA KAHAMA KUITWA SIR. BALI NI KWELI YEYE NI SIR.
ReplyDeleteEti ma-injinia wabongo hamjagundua kitu! We kweli hamnazo, juha namba moja wa leo.Inaonekana wewe na maswahiba zako hamjui hata mhandisi anapatikana kwa kupitia hatua zipi na wala hamjui kazi za wahandisi ni zipi. Yaani kwa hili ninyi ni ziro kabisaaaaaaaa.
ReplyDeleteSijui hiyo taaluma yako (ambayo huruhusiwi kuweka pre-fix) imesaidiaje kuondoa umasikini na ujinga katika familia yako, ukoo wako, kijiji chako, wilaya yako hadi Taifa lako.
Kwa taarifa yako, taaluma yako haina mchango wowote katika Taifa hili, imeshindwa. Na haina mvuto kuweka jina la utangulizi kama 'Eng.'.
Kwa hakika inavutia sana, kutamka jina 'Engineer.....' au 'Mhandisi...)
Ongeleeni taaluma zenu kama hamtaki jinyongeni; sisi tunasonga mbele na lazima mtuite hivyo.
Eng. Juma Kazimoja
BORA UMEMSAIDIA HUYO MASKINI WA TAARIFA NA MVIVU WA KUTAFITI.
ReplyDeleteWakati JK akitangaza timu yake pya baada ya kashfa ya Richmond 'kupindua' serikali mmoja kati ya ya wateuliwa alikuwa 'Engineer Chiza' na alimwita Eng.
ReplyDeleteMjadala huu hautaisha.
ReplyDeleteWatu wanapaswa kurejea darasa kamilifu la itifaki na protokali za matumizi ya majina ya makundi na au visifa vitangulizi au vya mishoni vya kitaaluma na vya heshima. Yaani hiyo yenyewe ni fani ya kufikia hadi uzamivu.
Yaani Wikipedia tu itapwaya sana hapa.
Niseme kuwa kuwa 'Engineer' inaweza kabisa kukubalika kuwa 'Title'. Na kuna nchi nyingi tu zinaitambua hivyo baada ya kuhitimu shahada husika na pia kusajiriwa katika bodi husika tena sehemu nyingine uzoefu wa kazi wa muda fulani huwa pia unahitajika na wengine wako makini kuzitimia title hizo wasivuke mpaka ya maeneo waliyosajiriwa!
KINACHOGOMBA NI NINI SASA?
1. Watu hatuna shule au uelewa wa itifaki gani inayotumika TANZANIA katika matumizi ya hizo 'titles' na 'abbreviations' zake na zinapotakiwa kuwekwa mwanzo au mwisho na pia zaidi wakati gani / mahala gani pa kuzitumia. Na zikitumika majina ya mtu yatajwe ki vipi.
Ningekuwa na uwezo ningewasambazia kitabu kimoja cha Robert kiitwacho 'Honour & Respect' kwa kuanzia tu mpate vionjo!
Kutokana na kuwa na uelewa mdogo na ama kutoelekezwa kwa msisitizo na taasisi husika namna ya kutumia hizo 'titles' basi watu hukurupuka katika matumizi ya hizo 'titles'.
Mfano: Kuna utofauti katika kujitambulisha kwenye busn cards, au tuandikapo barua za kikazi au maandiko ya kitaaluma au unapoitambulisha kampuni yako na kuweka jina lako na taaluma yako (kwa ajili ya wateja kujua sifa yako ili yumkini mtu ashawishike na matarajio ya ubora wa huduma ya Uhandisi wako). Lakini ni kituko au wengine wanasema ushamba (katika uelewa wa itifaki husika) mara nyingi kutumia 'titles' kama hizo katika 'salutations' yaani salamu au kumtaja au kumwita mtu hususani katika mazingira ya kawaida au kirafiki au katika mikusanyiko ya kijamii ambayo si ya kitaaluma. Ndiposa wengine wanafikiri kuwa watu wa nchi fulani hawapendi kutumia 'title' zao la hasha wanapenda sana ISIPOKUWA WANAZITUMIA KWA KUFUATA PROTOKALI HUSIKA!
Mifano michache:
a. Mfano ni kituko kama nina Ph.D halafu niko uwanjani nacheza mpira na mtangazaji anasema "Dr. Maji Marefu ana mpira, la Dr. anatoa pande la nguvu n.k " au unakutana na rafiki yako unaruka juu na kumwamkia ukisema "habari za leo Mhasibu, Masanja, CPA zehemu zote!"
Aidha ni kichekesho, Mstahiki Meya, kumkaribisha mjumbe wake kwenye baraza lake akisema, "ebu tumsikilize Mheshimiwa, Muuguzi Msajiriwa Bi, Nashu".
b. Ni ajabu kumwita mke wa Rais wetu, Mrs. Jakaya unatakiwa uandike Mrs. Kikwete (endapo hutaki kutaja jinale)!
c. Kwa sababu Uhandisi na hata Uhasibu pia ni 'titles' za kitaaluma, kwa mujibu wa sheria, Makampuni na asasi na hata idara za serikali sasa zinakuwa makini kuunda majina ya nyadhifa za wakuu wa idara husika. Yaani badala ya kusema 'Mhandisi wa idara ya ujenzi' mnamwita 'Meneja wa idara ya ujenzi' au 'Msimamizi Mkuu', au 'Mfawidhi wa Idara' maana wapo wengi tu lakini hawajawa na sifa za kitaaluma kuitwa Wahandisi. Vile vile Taasisi nyingi mfano za dini na NGO'S/ CBO's n.k zinakuwa makini na kuanza kuwaita wakuu wa idara zao za uhasibu kama Wahazini au Watunza Fedha au Meneja wa Fedha n.k kuliko kumwita Mhasibu (Accountant) ambapo unalazimishwa na sheria ya bodi uonyeshe nondo za shule na ya usajiri wake n.k
Mjadala huu umekuwa mzuri sana pamoja na yote yaliyosemwa, tufikirie changamoto moja ya nguvu kuwa je hizi 'titles'zina maana yeyote au zina athari yeyote katika mustakabali wa nchi yetu?
ReplyDeleteUtashangaa nitakapokujibu kuwa NDIYO NDIYO NDIYO KABISA!
Inapokuja katika shughuli rasmi, katika taaluma,katika masoko, katika biashara, katika huduma, katika ajira, usicheze kabisa, hizo 'titles' hazina maana ya kutafuta ujiko bali zinatumika kuwajulisha Waajiri, kuwajulisha walaji (Consumers), kuwajulisha wanafunzi wanaoelekea katika taaluma hiyo, kuwatambulisha wanachama wasajiriwa katika bodi husika za udhibiti na ithibati (accreditation) ya taaluma zao kadha wa kadha.
Si bure wenzetu wa EU ilibidi wakutane na kuweka utaratibu wa utambuzi wa 'titles' hizo katika nchi wanachama. Mmesikia pia the Bonn Agreement of 1994 (Ujerumani & Spain) n.k. Yaani hata sisi inabidi tuangalie je 'title' ya Udaktari wa Binadamu na nyinginezo, je zinaendana na kiwango sawa cha elimu katika nchi zote mwanachama wa EAC!
Msilete mchezo na hili suala hata kidogo.
Mimi na rafiki yangu sote tumehitimu Udaktari wa Falsafa chuo kimoja na katika fani moja, mwaka mmoja. Mimi nimerudi Bongo naendelea kutambulika 'Senior Lecturer' wakati mwenzangu Mu- Indonesia anaitwa Professor huko kwao! Hawezi kutambuliwa hivyo hakija hapa kwetu!
Lazima kuwepo na Taasisi husika zinazohimiza na kusimamia matumizi ya visifa hivi kwa kutoa maelekezo ya itifaki yake na pia kuvithibitisha inapobidi vinginevyo tusianze kulia kila mtu anagombea ubunge kwa kujitambulisha Dr. kwa kusema kuwa haijalishi wakati hivyo viherufi viwili na kituo chake tu vinaweza kuwa ndio kigezo tofautishi cha ama kumpa kura mmoja na kumwacha mwingine!
Tukiendelea hata Media huwa zinakuwa na itifaki zao za uandishi na uchapaji wanapotaja rejea hususani majina na visifa vya wahusika mfano tuwe na Michuzi style, Tz Govn't Press style, IPP media Style n.k, !
Somo la Ififaki & Protokali za Visifa linaendelea!
Washington DC tuko Watanzania zaidi ya 1,000. Jamaa aliyeandika hakutaja jina lake. Kuna sababu gani na haki gani ya watu kumtaja jina kwa kubahatisha?
ReplyDeleteHakujitaja basi, si muache tu?
Ila nakubaliana naye kwamba kweli hakuna title ya Injinia na ndiyo maana kwenye miaka ya nyuma hakukuwa na kioja hiki.
Hiyo mifano ya nchi alizoweka mdau mmoja hapo, ni upuuzi ule ule kama aliosema mwandishi. Hakuna title ya Engineer duniani.
Kama ipo, kwa nini watu wabishane?
Kuanzia sasa mhandisi mwenye akili atakuwa akijiita hivyo roho inamsuta, na akiona wamekaa watu wenye akili zao, lazima atakwepa.
ReplyDeleteUzuri wa ujinga ni kama ushamba, huwa haujifichi.
Hakuna engineer anayeweza kujibu hii. Hakuna.
ReplyDeleteacheni unyambilisi nyie na mambo ya title, PhD ndo baba na mama lao linapowekwa on top of the professional title kama tunazunguzumia academic achievement, titles zenye degree ya kwanza tu ni za kutafuta recognition in the professional society i.e doctor (MD), Eng, RN, CPA Judge, mkulima XX n.k
ReplyDeleteIEEE-USA recognizes that the title, “Engineer,” has a multiplicity of meanings within the
ReplyDeletecontext of laws of various U.S. jurisdictions. All jurisdictions protect the titles “Professional
Engineer”, “Licensed Engineer,” “Registered Engineer,” or some variation thereof, to refer to
individuals licensed in those jurisdictions to practice engineering. In addition, some jurisdictions
protect the title, “Engineer,” with no qualifying words added. The purpose of protecting these
titles is to ensure that the public can easily identify those individuals who possess the requisite
skill, knowledge and competence to protect public safety, health and welfare in the practice of
engineering. Generally, the public interprets the term, “Engineer,” to mean a person who is
qualified to practice engineering by reason of special knowledge and use of the mathematical,
physical and engineering sciences, and the principles and methods of engineering analysis and
design, acquired by engineering education and engineering experience.
It is our position that the title, “Engineer,” and its derivatives should be reserved for those
individuals whose education and experience qualify them to practice in a manner that protects
public safety and advances the health and prosperity of the public. Strict use of the title serves
the interest of both the IEEE-USA and the public by providing a recognized designation by
which those qualified to practice engineering may be identified. Such qualification is evidenced
by graduation with an engineering degree from an ABET/EAC accredited program of
engineering education (or equivalent*) and adherence to an applicable code of ethics in any
jurisdiction, and/or licensure as a Professional Engineer.
Soma hapa:http://www.ieeeusa.org/policy/positions/engineertitle.pdf
Michuzi asante kwa kuruhusu mijadala kama hii. Bigup Mumbogo nimekukubali. Je unaweza kutujuza tukupateje utupe somo hili la Itifaki zaidi!
ReplyDeleteMichuzi nakushukuru tena kwa blogu hii tunahitaji watu wanaotoa changamoto za namna hii.
DR.ricky,,,,lol,,,i know very much football
ReplyDelete