Habari za kazi Ankal,
Jina langu ni Benjamin, mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu Dortmund Ujerumani. Nimesoma katika tovuti yako habari yenye kichwa:- JE, “ENGINEER” NI TITLE KAMA ZILIVYO DOCTOR NA PROFESSOR?.

Hili ni jambo ambalo hata mimi niliwahi kujiuliza siku moja, ila nilipopata nafasi ya kuja kusoma hapa Ujerumani nikagundua kuwa wajerumani Engineer ni title kama title zingine. Jambo la ajabu zaidi hapa Ujerumani mtu anapoandika title yake kwa mfano kama ni Professor huwa hataji professor pekee, hapa watu hutaja elimu zao zote! mfano Pro. Dr. Eng. Dip James Johannes. Hii maana yake huyu mtu alisoma diploma kisha akasoma Engineering, kisha akasoma PhD, na mwisho akawa professor.
Wajerumani husema wanataja elimu zote kwa sababu kusoma elimu ya juu hakufuti elimu yake ya awali mfano elimu ya Diploma. Ujerumani Diploma inaheshimika sana kwani wao walikuwa hawana mfumo wa degree ambao umeanza siku za hivi karibuni, hapa ujerumani diploma ni sawa na degree.

Hivyo mimi sioni ajabu ma-Engineer wetu wanapotaka waitwe kwa hiyo title.

Ninakutakia kazi njema.
Ni mimi msomaji wa tovuti yako.
Benjamin kutoka Ujerumani.
-----------------------------------------------------
KAKA ISSA MIMI NAISHI NORWAY. HUKU BWANA BILA HATA KUANDIKA MANENO MENGI HATA RAISI WAO HAITWI MHESHIMIWA. MKUU WA CHUO NILICHO KUWA NASOMA NA WADOKTA, PROFESA WOTE WALIITWA KWA MAJINA YAO TENA YA MWANZO NA SIO YA UKOO. WAZIRI WAO AKIHOJIWA KWENYE TV AU RADIO WANAMWITA , MF "WEWE JOHN UNONAJE JUHUSU HII HOJA" . HUKU BWANA UKITAKA UJULIKANE WEWE NI MKUBWA, MSOMI N.K TAFADHALI FANYA KAZI, VUMBUA MAMBO, FANYA MABADILIKO BASI WATU WAJUE , *AMEWEZA KWASABABU NI INGINIA AU DOKTA. *KWA KIFUPI WASOMI WETU BONGO WACHAPE KAZI KAMA INAVYO TEGEMEWA NA SIO KUJIPACHIKA MATITLE.
MDAU
MARY AABERG.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Mdau wa ujerumani nafikiri umechanganyikiwa.Chungwa siyo chenza ila yote ni matunda.Kule nyumbani kulikuwa na usemi unaosema "advanced diploma is equivalent to degree".Na wewe unatuambia kuwa diploma ni sawa na digree.Kama hivi vitu vingekuwa sawa au equivalent basi vingetumia jina moja.Kwanini viwe na majina mawili tofauti.Inamaana waliotoa hayo majina walishindwa kuona hiyo equivalence/similarity.Kwahiyo ndugu zangu wenye advanced diploma au diploma ya ujerumani mtambue kuwa hamjapata degree bado na wala ninyi siyo graduates.Mrudi shule kupata degree.

    ReplyDelete
  2. GYNAECOLOGIST MUME WANGU, MIKANJUNI TANGAAugust 07, 2010

    Kuanzia sasa na mimi mniite/mnitambue kwa taaluma NILIYOISOMEA KWA SHIDA hadi nikafaulu na sasa naihudumia jamii kwa bidii zangu zote.

    GYNAECOLOGIST MUME WANGU

    ReplyDelete
  3. The president of united states is a professor of law but i have never heard from united states media addressing him as prof obama. in the states there are so many profs,docs and eng. but people dont give a damn about their academic achievement, they only use these tittles when they are working in academic sector (i.e teaching), here in tanzania we have the so called "educated people" who can't even express themselves in a simple english.

    ReplyDelete
  4. True say mdau..
    Nafikiri mdau alieanzisha huu mjadara hakufanya research ya kutosha.
    nimesoma China na sasa niko Japan,all these countries i have seen engineers are addressed the same way by there titles.mfano Dr.Lim Eng. Thiong.
    utaona pamoja na kuwa ana doctrate degree lakini professional status yake is indicated,ingawa iko kati.
    na basically huyu mtu ukimwambia ajitambulisha ata jitambulisha as: Lim Eng. Theong.
    hivyo hakuna makosa katika hili maana ni profession yake.
    gues yule mdau si engineer so he is trying to hate.

    Eng.*****
    Japan

    ReplyDelete
  5. Bwana Benja hicho unachoongelea wewe kinaitwa credidentials ambazo huwekwa chini ya jina la mhusika mfano kwenye official letter ama buzness card. Suala la kujiita tittle before the real name only exist in Bongo na kuna katabia kengine kila mtu sasa hivi bongo ni Dk hata kama huo udokta ni wa heshima, please this need to stop
    Mdau dc, maryland and virginia aka DMV

    ReplyDelete
  6. A Professional Engineer,Engineer is an engineer who is registered or licensed within certain jurisdictions to offer professional services directly to the public.

    ReplyDelete
  7. na mimi ni:
    dk. masters. sociologist. bachelor. adv level. o level, primary. chekechea. yaliyomo yamo.

    ReplyDelete
  8. Anko na wadau wenzangu, mimi kama mbongo mtu mzima niliye-drop college hapa US and A, nasema hivi: (kwa kuhate kidogo sababu yalinishinda), kama wewe ni mwanataaluma lakini sio DAKTARI WA WATU aka BINADAMU, yaani Dr. so and so, katika maongezi ya kila siku na mbele za watu, huna sababu yoyote ile ya kuweka eng, lawyer fulani na prefix nyingine zisizo na maana kabla ya jina lako au kutaka watu wakuite hivyo sababu unaamini ndo utapata heshima kama msomi mbele za watu. Sit your butt down and try to achieve something!!

    Kwani anko Michu huyu DC wa Tegeta ana udaktari gani au upfrofesa gani? Mbona kila siku watanzania laki kadhaa kama si milioni kadhaa kila siku tunaanzia kwake kujua anasemaje anko wetu huyu kipenzi? Je ametaka kuitwa Dr Michu? No! Prof Michu? No! Social engineer Michu? No! How about Dr, Prof, Soc. Eng, Tegeta DC Michu kama huyo mdau wa kwa Schroeder anavyopendekeza??? Wala!

    Wabongo wasomi popote mlipo, just close your lips and do something to earn our respect sio kudai kupewa hadhi tu kama hakuna cha maana mnafanya zaidi ya kupamba kuta zenu na vyeti

    Mdau, Dallas, TX

    ReplyDelete
  9. mdau wa hii article in Germany they call it diplom na sio diploma

    ReplyDelete
  10. Kuandika title mfano Juma (PhD), Eng. Juma, Advocate Juma, n.k. kwenye official documents is OK ugomvi wetu ni kujiita titles ambazo kama hujazitaja unalaumiwa na kuonekana wewe ni kama umemdharau huyo mtu. Hata anapojitambulisha kanisani/msikitini lazima aanze kwa kusema mimi naitwa Eng Juma, Prof. Juma, Advocate Juma, Mheshimiwa Mbunge Juma, n.k. it is rediculous!! Mimi naitwa Professor .... Ina maana usipotamka hiyo title ndiyo utaonekana hujasoma? Mimi niko Norway kwenye University kwa miaka karibu 5 sasa huwa sijawahi kuona kitu kama hicho. Watu wanaitana kwa majina yao ya mwanzo mfano Juma, Joseph, Stig, n.k. Wakati hao watu either ni wahandisi, maprofessor, madaktari, n.k. Ndiyo huo uhandisi wako utaisha? Nadhani ni kutafuta kulazimisha mambo.
    Mdau wa Norway

    ReplyDelete
  11. Nchi nyingi nilizotembelea watu huwa wanataja elimu yao katika business cards zao.

    Lakini tanzania ndio tanzania, mtu unakwenda ofisi kwa mtu au nyumbani kwa mtu na unaona ameninginiza certifacte ya primary school!

    ReplyDelete
  12. Mdogo wangu anaendesha daladala na kwa muda wote mimi namuhisabu kama ni pilot kwa sababu nae anasafirisha abiria kama walivyo warusha ndege au waendeshao meli. Na full title yake ni Captain mpo hapo?.

    ReplyDelete
  13. watanzania tumerogwa na nani jamaniii? baada ya kujadili mambo ya kujenga nchi kazi kujadili mambo yasiyo hata na faida baada ya kupata jibu kwani naona kipofu anamuuliza kipofu mwenzie njia.

    wenzetu wanajadili maendeleo ya nchi kutoka hatua moja kwenda nyingine ss ni kujadili ujingaaa. kwani mtu akijiita Eng, prof, mwl, mwathirika tatizo nn?

    kuna watu hapa hata hawajui chaki ya kuandikia inatengenezwa na nini, tuwe wachunguzi wa vitu vya maana na siyo umbea umbea tu majungu.

    ReplyDelete
  14. AndendekesamoAugust 07, 2010

    Mdau uliyetoa mada hii, kwanza mimi binafsi sijali kabisa kama watu bongo wakijiita Engineer James Johannes au wasipojiita, haiongezi damu wala kupunguza maji katika maisha ya watanzania.

    Pili, kutaka mfumo huo uanzishwe hapa Bongo, unatakiwa uje na hoja yenye akili, na wala siyo "Ujerumani wanafanya hivi"; Kwa sababu sisi siyo wajerumani na wala hatuishi ujerumani, na "U-ujerumani" siyo kipimo cha ubinadamu wetu.

    Tatu, kama wewe ni Engineer, basi utumie U-"engineer" wako kutatua matatizo sugu katika jamii yetu, kama vile upatikanaji wa maji safi, umeme wa kuaminika, kubuni vitendea kazi bora na kuboresha visivyokuwa bora, kubuni na kuanzisha ajira mpya kwa wale ambao hawajabahatika kuwa "Engineer" kama wewe, n.k.

    Ukifanya mambo hayo, hata usipojiita hiyo "tittle" ya Engineer, sisi tutakutambua tuu na kukuheshimu kama wewe ni Engineer wetu.
    Kujiita Engineer na kutegemea ajira za wawekezaji tuu, kama vodacom, barick gold, BP, na wengineo; wakati "ziro ubunifu"; inawezekana tittle inayokufaa ni "employable" James Johannes, rather than "Engineer" James Johannes.

    ReplyDelete
  15. Watanzania bwana kazi yao kulalamika tu bila sababu. Engineering ni Title msidhani mchezo km ilikuwa rahisi ngekimbilia history na kiswahili. Engineer aliyekamilika lazima atangulize hiyo Eng kwenye jina lake na hawa ni wale wenye vibali toka Engineers Registration Board na wanatambulika kimataifa kwa namba zao za usajili. Wewe na Bsc, Msc naPhd yako umesajiliwa wapi? Hawa ni watu wakuheshimu km Madaktari ambao wanakula viapo maalumu kwa ajili ya fani zao iwe wanyama au binadamu. Mnaniudhi sana jaribu tuone km mnaweza.

    ReplyDelete
  16. WABONGO NDOO ZETU, TUNAFURAHIA KUITWA MAJINA MAKUWA KULIKO MAJUKUMU TULIYO NAYO. ENGINEER KAZINI NA SIO USWAHILINI. NDIO MAANA TUNAO MAPROFESSOR WENGI LAKINI HAKUNA KINACHO FANYIKA. NDIO NI HAKI KUITWA ENGINEER, PROFESSOR, DR ETC LAKINI TATIZO KAMA ANAVYO SEMA MJUMBE HAPO JUU NI UWEZO WAKO WA KUDHITITISHA KUWA WEWE NI ENGINEER AU PROFESSOR AU DR. TUSIONE TUU KAMA TATIIZO NI MAENGINEER TUU HATA VYEO VYA ACADEMIC KATIKA JAMII VINA MAANA YAKE JAPO WATU WENYE NAVYO WAMEVIVAA TUU KAMA MIWANI ILI WAKAE VITI VYA MBELE .

    ReplyDelete
  17. lazima tutofautiane bana. kama wewe engineer ruksa kuandika au kujitaja ,kama dr. ruksa pia kama mganga wa kienyeji ruksa pia na kama hukwenda shule rudi ukasome afu ukimaliza jiite na wewe kulingana na proffessional yako. Allah nyie mnadhani nyanga mchezo?
    NIMEFUNGA MJADALA. SIRUDI NG'O

    ReplyDelete
  18. Watu wanawaogopa mainjia (magwin) ...nendeni mkasome na nyie muwe mainjia . FOE oyeeeee!

    ReplyDelete
  19. YES ni ujuzi

    Engr AAAA BBBB

    Mrs Engr AAAA BBBB
    au sijui ni
    Engr Mrs AAAA BBBB

    mie napenda wa west africa wanajua kujivunia walichopanda masomoni hata kwenye news
    utasikia Engineer AAAA BBBB

    ndivyo inavyotakiwa kujivunia ulichopanda mwenyewe

    LOL
    mwalimu
    atakuwa

    Teacher AAAA BBBB?????

    ReplyDelete
  20. Wadau mnaendelea kujichanganya kuhusu status ya mtu au title, ukiangalia kwa marekani mtu huitwa kulingana na status yake unakuta mtu mmoja ana status zaidi ya moja, kama Obama ni Law professor na ni rais ila anajulikana kama President Obama. Na ukiangalia kama Senators huitwa kwa utangulizi kama Senator Makein, au Congressman so and so hivyo huitwa kwa wadhifa wao sioni kuendelea kulumbana kama wewe haujisikii kumwita mtu kulingana na title yake mwuite kwa jina lake wala hakutakuwa na ugomvi hapo. Je swali baba yako au mama yako unawaita kwa majina yao? Jaribu kumwita baba yako kwa jina lake uone itakuaje italeta ugomvi na utaonekana hauna adabu wewe! Chukulia mifano hiyo midogo nafikiri topic hii ingeishia hapa kwani naona watu wengi wanaendelea kuchemsha. Asanteni kwa debate.
    Mdau USA.

    ReplyDelete
  21. HAYA MAMBO YA TITLE YAPO LAKINI YA UTARATIBU WAKE, KWA MFANO DOCTOR SI SAHIHI KUMUUITA MTU MWENYE PhD AMBAYO I YA UDAKITARI WA BINADAMU MAHALA AMBAPO SI SHULE DOCTOR WA FANI ZINGINE NIKIMAANISHA PhD AMBAZO SI ZA UTIBABU MAHALA POPOTE DUNIANI HUITWA HIVYO AKIWA KATIKA MASWALA YA ACADEMIC KWA MFANO AKITOWA MJADALA WA FANI YAKE, DARASANI MAENEO YA CHUO UNAWEZA KUMUITA DOCTOR LAKINI NJE YA HAPO MITAANI INALETA CONFUSION KWANI WATU WENGI WAME-ASSOCIATE DOCTOR NA MEDICAL DOCTOR NA NI MEDICAL DOCTOR TU AMBAYE MAHALA POPOTE DUNIANI ANAWEZA KUJITAMBULISHA HIVYO AU KUITWA HIVYO HATA AWE WA CHETI HAIJALISHI NI WA NGAZI GANI NI HII NI KWA SABABU KUNA ASUMPTION THAT DOCTOR HUWAGA HANA OFISI ANAWEZA KUFANYA KAZI MAHALA POPOTE PALE KWA MFANO MKIWA SAFARINI DOCTOR ANAWEZA KUSAIDIA ENDAPO KUTATOKEA MGONJWA GHAFULA. HAPO HAPO TRADITIONALLY MGANGA WA MENO ALIKUWA HAITWI DOCTO HUITWA SIMPLY DENTIST. KUHUSU PROFESSOR, PROFESSOR NI RANK KATIKA UALIMU WA KUANZIA SENDARY HADI UNIVERSITY WALA HAUSOMEWINA HAUNA CHETI NI HATUA TU MTU AMEFIKIA BAADA YA KUFUNDISHA KWA MUDA MREFU NA KUPANDA RANKS HADI KUFIKIA U-PROFESSOR NA HUO NI MTU ALIYEBOBEA KATIKA FANI YAKE AMEANDIKA NA KUTAFITI MAMBO MENGI KATIKA FANI AKE NA WALA SI LAZIMA AWE NA DEGREE KUNA WAALIMU WENGI NIMEWAONA HAWANA GEREE NA NI MAPROFESSOR WANA DIPLOMA NA WENGINE NI VYETI TU NA HII NI TITLE LAKINI PhD SI TITLE NA TITLE HUKOMA PALE TU MTU ANAPOACHA KAZI ILE KWA KUSTAAFU AU KUAMIA KAZI INGINE KWA MFANO HUWEZI KUENDELEA KUMUITA MTU PROFESSOR KAMA AMEACHA KUFUNDISHA KWANI KWA TAFSIRI NYEPESI PROFESSOR NI MWALIMU AMBAYE ANAENDELEA KUFUNDISHA NA AMEFIKIA RANK HIYO NA DEGREE, VYETI NA DIPLOMA ZINGINE ZOTE NI CREDENTIALS MARA NYINGI HUANDKIWA MBELE YA JINA NA SI MWANZO WA JINA UNAWZA KUTUMIA DR JUMA MWANZO WA JINA KAMA WEWE NI WA BINADAMU, UNAWEZA KUTUMIA PROFESSOR JUMA KAMA WEWE BADO NI MWALIMU UNAFUNDISHA SWALA DIPLOMA KUWA SAWA NA DEGREE HILO LIPO NCHI NYINGI TU IKIWEPO NA TANZANIA, LIPO USA, CANADA, UK NA MAHALA PENGI TU DUNIANI HALINA UBISHI HAPA WANASEMA SAWA YAANI EQUIVALENT HAWASEMI NI DEGREE LAKINI HUWA ZINA UZITO SAWA NA ZINGNE NI ZAIDI YA DEGREE KWA UZITO WAKE NA ZIKO NYINGI TU DUNIANI. NA MWALIMU SI RANK NI TITLE YA KAZI NA MWALIMU PIA HUWA ANA EXCEPTIONAL YAKE ANAWEZA KUENDELEA KUITWA MWALI HATA KAMA AKISTAAFU KWA VILE KUNA ASUMPTION KUWA ANAWEZA KUENDELEA KUFUNDISHA HATA AKIWA NYUMBANI KWAKE KATIKA MAISHA YAKE YA KAWAIDA LAKINI HUWEZI KUMUITA KWA NGAZI ALIYOACHIA KAZI UNAMWITA MWALIMU TU HUWEZI KUSEMA SENIRO LECTURER JUMA WAKATI AMESTAAFU ITAKUWA KICHEKESHO VILE VILE HUWEZI KUJIITA EMBASSOR JUMA WAKATI UMEACHA KUWA BAOZI HAILETI MAANA YOYOTE

    ReplyDelete
  22. Nchi yetu tusipoangalia vizazi vijavyo kuna kiza kinene mbeleni, Watu wanajiita whole bunch of fake names just to please themselves, Mfano sasa hivi kuna watu katika siasa utasikia ooh Rais wa Bariadi Mara ooh Rais wa Mvomero maaan I'm sick of this bogus names na tusipowaonya mtakuja kujiita Mungu watu before your real names.
    Please go do something productive and stop bitching Tanzanians
    Mdau, D dot C

    ReplyDelete
  23. Oyaa fanyeni uvumbuzi muwekwe kwenye historia ya nchi, watu kazi kujipachika mi taito wakati carrier zenyewe zero kazi ukihiyo tu na vyuo uncredited vya online kama ingekua hivyo basi pasingetosha hapa maana mimi ni tapeli by profession.Mbona mapharmasist hatuwasikii wakijitaja mi taito yao before there names c'mon people let's be serious ndo maana wakenya wanatucheka sehemu yoyote ile duniani

    ReplyDelete
  24. Candid ScopeAugust 07, 2010

    Kabla ya kupitia hizo degree zisemwazo niliona labda kuna cha pekee huko lakini sasa kumbe ni blabla tu na kudanganya watu kwa vifupisho vya DR. horn. nk. Wangapi tuna hizo degree lakini hazitufikishi na kuonyesha kazi na matunda yake. Kama ni Rhetorics hata babu yangu alikuwa nayo.

    Heshima ya mtu si kiwango cha elimu ila uwezo alio nao. Kwani wengi wana elimu lakini hawajaelimika. Kusoma si kuelimika ila inasaidia kuelimika kwa wachache wenye himaya ya hulka ya kuelimika.

    Nilifanikiwa kutembelea makumbusho ya watu mashuhuri mbalimbali duniani akiwemo Thomas Edison wa Marekani huko West Orange City, NJ.
    Thomas Edison alivumbua makubwa mengi ikiwemo kugundua hizi bulb za umeme tutumiazo leo na hata kitanda cha bango na shuka alizolalia usiku pale pale kiwandani pake zingali hadi leo, hakuwa doctor wala cheti cha degree kilichotundikwa ukutani ila akili ya ugunduzi tu ilivyofanya kazi ndo imemtilia umaarufu huo.

    Watanzania na waafrika tujifunze kuchapa kazi, ugunduzi na utendaji katika maisha na jamii zetu badala ya kuegemea tu heshima za kutundika makaratazi ukutani yasiyotenda kitu.

    Kumbuka kuwa hizo degree unazochuchumia ni kwamba unasomelea tu mawazo ya mtu fulani alivyopangilia, je we huwezi kuwa mtundu wa kuandaa ya kwako ili wengine nao waumize vichwa kuchukulia degree mawazo yako in future?

    ReplyDelete
  25. Nitachangia kama ifuatavyo: Kwanza ninadhani hizi title,eng.,dr. wa mifugo na miti shamba pia siyo jambo baya.Lakini ni muhimu jamii ikubali , kuhakiki ni taaluma gani na viwango vipi vipewe hizi title(Criteria). Kwa mfano, kuitwa Engineer Mwita inatakiwa umesimamia miradi ya barabara kubwa 5 kuanzia mwanzo mpaka mwisho, ndipo upewe title hiyo. Hii ita watia moyo graduates wa taaluma ya engineering watie bidii kufikia level ya kuitwa eng. fulani. Hali kadhalika kwa wanasheria,Waalimu,wapishi n.k.

    Pili, si lazima tufuate Criteria za mataifa mengine kuwapa title wanataaluma wetu. Title zifuate mazingira ya Tanzania na vipaumbele vyetu.

    Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika!
    Mdau, Manassas, Virginia

    ReplyDelete
  26. Vipi maengineer ndio wameonekana wa kushambuliwa? Vipi 'waheshimiwa', 'madaktari (wa kutibu watu, wa kutibu mifugo na wenye PhD), hao wajiite watakavyo?
    Watanzania shida ni kuwa kila mambo yakienda kombo mnataka kuwalaumu wahandisi. kuhalalisha mnaibuka na hoja za wenzetu hawafanyi hivyo au wenzetu wanafanya vile. Hapo bongo watu mtaani wanatambulishwa kama baba fulani na mama fulani kwa kuwahusisha na watoto wao. Nchi nyingine zinafanya hivyo? Tuache kufanya hivyo?
    Acheni kuiga bila kutafakari.

    ReplyDelete
  27. MDAU ULIYECHANGIA MADA WA KWANZA NAHISI UNA AUTISM NA KAMA HUNA BASI LEARNING DISABILITY LAZIMA ITAKUWA IMEKUPITIA KARIBU,WANAOSEMA ADV.DIPLOMA NI EQUIVALENT TO DEGREE HAWAKUWA WAPUMBAVU KAMA WEWE,MIJITU MINGINE BWANA KWA KUJIFANYA INAJUA,INGEKUWA SIO SAWA HATA KIDOGO BASI WATU WASINGE RUHUSIWA KWENDA LEVEL NYINGINE KAMA ZA MASTERS BAADA YA KUFANYA ADV.DIPLOMA...KICHWA CHAKO.

    ReplyDelete
  28. Jamani acheni kujichanganya mnaosema Obama hajiiiti professor kwa vile ni raisi sasa hivi sio kweli hata akimaliza uraisi wake hawezi kujiita professor kwa vile hana phd...Hili neno ni latin word na Europeans na Americans wanatumia kwa njia tofauti sasa west meets east ndio kunakua clash of the titans...."in America a professor is a title given to a much larger group of senior teachers in two- and four-year colleges and universities"
    na most of the times hao maprofessor ambao wana masters tu kama wanafundisha shule ya miaka minne huwa wanafundisha mwaka wa kwanza na wa pili tu au ndio wengi wako kenye hizi community colleges na wote wanaitwa professors. Ila wakati wa kuanza darasa (semester) ndio huyo mwalimu lazima awape credential zake zote..anawaambia kuwa yeye ni PhD holder au ana master tu..Lakini mimi nakumbuka sijawahi kufundishwa na mwalimu mwenye masters tu mwaka wa tatu na wa nne...

    ReplyDelete
  29. Sat Aug 07, 10:14:00 PM, Mtoa Maoni: think before you write. ati adv diploma ni equivalent to degree...heheeeehh sikubaliani na wewe kabisa ...just becuse kuna nchi zingine zinakupa credits na kuwaive basi usilinganishe hivyo vitu. Ina maana form VI ni sawa na form six...kwa vile kuna watu wamemaliza form four bongo nawakaanza universities nchi za nje. Sasa utasema kwa vile wamekubaliwa kuingia basi form four ni sawa na form six? Na au utasema post graduate ni sawa na graduate degree? noooooo kima umesomea marekani nadhani unaelewa angalia watu wanavyochanganyikiwa wakati wa final audit...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...