HABARI TOKA JIMBO LA MTERA LINASEMA MGOMBEA LIVINGSTONE LUSINDE AMEMSHINDA MH. JOHN SAMWEL MALECELA KATIKA KURA ZA MAONI NA ANATEGEMEA KUWA NDIYE ATAYEPITISHWA KUGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CCM KWA JIMBO HILO, KWA MUJIBU WA MATOKEO YALIYOTANGAZWA SAA 4 LEO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Uhuni mtupu! Saa nne haijafika? Mzee usinibanie

    Kingwalu

    ReplyDelete
  2. MZEE MALECELA USIJALI MAMA ATAKUWA MJENGONI NEXT TIME HIVYO DODOMA UKATAKWENDA WAKATI WA VIKAO VYA BUNGE KUKAA NA MAMA HOTELINI. LAKINI NDIYO HIVYO MAMA AKIWA MJENGONI WEWE UTAKUWA HOTEL ROOM UNAANGALIA BUNGE KWENYE RUNINGA.

    ReplyDelete
  3. DU! DUME LA NG'OMBE LIMEANGUSHWA SAFARI HII TENA NDANI YA CHAMA CHAKE. HII SI MCHEZO

    ReplyDelete
  4. HUO NDIYO UNAITWA MSUMARI WA MWISHO.

    ReplyDelete
  5. Mzee mzima pole sana!! Tutakulinda ndani ya chama kama mwenzio Msekwa, kuwa mpole mama asijepata sababu ya....!!!

    ReplyDelete
  6. fair play!!

    ReplyDelete
  7. YAMEKWISHA

    ReplyDelete
  8. Watanzania sasa tunaanza kubadilika. Sasa tunaanza kuelewa kwamba siasa za Tanzania hazina hati miliki. Yeyote mwenye uwezo (wa pesa au sera??!!) anaweza kushiriki. Prof Sarungi, Mailingi, Mungai, Makweta, kwaherini. Tunawatakia ustaafu wenye furaha. Wengine mlioponea chupu chupu akina Wasira, Mongela,Ana Makinda na wengine ambao tumekuwa tukiwasikia toka enzi za mwalimu, kwa mtini jifunzeni. Mnataka mng'atuke kwa kung'atuliwa au ka hiari yenu? Igeni mfano wa Mzindakaya na Paul Kimiti.

    ReplyDelete
  9. DAWA YA VIZEE KAMA HIVI NI KUVIUMBUA KWA MATOKEO MATAMU NAMNA HII NA BADO HATA MKEWE KULE SAME ATIE MAJI KICHWANI WEMBE NI ULE ULE,TENA MWAKA HUU CHADEMA FULL KUCHANUA,KWA DALILI HIZI SISHANGAI HATA KIKWETE KUKUBALI MATOKEO YA URAISI HAPO OCTOBER.
    VIVA VIJANA VIVA CHADEMA

    ReplyDelete
  10. wasipowang'oa vingunge wao tutawangoa sisi!Chadema wakae tayari kwa wazee wasiokubalika waliobaki!
    huu wakati wa vijana bana!

    ReplyDelete
  11. LIVINGSTONE LUSINDE ni mtoto (au mjukuu) wa Job Lusinde au wana u-ndugu?

    ReplyDelete
  12. Mzee alisahau kama amekuwa na umri mkubwa,kwani haoni ni aibu kwake kuwa bungeni na watoto wadogo akina January wamemsikia tangu wamezaliwa bungeni hadi leo hii waende wakabishane humohumo bungeni,hii ni fedheha kwa wazee wa umri kama wake kung'ang'ania viti achieni vijana jamani,Mzee umechoka sasa kapumzike.tumia Tv kuona bunge linaendeleaje si lazima uwepo na wewe,Mweee!

    ReplyDelete
  13. Ni vizuri mzee kakubali kushindwa hiyo bado ni heshima pia. Hongera Mzee Sam kwa utumishi wa muda mrefu na ulitukuka kwa jimbo la mtera

    ReplyDelete
  14. Pole sana babu yangu. Nakujua wewe ni mpiganaji mzuri katika kulitetea taifa hili. Basi baki kuwa mshauri mkuu wa vijana kwenye medani ya siasa. Pole sana lakini nina imani ukomavu ulionao kisiasa hilo sio tatizo sana.
    Pole na mapumziko mema kwenye ustaafu. Tuna pamoja na wewe katika kipindi hiki kigumu cha mpito.
    Mdau

    ReplyDelete
  15. Usijali mzee tingatinga tumia muda huu kuchonga barabara ya urais 2015. Wewe bado embe changa kabisa!!!!!

    ReplyDelete
  16. KingangitiAugust 04, 2010

    Nadhani tumeona mabadiliko yanakuja na kuchukua kasi yake.Ule usemi wa kilatino "Ubi mayor minor cesat" unatoweka taratibu na hili ni dalili kwamba sio muda mrefu tutakuwa na wakuu wa nchi zetu waafrika kama kina Obama.Wazee wasihofu kujitoa wenyewe katika siasa au madaraka mbalimbali waamini tu wataishi vizuri la msingi ni kutenda yote kwa kujali maslahi ya umma mwishoni basi unaambiwa,' Vema mtumishi mwema namwaminifu...." Lakini ukiongoza kwa maslahi yako utakiona tu.hayeni!

    ReplyDelete
  17. KingangitiAugust 04, 2010

    Ila kweli inauma sana 'my wife' ndani mi 'nje' tunakutakia uvumilivu baba.Taratiiibu utazoea la msingi akitoka mjengoni we mzidishie malovee! hakiharibiki kitu.Tunakupenda sana Concellor wetu OUT, e baba!

    ReplyDelete
  18. Malecela wamemuonea tu ....
    Kwani mjengoni watu wanabeba zege?

    ReplyDelete
  19. Ingekua ni busara saana kwa wale waliobaki wakajichukulia nafasi muafaka kwao kuliko kungoja kuabishwa na vijana!! Nafasi zilizopo ni pamoja na MSHAURI WA VIJANA, MJUMBE WA CHAMA, MSHAURI MASWALA YA UCHUMI WA NCHI Pamoja na NAFASI NYINGINE NYINGI!! Hapa Nadhani wangeweza kutunza heshima zao!! Lakini Sasa wabongo tulivyokua ving'ang'a! mh!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...