Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume akifungua mkutano wa siku tatu wa Kikanda wa Kimataifa wa kukabiliana na ugaidi na uhalifu wa kimataifa leo. Mkutano huo unaendelea katika Hotel ya Golden Tulip na unahudhuriwa na Majaji kutoka ndani na nje ya Tanzania.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume (kulia) akishiriki kuimba wimbo wa taifa wa Tanzania wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa Kikanda wa Kimataifa wa kukabiliana na ugaidi na uhalifu wa kimataifa leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Augustino Ramadhani. Mkutano huo unaendelea katika Hotel ya Golden Tulip na unahudhuriwa na Majaji kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Washiriki wa mkutano wa siku tatu wa Kikanda wa Kimataifa wa kukabiliana na ugaidi na uhalifu wa kimataifa unaendelea nchini Tanzania wakimsililiza Rais Amani Abeid Karume wakati wa sherehe fupi za ufunguzi uliofanyika katika Hotel ya Golden Tulip na kuhudhuriwa na Majaji kutoka ndani na nje ya Tanzania.

(Picha na Tiganya Vincent-Globu ya Jamii)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. hivi mbona marais wa nchi nyengine hawana jamaa hao wa nguo za kijani nyuma yao?

    au sisi bado tumo usingizini?

    ReplyDelete
  2. Waheshimiwa majai mnapokaa hapo golden Tulip muje na makubaliano ya pamoja ili taaluma yenu iheshimike. Mtoe ushauri kwa nchi za Kiafrika ziache kukaidi agizo la mahakama ya kimataifa, limshauri Omar Hassan Al Bashir, kama na uhakika kuwa yuko innocent basi na achukue likizo yake aombe kusindikizwa na kiongozi maarufu kama Mzee Madiba afike kule wamfungulie shtaka wamwachie kwa dhamana arudi nchini kwake akaendelee na kazi

    ReplyDelete
  3. Mungu akubariki sana jaji wetu mkuu. he is such a gift to our legal system.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...