Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid
Karume akiwa ni miongoni mwa Viongozi wa Nchi za SADC akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa siku mbili unaohusu masuala mbali mbali ya Kiuchumi na Kijamii,uliofanyika katika ukumbi wa Safari Court Hotel nchini Namibia,(kushoto) Rais wa Afrika Kusini Jacob Gedleyihlekisa Zuma.
Rais wa Malawi Prof Bingu Wa Mutharika akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika,Rais wa DR Congo Mh. Joseph Kabila,wakati wa Mkutano wa siku mbili kwa Nchi za SADC ambao pia pia uandhimisha miaka 30 tokea kuundwa kwa jumuiya hiyo.
Rais wa Malawi Prof Bingu Wa Mutharika akitoa hutuba yake wakati wa mkutano wa siku mbili Nchi za SADC unaoendelea Nchini Namibia.
Marais wa Nchi Mbali mbali wakiisimama wkati wa Wimbo wa Taifa za Nchi kbla ya kuanza kwa mkutao wa Jumuiya ya SADC nchini Namibia.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Shadya Karume,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Namibia Mh. Sam Nujoma wakati wa Mkutano wa Nchi za SADC nchini Namibia.
Waziri Nchi Afisi ya Rais anaeshuhulikia Fedha na Uchumi,Zanzibar Dk. Mwinyihaji Makame, akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mh. Mohammed Aboud wakati wa Mkutano huo
Washiriki katika mkutano huo toka nchi mbali mbali za SADC.
Wake za Marais wa Nchi za Jumuiya ya SADC,pamoja na Marais wastaafu wa Jumuiya hiyo kwa pamoja na washiriki wengine wa Mkutano wa siku mbili wa jumuiya hiyo
Marais wastaafu wa Jumuiya hiyo kwa pamoja na washiriki wengine wa Mkutano wa siku mbili wa jumuiya hiyo,wakifuatilia kwa makini,matukio mbali mbali yanayoendelea katika ukumbi wa Safari Court Hotel.
Wake za Marais wa Nchi za Jumuiya ya SADC,pamoja na Marais wastaafu wa Jumuiya hiyo kwa pamoja na washiriki wengine wa Mkutano wa siku mbili wa jumuiya hiyo,wakifuatilia kwa makini,matukio mbali mbali yanayoendelea katika ukumbi wa Safari Court Hotel.
Wanafunzi wa Secondary School walioshinda Insha zinazoelezea masula a ya SADC,wakia na vyeti vyao baada ya kukabidhia na Rais Kabil,(kushoto) ni Chresencia Stephen Marwa kutoka Tanzania na Incinon Adaiano Ganga kutoka Angola wakiwa katika ukumbi wa Mkutano wa SADC,Safari Court Hotel.
Mwenyekiti Mpya wa SADC,Rais wa Namibia Hifikepunye Pohamba akitoa hutuba yake baada ya kuwa Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya hiyo,katika Ukmbi wa Mkutano wa siku mbili,uliofanyika Safari Court Hotel,Nchini Nambia,pia mkutano huo unadhimisha miaka 30 tokea kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi wakuu wa Nchi za SADC walioshiriki Mkutano wa Siku mbili uliofanyika Nchini Namibia,katika Ukumbi wa Mikutano wa Safari Court Hotel,Nchini Namibia,Rais karume anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. michuzi tumekushtukia unajikomba kwa chadema,mbona habari ya mbunge wao kuhamia cuf umeibania,alafu habari za cuf hutoi kabisa.kulikoni

    ReplyDelete
  2. Kaunda anaonekana yuko vile vile tu, miaka nenda rudi. Sura ile ile staili ya nywele, nguo zile zile. Kuna watu wamejaaliwa kweli dunia hii..

    ReplyDelete
  3. hivi mama shadya umesahau kama huu ni mwezi mtukufu na kujistiri ni wajibu? si naskia wewe ni hajjat kulikoni. tumuogope Allah subhana wataala.

    ReplyDelete
  4. Kwanini Joseph Kabila hutaki General Defao kurudi DRC?nilifikiri utakumbuka mzee kabira alivyokaa uhamishoni kwa muda mrefu sana kwetu Tanzania, wewe umezaliwa pale nilifikiri unajua uchungu wa raia kuhamishwa nchi yake na mamulaka fulani, labda kwako haikuwashida sana kwani wakongo wansema wewe ni mutusi sio mkongo, je ni kweli? mruhusu Defao kurudi kongo huyu hawezi kukudhuru hata siku moja.
    Mdau uk

    ReplyDelete
  5. Eh hii kweli mpya? sasa jamani VIPI KARUME ATAMWAKILISHA JK? KWANI KARUME ANA WADHIFA GANI AU ILE YAKHE NISAIDIE LEO TU RAFIKI YANGU SIO SUALA LA SHERIA? NAOMBA ELIMU HAPO.PILI MZEE JK AFRIKA AHHH HAKUTAKI LAKINI WASHINGTON -DALLAS -COPENHAGEN,OSLO HAPO HUMWAMBII KITU ILA TARIME-TABORA - BUKOBA HUKO MUACHIE DR.SHEIN

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...