
Warembo wa Ilala,Temeke na Kinondoni wakiwa wameshikilia tuzo zao mara baada ya kukabidhiwa na wadhamini wao katika hafla ya kuwapongeza walimbwende hao ambao wanaingia katika kambi ya Miss Tanzania hivi karibuni.

Meneja wa kilaji cha Redd's Original ,Kabula Nshimo akimkabidhi tuzo Miss Ilala 2010,Bahati Chande katika hafla ya kuwapongeza warembo hao iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika hotel ya Movenpic jijini Dar.

Meneja wa kilaji cha Kilimanjaro,George Kavishe akimpa tuzo Miss Temeke,Geneviva Emmanuel

Meneja Mawasiliano wa TBL,Edith Mushi (kulia) akimpa tuzo Miss Kinondoni 2010,Alice Lushiku katika hafla ya kuwapongeza warembo hao wanaojiunga na kambi ya Miss Tz hivi karibuni iliyoandalia na TBL kupitia kilaji chake cha Redd's Original ambacho ni kinywaji rasmi cha Vodacom Miss Tanzania katika hotel ya Movenpic usiku wa kuamkia leo.kati ni Miss Temeke,Geneviva Emmanuel

Wadau wa Frontline Management limited ,Nancy Sumari (shoto) na Irene Kiwia wakishoo love.

Da' Asia Idarous (pili shoto) akiwa na super model,Fidel Iranga (pili kulia) wakishoo love na meneja wa kilaji cha Redd's Original,Kabula Nshimo (kulia) pamoja na mdau George.

Wadau wa TBL katika picha ya pamoja.


Wageni waalikwa wakifuatilia shughuli hiyo huku wakibadilishana mawazo mawili matatu.
kwa picha zaid za hafla hii
BOFYA HAPA.
Huyo super model heshima...sijui nimewasahau mabinti wabongo..maana nilipoondoka ..walikua wanavutia .. ila huyu super modoooooo.... damn!
ReplyDeleteGeorge, nakusalimia tu (huyo George aliyoko na mamaa wa mitindo).
ReplyDeleteHawa models kwa kweli ni wazuri.
ReplyDelete