Marehemu Levis Msillo Lyaruu
KUZALIWA 17-04-1954
KUFARIKI 14-08-2010

Familia ya Marehemu LEVIS MSILLO LYARUU wa Oysterbay Dar es Salaam inasikitika kutangaza kifo cha baba yao mpendwa LEVIS MSILLO LYARUU kilichotokea 14/08/2010 katika hospitali ya Regency Upanga jijini Dar es Salaam.

Ibada ya kuaga mwili wa marehemu itafanyika kanisa la MT. PETRO OYSTERBAY DAR ES SALAAM kuanzia saa sita mchana tarehe 18/08/2010
Ibada ya mazishi itafanyika kanisa la MT. BERNADETHA, POROKIA YA KILEMA 19/08/2010 na kufuatiwa na mazishi nyumbani kwa marehemu IMMI Ngagu Kilema Moshi.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe
Amina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. R.I.P Levis

    ReplyDelete
  2. We will miss you so much Bro, ucheshi wako kaka. Mungu aliyekuumba akakuleta duniani na kutuunganisha na wewe, sasa anakuhitaji katika ufalme wake, hakuna wa kumpinga. R.I P Brother

    Tutakupenda daima!!
    Bk.

    ReplyDelete
  3. pole sana comfort,
    mungu awape nguvu wewe na mama yako ktk kipindi hiki kigumu...

    ReplyDelete
  4. Sisi tulikupenda sana lakini mwenyezi mungu amekupenda zaidi.

    Upumzike kwa Amani Kaka yetu mpendwa LEVIS

    ReplyDelete
  5. La kifo kweli hakina subira. Huyu jamaa alikuwa mcheshi kwa kila mtu, jamani. Namkumbuka nilisoma naya Livingstone Secondary (now Kigoma Secondary). Huko alitokea kujifunza kuongea Kizaire , mpaka anafariki najua kuna watu walikuwa wanadhani ni M Congo,kumbe mchaga wa watu maskini. PAPA LEVIS kende malamu(Nenda salama) nasi tuko nyuma yako. Tokoya, Nzambe liboso.

    ReplyDelete
  6. Familia ya Mbine Shayo tunawapa Pole familia ya Mzee wetu Levis na uvumilivu hasa katika kipindi hiki kigumu cha Msiba. Daima tutamkumbuka na kumwombea.
    Mungu amlaze Mahala Pema.

    ReplyDelete
  7. Shemeji Asante kwa kazi uliyonifanyia wakati wa uhai wako sina cha kukulipa ila nakuombea mapumziko mema mpaka tutakapo onana tena siku hiyo isiyokua na jina.

    Ni kweli Shemeji sisi tulikupenda (pamoja na Dada yako) kwa ucheshi wako na utani wako kwa kweli ilikuwa ni furaha kuwa na wewe lakini Mungu amekupenda zaidi na sasa Ngoja tukusindikize kwenye safari yako ya mwisho KILEMA.

    Mungu akulaze mahali pema Shemeji.

    Ruwa Aichi.

    Aminaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...