


TIMU YA TAIFA YA CRICKET JANA IMEMALIZA RASMI MICHEZO YAKE YA KUJIPIMA NGUVU HAPA NCHINI UINGEREZA JANA, NA KUTEMBELEWA NA MAOFISA KUTOKA UBALOZI NA, MSTAHIKI MAYOR WA MJI WA WATFORD. IKIWA HAPA NCHINI UINGEREZA TIMU YETU ILIWEZA KUSHINDA MECHI MBILI, NA KUPOTEZA MCHEZO MMOJA. MICHEZO HIYO ILIKUWA NI MOJA SEHEMU YA MAANDALIZI YA MICHUANO ITAKAYOANZA WIKI IJAYO NCHINI ITALIA. WAWAKILISHI WETU HAO WAMEALIKWA RASMI KUTEMBELEA OFISI ZA UBALOZI WETU SIKU YA JUMATATU KABLA YA KUANZA SAFARI YAO TAREHE 18/08/2010 KUELEKEZA ITALIA. PICHA NA HABARI NA MDAU RASHIDI DILUNGA WA UBALOZI WETU LONDON.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...