akiwa na mchezaji wa Seattle Sounders
Wachezaji wa Twiga Stars wakisaini vitabu vya
mashabiki baada ya mchezo wao na Seattle Sounders
Kipa wa pili wa Twiga Stars Maimuna Saidi akitia saini
Picha ya pamoja wachezaji wa Twiga Stars na Seattle Sounders
Twiga Stars usiku wa kuamkia leo wamecheza na timu ya Seattle Sounders ya wanawake katika mchezo wa kusisimua ambapo wageni walifungwa bao 4-2 katika uwanja wa Starfire Sports Complex jijini Tukwila, WA, nchini Marekani, mbele ya mashabiki wa Seattle Sounders fans na Watanzania wanaoishi maeneo hayo.
Sounders ndio walioanza kupata bao dakika ya sita na kupata la pili dakika chache baadaye. Dakika 40 ya mchezo Twiga walikuwa wameshafungwa bao 3-o, lakini wakarejesha moja kabla ya mapumziko kupitia kwa winga wake machachari Mwanahamisi Omary kwa kona iliyoenda wavuni moja kwa moja.
Kipindi cha pili Sounders walianza kwa nguvu na kupata bao la nne baada ya kipa wa Twiga Stars kutema mkwaju mkali ambao mfungaji aliuatia na kufunga. Asha 'Mwalala' Rashidi alifunga bao la pili kwa kichwa baada ya kona safi ya Eto Mlenzi.

MICHUZI TAFADHALI ANGALIA SANA HABARI ZINAZOKUJA MEZANI KWAKO TUTAANZA KUKUKIMBIA SASA,SASA HABARI KAMA HII HAIJITOSHELEZI KABISA SEATTLE SOUNDERS NI TEAM YA WAPI?NA HUO MCHEZO UMEFANYIKA WAPI?NA LINI?...KWA FAIDA YA WATU KAMA SISI TUSIOJUA HIYO SEATTLE SOUNDERS UNATUELEZA NINI KHAAAA.
ReplyDeleteMDAU ULIYETOA MAONI HAPO JUU. SINA KAWAIDA YA KUINGIA HAPA ILA LEO IMEBIDI ILI WATU KAMA WEWE MJIFUNZE SUBIRA NA KUSOMA HABARI KAMILI KABLA YA KUTOA MAONI AMBAYO HAYANA NIA NJEMA KAMA YAKO. AIDHA HAKUNA ANAYEKUZUIA KUKIMBIA ENDAPO UNAKUWA NA JAZBA HATA KABLA HABARI HUJAISOMA VYEMA NA KUROPOKA.
ReplyDeleteNAOMBA KUKUULIZA NI KIPI KATI YA HIVYO UNAVYODAI HAKIPO? KWA FAIDA YAKO BINAFSI NAKUWEKEA TENA PARAGRAPH YA KWANZA HUENDA KWA JAZBA YAKO HUKUISOMA. POLE SANA KWA INDA ILIYOKUJAA NA AGENDA YAKO ISIYO YA SIRI YA KUTAKA KUTOA WATU RAHA. ILA NAFURAHI UMETUMIA UHURU WAKO WA MAWAZO BAADA YA (BILA SHAKA) KUANZA KUJUA NAMNA YA KUTOA MAONI. NAKUPENDA NA KUKUHESHIMU SANA. WALA SINA KINYONGO.
-MICHUZI
Twiga Stars usiku wa kuamkia leo wamecheza na timu ya Seattle Sounders ya wanawake katika mchezo wa kusisimua ambapo wageni walifungwa bao 4-2 katika uwanja wa Starfire Sports Complex jijini Tukwila, WA, nchini Marekani, mbele ya mashabiki wa Seattle Sounders fans na Watanzania wanaoishi maeneo hayo.
Sawa nawapongeza Twinga kwa mazoezi mazuri wanayofanya. Lakini mdau uliyeleta habari au uliyetaka kuboresha habari, ninachotaka kujua, je Twiga nio walikuwa wenyeji wa timu ya Seattle Sounders au mwenyejki nani, maana hapa unasema Wenyeji washindwa 2-4
ReplyDeleteKibonde japokuwa ijumaa kwenye kipindi cha Jaazi ulikuwa unajifagilia kuwa kitambi chako ni cha mzoezi, nafikiri bado unahitaji kuonana na 'dietician, japokuwa kwa bongo wanapatikana kwa shida sana, ili upunguze kitambi lchako zaidi maana linakuja kwa kasi ya ajabu.
ReplyDeleteNkyabo - Bongo
Huyo mdau wa kwanza KICHWA PANZI sio kosa lake, umekurupuka ka bao la kwanza ka sio mkojo wa asubuhi.
ReplyDeleteWA stands for washington state fool.
Habari inaeleweka hiyo, next time ukila jani usikimbilie kwenye net instead kimbilia kwenye kupiga box au ukale vumbi
Kwa hakika Twiga stars imejitahidi sana, na haya maandalizi yataisaidia katika mashindano yajayo ya Africa, maana Twiga stars ndio wawakilishi pekee katika ukanda wetu wa Afrika mashariki na kati.
ReplyDeletePongezi nyingi kwa Mkwasa na timu pia maafisa na wafadhili pia.
Michu,
ReplyDeleteHakukuwa na haja ya kumjibu huyu jamaa. Tatizo watu wengine huingia humu tayari wameshapiga ka dirinki so wanabakia kuropoka tu.
Hii Timu anaimudu kocha Rogatian Kaijage tu kwa sasa.Ukweli ndio huo.
ReplyDeleteAnno wa kwanza nakushauri jifunze kwanza mfumo wa kujua uandishi wa habari hapo utajua kuelewa habari ziandikwazo.
ReplyDeleteMtuma habari hii katika paragraph ya kwanza ameandika kila litakiwalo kulielewa na haihitaji ufafanuzi zaidi, vinginevyo tukupe somo la kuelewa journal writting ili tukurahisishie urahisi wa uelewa wa uandishi wa habari. Mwandishi kajibu maswali yote muhimu matano ambayo ungeelewa hungeuliza hilo, ila maswali yote yamejibiwa katika sentensi moja na ambayo inaunda paragrafu moja tu.
Pili labda tatizo kuelewa jiografia huenda hujui Seatle jiji la Marekani lililoko katika state ya Washington kaskazini ya state ya Kalifonia, nchini Marekani ndiko mchezo ulikochezwa. Nimejaribu kukusaidia kuelewa kidogo.
Asante
Tuwasiliane wachezaji wa timu ya Twiga na mimi ninependa sana kujiunga. Napenda sana kucheza mpira wa miguu. Naomba tuwasiliane kwa hii email mwaipopog1980@yahoo.com.
ReplyDeleteNaishi North Carolina-USA