Ankal akiwa na mdau Eric David Nampesya wa BBC wakiendeleza libeneke
Baadhi ya wasanii wakiwa nyuma ya jukwaa kabla ya kunda mmoja mmoja kuburudisha

Sir Juma Nature na watu wake wakighani mistari

Chege (shoto) na Mheshimiwa Temba wakiwajibika mbele ya maelefu ya wakazi wa Mwanza wakati wa mkutano wa kampeni wa JK Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza



Msanii Diamond akifanya vitu vyake

Pailkuwa hapatoshi
Wasanii waliotoa burudani katika picha ya pamoja baada ya kupeana mikono na JK ambaye hakuficha kusema kwamba yeye ni mpenzi sana wa Bongo Fleva na kwamba ingawa hachezi anasikiliza sana midundo yao na ameahidi kuwasaidia. Kwanza ameshaleta mtambo wa kisasa wa kurekodia na kufanya mixing wenye thamani ya dola elfu 50, amewapatia nyumba ya studio na wataalamu wa kufundisha mainjinia wa sauti wako njiani. Vile vile ametoa milioni 20 kuwapatia wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuandaa mkakati wa jinsi ya kuwasaidia wasanii wa muziki na filamu kuwa na uwezo wa kusambaza kazi zao na kupata faida ya kuvuna jasho lao, badala ya hali ilivyo sasa ambapo wafanyabiashara wanatawala soko na kuacha wasanii wakiumia na wachache kuneemeka kwa kazi zao
Msanii Dokii (kijani) akiwa na kundi la Flora Mbasha ambalo lilitia fora sana kwenye mkutano huu wa kampeni








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. mimi kama ningekuwa na uwezo wa kumuona live raisi wetu we acha tu yaani ana moyo sana na katunyanyuwa wa tz mtake msitake songa mbele jk
    waache waseme ccm oyee

    ReplyDelete
  2. Nice CCM campaign coverage from blog ya jamii, but I expect other major parties to receive the same coverage to be fair and balanced.

    ReplyDelete
  3. Kwa Style Hii CCM Simchezo

    ReplyDelete
  4. Kwani Kaka Misoup huyo Diamond hana Nguo nyingine? manake kila video Nguo hizo hizo mpaka live shoo nguo hizo hizo!

    ReplyDelete
  5. Bradha,

    Huyo DOKII huyo asije kuwa kama VIKI KAMATA!

    Lakini uongo m baya, me ana-kill huyo Dokii huyo! We acha tu

    ReplyDelete
  6. MICHUZI UNAZIDI KUONYESHA WAZI KUWA NA WEWE NI MTU WA CHA CHA KIDUMU

    ReplyDelete
  7. Hivi Michuzi huu uchaguzi ni wa chama kimoja tu cha CCM? Hebu jamani oneni aibu kidogo na kujaribu kuwa fair. Hata kama ni njaa hii sasa imezidi. Shame on you. Wewe ni mtumishi wa serikali Michuzi sio mtumishi wa CCM. Halafu mlimfukuza kazi Prof Baregu kwa kuwa mwana CHADEMA wakati wewe Michuzi hawakufukuzi Daily News wakati ni wazi wewe ni kada mwanausalama wa Taifa. Shame on you man. Shame on you. Nibanie hii ufurahi zaidi ila ujumbe umefika.

    ReplyDelete
  8. Mnacheza na pesa nini,kuanzia Ankal hadi na hao wasanii,huu ni wakati wa mavuno tu kwao,wanakula fungu la kutosha.subirini hizo coverage za sijui CUF nk kama mtaona kitu.Hapendwi mtu hapa.

    ReplyDelete
  9. Hii ni aibu.Kujipendekeza gani huku kwa watawala. Hivi pamoja na umasikini wa nchi sasa,mfumuko wa bei,kuanguka kwa thamani ya pesa yetu na ufisadi mkubwa wa wizi wa rasilimali zetu, hawa vijana kweli wanapanda jukwaani na kuwaambia wenzao chagueni tena CCM? Kweli njaa inaondoa utu na uwezo wa kufikiri

    ReplyDelete
  10. napenda sana wasanii simple kama alivyo mh temba veeeeeeeeeeeeery simple sio kujiweka manywele kama kichaa na kushusha suruali kwenye makalio, wengine igeni mfano cha muhimu ni kushusha mistari sio kujiwekaweka tuuuuuu!!!!!!!!

    ReplyDelete
  11. why not other political parties???

    ReplyDelete
  12. Alaaaa kumbeee Michuzi ni sisiemu,

    ndio maanaaaa eheee.................!

    ReplyDelete
  13. WEWE BWNA MICHUZI KAMA UMESHINDWA KAZI ACHA MAMBO YA KUTUANDIKIA HABARI ZA CCM TU UNAFIKIRI WOTE NI WAM CCM? AU NDIO MAMBO YETU YALE YA TAKRIMA ACHA HUO MCHEZO HII NCHI NI YA KIDEMOKRASIA NA UTAMBUE SIO WANA CCM WANAOTEMBELEA BLOG HII KUNA WA VYAMA VINGINE NA WASIO NA VYAMA WOTE WANAHITAJI HABARI TEK KEA KAKA

    ReplyDelete
  14. ELIMU YA SOMO LA URAIA TANZANIA BADO, KWANI KASUMBA ZA TANU BADO ZINATAWALA NA WALA SI HOJA YA SERA ZA KWELI ZA UMMA.
    UCHAGUZI UKIKARIBIA HAPO TUNAWAJALI WANANCHI NA KUGAWA MAGWANDA YA BURE ETI TAMASHA LA CCM.
    VIWANJA VYA MIPIRA VILIJENGWA KWA NGUVU YA WANANCHI WOTE VIMETEKWA NA KUWA MALI YA CCM.
    HOJA YA KUONGEZA MISHAHARA ILIKATALIWA LAKINI WAKAONGEZA BAADA YA KUONA KAMPENI ZAANZA KUWAZUGA WAFANYAKAZI
    MIRADI MINGI IMEFANYIKA MIEZI YA KARIBUNI NA UCHAGUZI
    HAPO MCHEZO WA KISIASA NDO UNAFANYIKA.

    VIONGOZI WALIO NA SKANDAL ZA KUTUMNIA OVYO MADARAKA NA WIZI WA FEDHA ZA UMMA NDO WANAPETA KWENYE UTEUZI WA UBUNGE, HAPO NI KUTUPAKA MAFUTA KWA MGONGO WA CHUPA

    ReplyDelete
  15. Shame on you wote mnaomlaumu Michuzi, inaonyesha jinsi upeo wenu wa kuelewa ulivyo mdogo! Astaghafirullah kwa kusema hivyo lakini inabidi isemwe.

    Hivi nyinyi nakuulizeni uwezo wa utambuzi mdogo, kusoma hamjui BASI HATA KUONA KWA MACHO HAMUONI? Huyu Michuzi kaweka mpaka na picha yake kuwa yuko kwenye hiyo mikutano ya campaign ya CCM, na ndizo hizo picha anazozitoa kwenye blogu kwa sababu anazipiga mwenyewe. Sasa kama hao wa vyama vingine hawamtumii picha akaziweka mnataka afanyeje? Yeye azitoe wapi hizo picha wakati huko hayuko?

    Mwisho sidhani kama blogu ni hii hii tu ya Michuzi Tanzania nzima, kuna blogu kibao tena nyingine ni za WAKEREKETWA WA VYAMA VYENU KABISA, cha ajabu kwa nini hawaendi kupiga picha kwenye mikutano yao ya kampeni na kuzitundika kwenye blogu kuthibitisha ukereketwa wao.

    Big Up Michuzi kila mtu ana interest ya kuona kampeni hasa ya CCM maana tulivyokuwa tunasikia humo mitandaoni kuwa mwaka huu hawana lao, lol! mbona imekuwa aibu jinsi watu walivyojitokeza kwenye mikutano yao ya kampeni tena hakuna helikopta wala nini. Waache wakuite sekuriti gadi sijui nini wewe endeleza libeneke!

    ReplyDelete
  16. Kwani siku zote hamjui kama michuzi ni ccm damu,na swahiba wa kaka mkubwa toka wapo pamoja kwenye kupiga mbizi maji na kaboti kao wakati kaka mkubwa hajawa big brother alipo kwenda kuwaangalia jimboni kwake walipopata mafuriko na kuna uwezekano wa kuwa michuzi ni usalama wa taifa.

    ReplyDelete
  17. akiwa usalama asiwe usalama its none of business!Stop being paranoid

    ReplyDelete
  18. Njaa tupu hamna lolote. Flora Mbasha bwana asifiwe sana. Ha ha ha !!

    ReplyDelete
  19. THIS IS LIKE WATCHING A MOVIE THAT'S WHAT OUR COUNTRY HAS BECOME. WHY ALL THIS? WHAT A PARTY, DEAL WITH REAL ISSUES. HE NEEDS TO CHECK HIMSELF IN A GOOD HOSPITAL FIRST.

    ReplyDelete
  20. michuzi watu wanachonga sana juu yako achana naoooo,tupe vituuus.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...