
Na Sekela Mwasubila - Ulanga
Watoto wawili wa familia moja wamefariki dunia na bibi yao kuungua vibaya kutokana na moto ulioteketeza nyumba yao majira ya saa nne usiku katika kijiji cha Isyaga wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.
Akiongea na mwandishi Bi Sabina Nambamoka (35) ambaye ni mtoto wa majeruhi amewataja waliofariki kuwa ni John Makamo (9) na Edwini Kologero (5) na Bi Kilala Mgala (60) ambaye ni mama yake mzazi.
Amesema yeye anaishi kijiji cha jirani na eneo la tukio hivyo alikuja kuitwa usiku kuwa na nyumba ya mama yake inateketea kwa moto na alifika eneo la tukio alikuta moto umetanda na juhudi za kumuokoa zikiendelea, baba yake alikuwa amekwisha okolewa na alijeruhiwa kichwani na mkononi.
Aliongeza kuwa baada ya mama yake kuokolewa moto ulizidi na kupelekea watoto kupoteza maisha yao kwa kuungua vibaya na kumfikisha mama yake hospitali ya Wilaya mnamo saa tisa za usiku.
Akiongea Dkt. Malekano toka hospitali ya Wilaya ambaye ndiye anayemhudumia mgonjwa aliyejuruhiwa kwa moto huo amesema kuwa baada ya kupata matibabu hali ya mgonjwa inaendelea vizuri japokuwa ameungua asilimia sabini na tano ya mwili wake.
Mkuu wa upelelezi wa Wilaya L.N Buya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha moto ni moto uliokuwa umeachwa nje kutokana na upepo ukashika nyasi zilizoezekewa nyumba na kupelekea kuungua kwa nyumba hiyo.
pole mama.Mungu akupe nguvu
ReplyDelete