Wistone Chidumule na Selina Tendayi wakimeremeta wikiendii hii baada ya kuishi pamoja kwa miaka 35 na kupata watoto sita na wajukuu saba kabla ya kuamua kufunga ndoa rasmi Maharusi na wapambe baada ya kumeremeta
Maharusi na mdau wa Ujerumani na wapambe watoto
Wakitoka kanisanin kumeremeta
Kimasomaso mwanangu isimuoneeee....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Brother Michuzi naomba iwekwe wazi, hiki kitendo cha kubariki ndoa ni nini?
    au wanafunga ndoa baada yakuishi bila ndo kwa muda wote bila ya kuwa katika ndoa?


    KILA MTU UTASIKIA NABARIKI NDO, JEH! MTUAMBIE NI LINI MLIFUNGA NDOA MPAKA LEO MNAIBARIKI?

    ReplyDelete
  2. Hongereni Maharusi. Bibi harusi bado anadai, utasema ana miaka 35 hivi.

    Mkipenda watoto wenu muwaasili (muwa-naturalise ????) ili kuwafanya wawe watoto halali wa ndoa na kuwatoa uwanaharamu (kumradhi kwa lugha kali). Maana sheria msumeno. Mathalan, ikatokea mkapata watoto wengine kwa sasa (baada ya kufunga ndoa, that is), watakuwa na hadhi na haki zaidi kuliko hao watoto wenu mliowazaa kabla ya kuoana - you know what I mean? Maana kuna leo na kesho.

    Maisha mema ya ndoa.

    ReplyDelete
  3. Hii nimeipenda, big up kaka chidumule.
    Mdau wa London.

    ReplyDelete
  4. Hongera wadau kwa kutimiza miaka 35. Ni muda mrefu sana mungu azidi kuwapa nguvu.

    Mdogo wenu nimeoa na ndoa yetu ina miaka 10 lakini nimeichoka kweli kweli.

    Natafuta jinsi ya kufyatuka.

    ReplyDelete
  5. thats wonderful, congratulations to both of you

    ReplyDelete
  6. Hongereni saana.ila sasa ndio mwanzo wa kuachana.maana mmezini miaka yote hiyo hamkuwa na tatizo ila sasa mmeharalisha ndio mtapo achana.
    kuzini raha bwana asikwambie mtu.

    ReplyDelete
  7. Kweli Ndoa ni Upendo Kwanza na siyo Makaratasi yaliyotiwa wino au sherehe kubwa.

    Upendo Huvumilia Yote shida, raha, huzuni, gubu n.k.

    Ndiyo maana hawa wapendanao wameamua kukamilisha Upendo wao kwa shamrashamra ya Makaratasi yaliyotiwa wino, baada ya kutibitisha Upendo wao kwa vitendo miaka 35, nasema miaka 35.

    Hongereni sana Wapendwa.

    Mdau
    YoungBoy.

    ReplyDelete
  8. Hoja ya Haja,

    Ndoa inahalalisha watoto waliozaliwa nje ya ndoa (Children born out of the wedlock)? Does it (Retroactive Marriage) make them (children born out of the wedlock)legitimate children of the marriage?

    Najua kuna nchi nyingine watoto waliozaliwa nje ya ndoa wanakuwa legitimate children pindi wazazi wakioana, lakini ndani ya kipindi fulani, say within a year.

    Je, Sheria ya nchi inasemaje? TAFAKARI!

    Kisha changia hoja.

    Hongera kwa Maharusi.

    ReplyDelete
  9. Retrospective sorry, and not Retroactive.

    Does Retrospective marriage make natural children born out of the wedlock legitimate? Ndoa inawafanya watoto wa nje ya ndoa wa wazazi wanaooana halali?

    ReplyDelete
  10. Kula tano broda, hongereni sana kwa kuwaonyesha watu ni jinsi gani maisha ya wawili yanatakiwa,sio matarumbetaa meengiii na manjonjo kibao and at the end of the day ndoa inadumu mwaka 1 tuu.
    HONGERENI SANA BANDUGU...BAELEZEEE NA BAONESHE!!
    Cha chandu - uk

    ReplyDelete
  11. Siku ukimfurumusha mama yao utakiona cha moto. Hapa ni kwamba umedihirishia watoto kuwa wewe na mama yao mna upendo kweli sio unafiki. Na ndo maana ulisubiri wazaliwe na wajukuu wakue ili uwaonyeshee kuwa unampenda bibi yao kimaso maso. Malaika azidi kuwalinda katika ndoa yenu ili shetani asipande nafasi.

    Nyumba ujengwa kwa mawe matofali na miti, Bahari ndoa imara ujengwa kwa Upendo na Amani ya kweli.

    Mdau USA

    ReplyDelete
  12. Bibi arusi punguza vyakula vyenye mafuta na sukari bado ungali kijana. Mwili wako utapendeza sana. Sio lazima ufanye nazoezi ya kukimbia ama kutendea Maji ya moto kila siku yanayeyusha mafuta. Na usinywe soda. Utakuwa safi kabisa. Labda kama huko na ujauzito hapo sawa. Nimependa sana mipango yenu ya Baada Ya,,,

    Mdau USA

    ReplyDelete
  13. Mmmh, yeah!anyway, better late than never!

    ReplyDelete
  14. Kuna watu wameng'ang'ania watoto wa nje ya ndoa sasa wanakuwa ndani ya ndoa, c'mon people does it make any difference? Ni mtoto gani atakayezaliwa baada ya hapo ampigie kelele kaka yake aliyemtangulia (kwa wazazi hao hao) eti kazaliwa nje ya ndoa? Are u serious?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...