Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon

Na Mwandishi Maalum,
New York

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amemteua Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin William Mkapa ,kuongoza jopo la tume ya watu watatu itakayoangalia mchakato wa kura za maoni Sudan Kusini na Jimbo la Abyei.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa leo, uteuzi huo unatokana na maombi yaliyotolewa pande mbili zinazounga mkono makubaliano ya amani ya kudumu nchini Sudan.Pande hizo ni Serikali ya Sudan na Kikundi cha People’s Liberation Movement.

Wengine walioteuliwa ni aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ureno, Bw. Antonio Moteiro na Bw. Bhojraji Pokharel Mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Uchaguzi nchini Nepal.

Akizungumzia uteuzi huo, Ban Ki Moon anasema ana imani kwamba tume aliyoiteua itasaidia kufanyika kwa kura hiyo ya maoni itakayozingatia matakwa ya watu wa Sudan Kusini na Jimbo la Abyei

Jukumu kubwa la tume hiyo pamoja na mambo mengine ni kufanya ziara za mara kwa mara nchini Sudani katika kipindi chote cha mchakato wa kuelekea kura za maoni. Upigaji wa kura za maoni unatarajiwa kufanyia mwezi Januari 2011

Tume hiyo pia inatarajiwa kukutana na kushirikiana na pande zote zinazohusika katika mkataba wa amani, tume inayoratibu kura ya maoni, jumuia za kiraia na makundi ya waangalizi wa kura hiyo.

Pamoja na kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, tume hiyo itafuatilia kwa karibu mchakao mzima wa kura za maoni na pia masuala ya kisiasa na hali ya usalama.

Tume itatakiwa pia kufanya kazi ya kuhakikisha inaimarisha imani ya mchako wa kura za maoni, kuhakikisha na kuzitaka pande husika na viongozi kuchukua hatua za pamoja za kutatua matatizo yoyote au migogoro itakayojitokeza.

Wananchi wa Sudan Kusini watapiga kura yao ya maoni kuamua iwapo wajitenge na Serikali ya Khartoum ,wakati wananchi wa Jimbo la Abyei linalogombaniwa na pande zote mbili ,wao watapiga kura ya kuamua wajiunge na upande upi iwapo Sudan Kusini itajitenga na Kaskazini.

Upigaji wa kura ya maoni ni miongoni wa mabadiliko yaliyofikiwa katika Mkataba wa Amani wa mwaka 2005(CPA), uliomaliza vita vya zaidi ya miongo miwili nchini humo. Aidha kura hiyo ni muhimu sana kwa mstakabali wa nchi yote ya Sudan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mkapa Kichwa bwana! big up and thank you for holding our flag high!

    ReplyDelete
  2. I am a Tanzanian who is proud of your work and intellect, good to see the World appreciating your good work. Mkapa Oyee

    ReplyDelete
  3. masiara haya sasa

    ReplyDelete
  4. Kweli Nabii hathaminiwi nyumbani kwake na Ukisema wa nini wenzako wanasema nitampata lini.

    Mkapa nyie mnamgalagaza hapa kila siku wenzenu wanam admaya!

    ReplyDelete
  5. Naungana na bw.Bankin moon kwa kujua au kuona ufanisi wa bw.mkapa master alikuwa kiongozi wa ukweli for my side na muadmire!mungu amjalie atuwakilishe vyema,tchao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...