Habari za kuaminika zinaripoti kuwa, Taasisi za Elimu zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki katika Kata ya Kilema Kusini wilaya ya Moshi Vijijini, ZITAVUNJA MASOMO KESHO ALHAMISI 30 Septemba, ili zishughulikie zenyewe, kwa nguvu kazi , barabara ya Kilema , ambayo imeharibika vibaya mno na kusababisha usafiri mgumu kuzifikia taasisi hizo.

Kwa mujibu wa habari hizi taasisi za Seminari ya St James, Sekondari ya Olaleni, Kilema Youth Technical Training Center Mandaka na shule mpya ya Askofu ya Sekondari ya St Amedeus watashiriki katika zoezi hili.

Kwa muda mrefu barabara hiyo muhimu inayohudumia pia hospitali ya Kilema, Chuo cha Ualimu Mandaka, shule za Sekondari za Serikali za Mrereni na Kisuluni , imeharibika vibaya mno na kulalamikiwa katika kila ngazi lakini hakuna kilichofanyika.

Inasemekana hata wageni mashuhuri wa Kitaifa waliokuwa watembelee baadhi ya taasisi walibadilishiwa ratiba ya ziara kwa hofu ya wao kuuona ubovu huu wa kutisha.

Sasa basi, taasisi za dini zimeamua kuishughulikia. Haijafahamika kama taasisi za serikali kama Chuo cha Ualimu Mandaka na Sekondari za Mrereni na Kisuluni zitawaunga mkono wenzao, lakini ukweli ni kuwa barabara hii imefikia hali mbaya sana na ya kutisha wakati viongozi wanaiona na wanapewa taarifa za mara kwa mara.

Hata hivyo mwandishi wetu alipojaribu kuwasiliana na Mtendaji Kata kujua kama anazo taarifa hizo lakini hakuweza kupatikana na alipomtafuta Mhandisi Barabara wa Halmashauri ya Moshi Vijijini kwa ufafanuzi pia hakufanikiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. tatizo lenu moshi mnapenda kulalamika sana hata vitu vidogo as if mikoa mingine iko safi barabara zake, nafikiri kama kuna mkoa ambao ulipendelewa kwa ujenzi wa barabara basi kilimanjaro inaongoza na ukiangalia kwa huko juuutakuta bara2 yenye matatizo ndio hio hio moja nyingine zote zipo poa kama ile ya mpaka maarangu mtoni na kupanda juu kidogo iko poa eccept hako kakipande kadogo tu nyie mnaliaaaaaa kam moshi nzima haina barabara ningeomba kwanza mtembelee mikoa mingine especial ya kusin muone ndio mngejua kwamba hio barabara ya kilema ni lami kwao wangeipata kama hio ya kilema wangempa jk kura bila matatizo cos kwao ingekua inatosha, so wachaga kuweni na subira sometimes, zile enzi za kupendelewa zimeisha so mkubali kuwa kwenye kyuu muda ukifika jibaba jk litawajengea si mnalijua liprezda letu lilivyo makini limeisha sikia kilio chenu so u just wait

    ReplyDelete
  2. kwanini walikataa hao watu wasione hizo bararara? je walipewa hela za kutengeneza na mwishowe kuzila au nini vipi? ni muhimu kuona nchi ilivyooza ili wakienda bungeni wakajitahidi kuweka budget ya infrastructures kwa nchi nzima.

    ReplyDelete
  3. tatizo hela ilitolewa, wenye nayo wakala... sio kwamba tunalalamika na sio kwamba tunataka kupendelewa.. ni kazi ya serikali kutengeneza barabara na kodi tunalipa kwa nn tusitengenezewe bara bara!!! hao wengine kama wameshindwa kudai haki zao basi sisi tunataka!!

    ReplyDelete
  4. Anayesema moshi ni walalamishi anakosea. Maendeleo hayaji kwa kujifananisha na maskini. Ukijifananisha na maskini utabweteka na kujiona umeshafika. Maendeleo yanakuja kwa kuweka standard na kupigania kuifikia. Kama bado kilichopo kiko chini ya standard then something needs to be done. Uwezo wa kujieleza na ku demand kilicho bora usiwe confused kama kulalamika. Mdau Australia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...