Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Azam Bw. Said Salim Baharesa, baada ya kumaliza kula futari aliyoiyandaa kwa ajili ya wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam nyumbani kwake Oysterbay jana jioni.
Baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha Nchi mbalimbali hapa Nchini pamoja na wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam, wakisoma Dua ya pamoja baada ya kumalizika Sala ya Magharibi kabla ya kula futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein nyumbani kwake Oysterbay Dar es salaam jana jioni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein katikati akila futari pamoja na wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam aliyoiyandaa kwa ajili ya wananchi wa Mkoa huo nyumbani kwake Oysterbay Dar es salaam jana jioni. Kushoto Mufti Mkuu Sheikh Issa Shaaban Simba, kulia Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Geoseph Warioba.Baadhi ya Mabalozi wa Nchi mbalimbali waliopo hapa Nchini, wakila futari pamoja na wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam, iliyoandaliwa na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein nyumbani kwake Oysterbay Dar es salaam jana jioni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. HIZI FUTARI ZA KILA LEO ZA VIONGOZI WA CCM ZINACHUKUWA NAFASI YA POCHI NINI? MICHUZI NAFASI HII SI ANGALAU UNGETUWEKEA HABARI ZA KAMPENI ZA UPINZANI HATA KAMA UNGEWAJUMUISHA WOTE KWA PAMOJA. YAANI KAMPENI ZA FUTARI WEWE UNAZIONA BORA!

    ReplyDelete
  2. Baharesa na Geoseph ndio kina nani? Mwandishi kuwa makini na majina ya watu hususan 'wakazi wa Dar es Salaam'.

    ReplyDelete
  3. Mimi ninampenda sana huyu mzee Said Bakhresa, yeye yupo kimya sana wala humuoni kurumbana kwenye TV, kama hawa matajiri wetu wa epa, kila siku ni kijikweza na kurumbana tu kwenye TV na magazeti, Jamani igeni mfano wa huyu baba

    ReplyDelete
  4. HI NA MIMI NI MWANANCHI WA DAR HAPA RANGI TATU, NIKITAKA KWENDA KWENYE HIZI FUTARI NIFWATE UTARATIBU GANI AU NDO HADI NITUMIWE BARUA ya mwaliko?

    KCC

    ReplyDelete
  5. Kaka tafadhari rekebisha jina la Joseph S Warioba na sio Geoseph

    ReplyDelete
  6. Tanzania haijawahi kuwa na "Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Geoseph Warioba."

    Tufundisheni kwa umakini zaidi!

    Jina lake kamili: Joseph Sinde Warioba.

    ReplyDelete
  7. NI HIVYO HIVYO TU SI MRADI MMEELEWA, MAJINA YA KIZUNGU MAGUMU NDIYO SABABU WALIMU WANAWAFANYIA MITIHANI YA KIINGEREZA WANAFUNZI.

    ReplyDelete
  8. Ndugu zangu kuna mtoa maoni anasema anampenda Bakhresa kwa sababu hajikwezi kama tajiri ya epa, huyu hawezi kwenda tv kwani anajua watu watamwuliza alivyopata national milling pugu siyo halali kabisa hawa ndiyo waaribifu wakubwa wa uchumi wa nci yetu wala husimpende sana, mkulima wa mahindi ananyonywa wao kwao neeme sana tu.
    Mdau uk

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...