Mwalimu wa Kimataifa wa somo la Ujasiriamali, Eric James Shigongo amesogeza elimu nyumbani kwako na kukupa mafundisho yenye hadhi ya Chuo Kikuu cha Mtaani.

Shigongo atazindua CD inayoitwa Street University (Chuo Kikuu cha Mtaani) hivi karibuni, lengo likiwa kuwawezesha watu mbalimbali kujifunza somo la Ujasiriamali.Akizungumza na gazeti hili wikiendi iliyopita, Shigongo alisema kuwa ameamua kutoa CD hiyo ili kutoa fursa pana kwa wajasiriamali chipukizi kujifunza mbinu mbalimbali za kunufaika kibiashara.
“Ndani ya CD hiyo natoa elimu bora kabisa. Elimu ya kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wakubwa. Elimu ya kuwakomboa Watanzania katika mambo ya kiuchumi,” alisema Shigongo na kuongeza:“Nahitaji kuzalisha mabilionea wengi kadiri inavyowezekana, kwahiyo Watanzania wenye kiu ya kutaka kuwa mabilionea, wanaweza kunufaika kupitia CD yangu.”Shigongo aliendelea: “Watu wajiandae kuipata hivi karibuni. Itapatikana kwenye maduka ya Zizzou Fashions.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Matatizo yote nikosoma Dini Mwenyezimungu ndio Mtatuwa matatizo yote.

    ReplyDelete
  2. Wadau au kutoka kwake yeye, Naomba wasifu wa Eric(academical and carrier wise )

    ReplyDelete
  3. we Anony hapo juu.
    Kazi ya Motivational speaking haihitaji mambo ya academical.
    Hii ni sawa na pastor au sheikh.
    Cha muhimu ni lazima uwe successful kwa watu kuamini maneno yako.wewe endelea na uwakademiko wako.In the funeral celemony people say"The late had a degree but he never made monies in his life"

    ReplyDelete
  4. Mdau unayetakamjua shigongo..mmiliki wa kampuni namba moja ya magazeti ya udaku tanzania,Global Publishers mtunzi wa riwaya na novels, mjasiriamali, mwanasiasa......

    ReplyDelete
  5. to the best of my knowldge hajamaliza hata form four. alikuwa mchoma mishikaki kisha mtoa photcopy na kaaanzisha magazeti
    ni mjamja na anaogopa sana wasomi

    ReplyDelete
  6. Eric Shigongo, mwizi, tapeli aliyefanikiwa kupitia kasoro za system zetu mbovu...Leo anaweza kusimama na kueshimika kwa sababu ya pesa, akijifanya yeye ni mbunifu na mjuaji kuliko wale waliosoma...kufungua chuo sio gazeti la udaku. Ushauri: Unafahamu mafanikio yako ni kupitia ujanja ujanja na wizi, sasa rudi shule ukajifunze zaidi..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...