Mkurungenzi wa kampuni ya Pili Pili Entertainment (katikati) Sameer Srivastava akimpongeza nyota mmojawapo wa filamu mpya iliozinduliwa usiku wa leo iitwayo Black Sunday,ndani ukumbi wa cinema wa Mlimani City,Steven Kanumba kwa kuonyesha umahiri wake mkubwa wa kuigiza ndani ya filamu hiyo iliokuwa na msisimko mkubwa kwa watazamaji. Mbali ya Kanumba pia kulikuwepo na nyota wengine walioinogesha filamu hiyo vyema kama vile Aunt Ezekiel,Monalisa,Yusuph Mlela na wengineo.Uzinduzi wa filamu hiyo uliandaliwa na kampuni ya Pili Pili Entertainment na kuhudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali.
Nyota wa filamu ya Black Sunday iliozinduliwa usiku wa leo,Steven Kanumba akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa waliofika kwenye uzinduzi wa filamu hiyo iliokuwa na waigizaji wenye vipaji kibao, mara baada ya kutoka kuitazama.
Wageni waalikwa wakiingia kwenye ukumbi kuishuhudia filamu hiyo usiku huu.Kwa picha mbalimbali za tukio hili ingia hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Lakini kwenye sifa lazima tutoe... steven kanumba anaigiza vizuri wengine wangeiga mfano kwake manake saa zingine unasikia wazi kabisa kuwa mtu anasoma lakini steven anaweka "uhai" kwenye sinema zetu

    ReplyDelete
  2. hivi jamani steven kanumba kaoa??? au bado ni mwindaji tu?? mimi ni daktari ningependa kukutana nae kama ni yu singo

    ReplyDelete
  3. steven kanumba naomba sana ufanye mchezo na dachi, kalunde na mlacha majina yao siyajui ila ni waliigiza sinema ya fair decision, kwa kweli wamenifurahisha na mwingine mtu mzima mhaya simjui jina anafanya sauti yake inakuwa mbaya sana kama ana chura kooni ila ni mwigizani fresh sana

    ReplyDelete
  4. Dah,kijana hongera sana kwa kazi nzuri. Mi mpenzi sana wa filamu (hollywood,bollywood,nollywood etc na pia kwa saaaaaana, The Bongo Movies. Namkubali sana mzee mzima Kanumba, si kwa kuigiza tu, ila pia kubadilisha sekta ya filamu bongo na kuwa kibiashara zaidi. Enterpreneurship!Nimeipenda hii

    A millionaire in making
    Perth,Australia

    ReplyDelete
  5. nshimimana aka dumisaneSeptember 24, 2010

    kanumba bwana, sasa hapo sijui ndo atakuwa anasemaje!?

    lion children, lol.

    hee hee.. nikikumbuka nacheka kweli!?

    = = =
    Buffalo,
    New York

    ReplyDelete
  6. mdau wa buffalo we kiboko imebidi nicheke tuu, watu hamsahau ha ha haaa, im closing!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...