
NA MAMBO YATAKUWA MSWANO ZAIDI
UKITAKA KUONA POST HII AMBAYO NI YA KWANZA SIKU HIYO YA SIKU
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hongera mno Kaka Michuzi, Mungu na azidi kuwa nawe unatuhabarisha mengi kwa kweli. Asante sana.
ReplyDeleteHongereni sana wakurugenzi wa Globu ya Jamii kwa kutimiza miaka 5 ya maendeleo,tunazidi kuiombea globu ya jamii mafanikio mema na maisha marefu,Pia tunakupongeza Ankal kwa uvumilivu uliokuwa nao mda wote huu,kwa kuyavumilia mawimbi na ngurumo kali za wadau wa globu,tupo pamoja nawe ...kwani ukubwa jalala,utupiwa mema na mabaya ...
ReplyDeleteHongera sana,tuhongere sote..
wadau
FFU wa ughaibuni
Asalaam alaykhum ankal, Pole na swaumu! Hongera sana kwa kazi nzuri nasi tunafata nyayo za juhudi zako katika kupasha habari jamii duniani kote. Insahaalah mola akujaalie maisha marefu na yenye furaha kila mmoja nafurahia na kufaidika san na huduma yako. "Blog ya jamii idumu daima" Amiin!
ReplyDeleteWasalaam
Chef Issa
E bwana ee, siku hazigandi. Hongera sana Bro Michuzi kwa kazi njema kwa jamii. Ni miaka mitano ya mafanikio. Tunataraji miaka ishirini na tano ijayo ya MAPINDUZI makubwa.
ReplyDeleteMaggid
Iringa
Sababu zilizo nje ya uwezo wako? Ankal....tafadhali chukua chako mapema!!!
ReplyDeleteHongera sana kwa kutimiza miaka mitano ya kublogu, nakutakia heri na mafanikio katika miaka mingi ijayo.
ReplyDeletemichuki nakupongeza sana na glob for five year anniversary. Ila uwe makini sana ukuaji wa glob ya jamii naona umetwkwa na siasa na ndiyo hapo "professionalism" inakufa. Mimi naikubali sana hii glob kwa kufanikisha upashaji habari, kuelimisha na kuburudisha..ila imeshindwa kumaintain neutrality na profssionalism hasa kwenye siasa. Ninajua kuwa kuna habari kibao ukipewa badala ya kuzirusha hewani unawauliza wahusika eti"jamani kuna hii mpya nimeletewa niirushe au vupi" tena nyuzi ya kawaida tu ila kwa kuwa inahusu mrengo fulani inakuwa soo. Blog hii inakazi zaidi ya unayofikiria.Hii blog inatumika pia kama "watch dog" kwa wenye madaraka na waliopewa dhamana. kwa hiyo ni zaidi ya unavyofikiria. Ni vyema ukadumisha "professionalism" na haki kwa wote ili blog hii ya jamii iendelee kutoa mchango zaidi katika maendeleo ya nchi badala ya kuonekana ni chombo cha propaganda cha watu fulani...
ReplyDeleteNi maoni yangu najua unaweza yarusha au kuyaweka kapuni as usual..ila Naikubali
Sidhani kama huyu jamaa wakati mnaanzisha blogu hii alikushauri uweke habari za kukandia vyama vyovyote isipokua CCM... na kwamba unapopewa habari nzuri za hivyo vyama vingine usiziweke (kama ile ya majibu ya mchumba wa Dr Slaa kupitia kwa mwanasheria wa Chadema niliokutumia na hukuiweka). Unachuja na kuweka habari za CCM na kuweka kashfa za uongo za vyama vingine. Ukiletewa majibu ya hizo kasfha wewe unakua huziweki. Acha kuwadandia waliomo madarakani kwani siku zao zahesabika. Sijui utajificha wapi wakishindwa.
ReplyDeleteTukiacha hisia za kibinadamu ambazo kila mmoja wetu anazo, pamoja na mitizamo yake, blogu hii pamoja na mmiliki wake wamekuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa vijana wengine. Jina la MICHUZI lina historia kubwa katika tasnia ya habari na itabaki kuwa hivyo. HONGERA SANA MKUU
ReplyDeleteMgombea Mwenza wa CUF Juma Duni Haji alilieleza gazeti hili kwamba Watanzania waelewe kuwa hata wakiipa CCM miaka mingine 100 ya kutawala hawataweza kuwa na maisha bora.
ReplyDelete“Kuna silaha mbili zinazotumiwa na CCM kushinda. Kwanza, masikini na mtu mjinga ndiye anayetawalika. Pili, tajiri hawezi kutawalika. Kwa hiyo wanatambua hizi silaa na wanahakikisha watu wanabaki kuwa masikini na wajinga ili waendelee kutawala.
“Tumefika kwenye shule moja tumekuta ina wanafunzi 900 lakini walimu wanne, kwenye shule nyingine mwalimu mmoja huyo huyo amejiita Mwalimu Mkuu, ukimuuliza kwa nini ajipe cheo hicho anacheka tu,” alisema Duni.
Athari kubwa ambayo inatukabili ni matumizi makubwa ya fedha kwa upande wa CCM, tupo njiani kuelekea Bukoba Vijijini ni dhahiri fedha nyingi zimetumika na hii ni njia mojawapo ya kukandamiza demokrasia,”
Alipoulizwa kwamba matumizi ya fedha hizo inawezekana ikawa kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi inayotaja kiwango hadi Sh bilioni 50, Maharagande alisema kwa vyovyote vile na hasa kwa kuzingatia mazingira ya Tanzania, demokrasia inaathirika.
“Wamesambaza mabango kila kona, fulana zitagawiwa karibu kwa kila Mtanzania…najiuliza inakuwaje mabilioni yamwagwe kiasi hicho wakati huduma za jamii kule wanakoenda kuomba kura zikiwa zimezorota. Dawa hospitalini hakuna hata karatasi za kuandika taarifa za wagonjwa lakini karatasi za kampeni zimesambazwa hadi vyooni,” alisema Maharagande na kuongeza kuwa wana matarajio makubwa kwamba Profesa Ibrahim Lipumba mgombea urais kwa tiketi ya CUF atashinda na kuunda serikali licha ya matumizi hayo makubwa ya fedha kwa upande wa CCM
Hongera Ankala kwa kutimiza miaka 5 ya globu hii ya jamii imekuwa ikitufikishia habari mapema mno. Hatuna budi kuipongeza
ReplyDeleteGLOBU HOYEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!.
Hongera mkubwa! najua umeanzia mbali
ReplyDeleteAhsante kwa kutuhabarisha.
Lakini Ankal usiegemee sana upande mmoja...........
Na wala usiwe unatubania tunapoweka comments zetu zinazopingana na mtazamo wenu.....
Billy
uwege pia unasikiliza ushauri wa wanaglobu basi. hasa mambo ya kukurupuka kuandika habari na kuipublish kabla ya kuhakiki ubora na kubana comment zenye kujenga
ReplyDeleteEBANAEE! KAMA VIPI KWENDA ZAKO, SIKU ZA HIVI KARIBUNI KUFUATIA MASWALA YA KAMPENI UMEKUWA UNANICHEFUA FULANI, KUTOKANA NA BAYAZNES YAKO KATIKA HABARI ZA VYAMA VYA SIASA UMEKUWA UNAKIPENDELEA SANA CHAMA CHA MAPITUNDUZI KWA SABABU YA UKEREKETWA WAKO. SIPONGEZI WALA NINI
ReplyDeleteMuhidin mbona unabania maoni yangu? Nakuuliza, kama Dr. Slaa anatakiwa kufikishwa kizimbani kwa kuiba mke, lini Msekwa atafikishwa pia kwa kumuiba Ana Abdala toka kwa mumewe halali? Tena ni lini Makamba atafikishwa mahakamani kwa kubaka mwanafunzi akiwa mwalimu kule Kasulu? Na ni lini JK atafikishwa kizimbani kwa kuingilia wanawajke wa UWT kila wilaya Tanzania? Umeweka ugali mimi natupa mboga.
ReplyDeleteHongera sana Ankal Michuzi, katika kipindi hicho ambacho kinaonekana kama ni kifupi, lakini ni zaidi ya jumla ya siku 1,825 umekuwa active na blog yako iko current kila wakati! Si mchezo!!!! Ama hakika unastahili pongezi nyingi, na ankal tambua kwamba wewe umekuwa faraja kubwa sana hasa kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi. Mimi nime experience hilo na nakuhakikishia ukiwa far from home at least twice a day utaingia kwenye blog ya michuzi kuangalia "Nini khabari huko home" (I used to. na hapa home, ukiingia maofisini asubuhi, kila mtu yuko kwenye Michuzi blog, yani uko juu kuliko formal doe coms za newsrooms za hapa bongo. Keep it up ANKAL na happy 5th Anniversary!!!RAM
ReplyDeleteHongereni!Ila ushauri wa bure mnakoelekea si kuzuri kuwa washabiki wa kisiasa, mtatupoteza wengi. Hata ukiibania comment yangu ila msg delivered!
ReplyDeleteMichuzi, hii ni blog tu, huku Marekani hata watoto wa darasa la tano sasa wana blog zao, kwa nini ni issue kubwa kwako kuwa na blog sasa? Ningekuelewa kama tupo 1990, lakini sasa ni 2010.
ReplyDeleteHongera kwa vyovyote na wasalimie wanasiasa wako wa CCM.
Maraha ni pesa
USA
Hongera Michuzi.Ndesanjo huko wapi?
ReplyDeleteMdau Toledo.