Uzinduzi wa usafiri wa helikopta juu ya
hoteli ya holiday inn jijini dar leo

Usafiri mpya umeanza jijini Dar leo katika harakati za kukwepa msongamano na foleni. Usafiri huo, ambao ni wa helikopta umezinduliwa kwa mbwembwe leo jijini ambapo vikwangua anga kadhaaa vitatumika kama viwanja kama ilivyo katika nchi zilizoendelea zenye msongamano mkubwa wa usafiri wa ardhini.

Uzinduzi huo umefanyika hoteli ya Holiday Inn saa 5 asubuhi na kushuhudiwa na waandishi wa habari. Kampuni ya kukodi ndege ya Everett Aviation ndio wamiliki wa helikopta hiz ambazo idadi yake haijaelezwa.

“Huu ni mlango mzuri wa kuboresha biashara. Tutakuwa tukiwatoa wateja hapa na kuwapeleka maeneo kama Zanzibar, Mtwara na hata Uwanja wa Ndege kama mtu au kampuni itataka kupatiwa huduma hiyo.

"Wageni watakapokuwa wakiwasili kutakuwa na mawasiliano na mamlaka ya anga hapa nchini, lakini pia hata hapa kwenye hoteli ghorofa ya 11 kutakuwepo na waongoza ndege kutoka kampuni binafsi na wale ambao watakuwa tayari kukabilina na dharura yoyote itakayojitokeza kama ajali au moto, ingawa hilo hatutegemei kutokea,” alisema Meneja Masoko na Mauzo wa hoteli hiyo, Ruan Schreuder.

Schreuder alisema kuwa bado wanafanya mazungumzo na Malaka ya Anga Tanzania ili kupewa kibali cha kutoa huduma hiyo katika paa la hoteli yao na kuwa wanatarajia kuanza kutoa huduma hiyo mwezi Desemba mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. mbona kanafasi kadogo?? kagengo kasije dondoka

    ReplyDelete
  2. hala hala jicho na kidole. vikwangua anga vyenyewe huwa vinaanguka hata bila kuzukumwa sasa vitaweza kuhimili hizo CHADEMA? (Helkopta)

    Hiyo biashara iangaliwe sana, vinginevyo, muda si muda.

    ReplyDelete
  3. i think it is ridiculers! wenzenu wanajenga msingi kabla ya ghorofa. how is it, they are trying to avoid traffic, i personally don't get it au kutakuwepo na private roads zinazo connect hapo angani helicopter inapotua. this is rubbish and it is a complete misuse of resources or (tax payers money). who ever came with this idea sucks even in developed countries it is hardly been used not even in case of emergency....there are so much better things to worry about eg improve our existing infrastructure to suit our needs. we surely don't really need that. it is basically a childish and a showoff kind of business. we are not at that flashy stage in life.

    ReplyDelete
  4. teh teh teh ninavyowajua wabongo kwa kuiga na mwingine naye aagize zake tunaze kuona zinavyopishana huko juu kwa ju...Mweeee tulio chini tuombe Mungu atulinde tu....

    ReplyDelete
  5. Ama kweli duniani kuna mambo... Nchi ya NNe kutoka chini kwa umasikini Duniani kuna helikopta za kukodi!??? Na watu watapanda!.... Kweli baba alisema mwanangu kua uyaone...

    ReplyDelete
  6. itakuwa kama vibajaji vile....kuendeshwa bila leseni wala bima.
    Uwwiiiiiiiiiii...Hilo li nchi linaenda pabaya.
    Nafikiri Serikali ipo kama haipo na wananchi wamelala hawajui wafanyenini zaidi ya kulalamika kuwa hawana pesa na maisha yanazidi kuwa magumu.

    ReplyDelete
  7. Ndio mambo ya jumuiya ya Afrika Mashariki, waKenya hao wametia timu na kampuni yao ambayo pia ina ofisi Uganda.
    Ni jambo zuri likitumiwa vizuri, tusiwe negative sana, kama wewe hauhitaji, wapo wanaohitaji.

    ReplyDelete
  8. sasa hizi helicopter hazitui chini? au za kichina hizi? Maana kama kukwepa foleni na kufika haraka basi naonautachelewa zaidi kwa hili helicopter lao,maana hadi ushuke ghorofa ya 11 si ni sawa na kupanda kibajaji? hizo lifti za hayo majumba si zitakufa siku mbili tu? na vile vile tutaambiwa tulipie lifti umeme. SASA SIJUI KUPAKIA MAGUNIA YA NYANYA INARUHUSIWA AU VIPI?

    ReplyDelete
  9. Swali ni Je tathimini juu ya athari za mazingira na jamii imefanyika?? NEMC mpo hapo?. Ni mimba ngapi zitaharibika au wagonjwa wangapi watakaokufa kwa mshtuko Ocean Road Hosp?.
    I appeal to NEMC to order rapid Environmental and Social Impact Assessment for this type of transport. It may be disastrous to people's heath and safety. Noise pollution and nuisance issue. Richard Mazingira

    ReplyDelete
  10. wewe samuel hapo juu tatizo sio kuhitaji...haina matumizi....cost benefit analysis ndugu yangu we need to work on that la sivyo hatutakaa tufike. huyo mtu ambeye anahitaji lazima kuna ? where on earth is getting this money to spend kama sio matumizi mabovu ya hela ya watanzania maskini wasiokuwa na usemi. the whole idea is nonsense

    ReplyDelete
  11. hiyo ndiyo fati traking' au?
    ama kweli yaliyomo yamo.

    ReplyDelete
  12. Tusiwe na mtindio wa kufikiria, kama demand ipo wacha watu waitumie. Hii ya kusema ni nchi ya nne kwa umaskini hizo ni takwimu tu. And it is a bad mindset!! Kuna watu wana uwezo wa kuitumia hiyo huduma.

    Kulinganisha hapa kwetu na mambo ya dunia ya kwanza sio sahihi. Kama inawezekana kufanya kitu amabcho hata huko hakipo ruksa kufanya, mradi vigezo na masharti kuzingatiwa!!

    Technologia ipo, tunaichukua ile latest, ili mradi uwezo wa kulipa upo, atakayeachwa nyuma kwa kuendelea kuwa na mtazamo wa kimaisha wa karne za giza, huyo hakuna msaada.

    Hata tunapoagiza magari hatusemi tuagize Model T ya Ford eti kwa sababu tu maskini tuanzie walipoanzia. Chukua Mercedes au Hammer kutokana na kina cha mfuko wako.

    Chadema (Helikopita) Oyee!!

    ReplyDelete
  13. Huu ni wizi mtupu! Tunaambiwa dhumuni ni kukwepa foleni, je hata kwenda Zanzibar, Mtwara, na mwishowe mikoa yote, kuna foleni? Serikali na Mamlaka husika ikiruhusu hili, shirika letu la ndege kwisha! Na je huo mpango wa magari ya kwenda kasi utakua na faida gani? Mi naona ni kuwaongezea watu sababu ya kuiba pesa za walipa kodi. Wizi mtupu!

    ReplyDelete
  14. kuna watu wana negativity sana. hiyo ni business idea ya mtu na ameshaju7 anani atakuwa customers wake. kuna daraja la juu labda hao ndo walengwa. hukuwekewa wewe usiye na uwezo kwa hiyo hamna haja ya kuanza kuonyesha negativity

    ReplyDelete
  15. was the design of Holiday Inn took into account a Helipad [uwanja wa Helcopter]
    haya ni mambo ya msingi sana kuangalia, usalama wa anga nk.Otherwise hayo ma-shuttle helcopter yapo sehemu nyingi sana.

    ReplyDelete
  16. Bora iwe AIR AMBULANCE iokoe maisha ya watu wanaopatwa na ajali kila siku

    ReplyDelete
  17. Walalahoi kazi kulalamika tu.

    ReplyDelete
  18. Only in the 3rd world.Badala ya kutafuta suluhisho la muda mrefu wana sugarcoat tatizo.

    ReplyDelete
  19. Acheni ku hate ninyi. Kama wako watu wenye uwezo wa kukodi wache wazikodi. Hela si zao. Wewe kinakuuma nini?

    ReplyDelete
  20. Badala ya kujenga visima watu wapate maji ya uhai na wasiambukizane magonjwa kwa kutumia usafi na badala ya kusaidia dispensari zipate madawa kusaidia wagonjwa na kadhalika helikopta ndiyo ya maana? Hiyo helikopta inatumia mafuta kiasi gani? Hala hala wakazi wa Dar angalieni maana ajali za helikopta hizo. Msituulie ndugu zetu kwa biashara isiyokuwa na kichwa wala miguu.

    ReplyDelete
  21. Asante kwa kuleta ndege tatizo tu ni kwamba tukiomba msaada wa watoto wapo hatarini mtusaidie tu, Kwa sababi hatujui hii helcopter itamsaidia nani siku moja, ninachojuwa tunahitaji vyombo vyote vya usafiri. Kuhsu ujenzi wewe sahau hakuna wajenzi wala wakaguzi wa ujenzi, ukitaka kujuwa tafuta code ya ujenzi Tanzani kwenye mtandao kama utapata hata muelekeo unaelekea wapi. Ukitaka kujenge wewe weka mfuko kando wa kuomba vibali na vinginevyo, hapo unamafanikio mazuri kuliko kuangalia code. Hao jamaa wakishamuona mtu mweupe kila kitu wanapewa, Subiri tu siku moja tutatawaliwa tu na hatuna ujanja wa kutoka nje ya hapo.

    ReplyDelete
  22. hahahahahaha nimecheka sana jamani kama anon mmojawapo alivyosema msiwe na mtindio wa mawazo hiyo ni biashara ya mtu sasa mnaanza ohhh tukiomba msaada ohhh sijui dunia ya tatu, kweli mnakurukupa na mnachekesha yaani shida zenu wengine wasiwekeze biashara zao hiyo ni liugha tu ya biashara hapo ndio kaweka mbwembwe za kuongelea foleni, jamani tuwe na mawazo huru na sio mawazo mgando

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...