Kocha atakayeinoa timu ya Taifa ya Netiboli, Simone Macknis (katikati) akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo jioni kwa ajili ya kuinoa timu hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Bayi na sht ni nahodha wa timu hiyo Jackline Sikozi. Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. kosha wa netball wa nini tena bora mngewaleta kocha wa basketball ! plus mimi nazani tungezingatia kujenga viwanja vya michezo then kuleta kocha wa kigeni ni kupoteza pesa tu ! viwanja vyenyewe viko wapi ? huyo kocha naye njaa tu hatafundishia wapi?

    ReplyDelete
  2. Boss Francis, huyu coacher anawasili toka wapi Kyela, Nzega au wapi ?

    ReplyDelete
  3. Makochawanje-phobia! Mbona zamani timu zetu za netball zilifanya vizuri bila makocha wa nje?

    ReplyDelete
  4. WHY VIONGOZI WETU WA MICHEZO ALWAYS WANA TASWIRA NZURI WACHEZAJI WANAO TOA JASHO CHOKA MBAYA,TASWIRA YA PICHA HII USINGE WEKA MAELEZO UKAULIZA WADAU UNGEPATA MAJIBU TOFAUTI JUU YA NAHODHA.AKINA PENINA MADUHU,AMINA BAKARI,ASHA BARAKA,NK WALIOWIKA ENZI ZA GEREZANI NA BORA,BIMA,TANESCO,JKT MBONA HAWASHIRIKISWI KUNANI.

    ReplyDelete
  5. Hivi jamani nani kaharibu akili za viongozi wetu? E baba Nyerere naomba urudi utuokoe! Kila siku tunasema Watanzania hawana ajira lakini utasikia hata kazi ua Ukocha wa Netball anapewa mtu wa nje. Hivi ni kusema Tanzania hatuna mwalimu mzuri na bora wa Netball? Mimi siamini katika hili na niko tofauti kabisa na mtazamo wa viongozi wetu. Viwandani kuna wazungu na wahindi, kwenye michezo wageni, hivi ndo kusema Watanzania tunanyang'anywa nchi yetu na kazi zetu? Tusije tukasababisha tatizo lilotokea Afrika Kusini hivi karibuni pale walipoandamana kwa madai kuwa wageni wanachukua kazi na ajira za wazawa! Tuwe macho jamani.

    ReplyDelete
  6. Hii dira na mwelekeo wa kuleta makocha wa nje sijui chanzo chake ni nini. Jamani hawa wanakuja third world kuganga njaa hawana mbinu yoyote ya kuinua michezo. Kinachotakiwa ni kuwa-motivate wachezaji wetu na sio kuleta makocha wasiokuwa na kichwa wala miguu. Mbona zamani watu walikuwa wanacheza vizuri? Jamani tuamke he...

    ReplyDelete
  7. Ashukuriwe Rais mpenda michezo kuliko wote Jakaya Mrisho Kikwete.Kipindi kimoja tu cha rais kikwete kuwepo madarakani tumeletewa makocha wawili wa kuinoa Taifa Stars,Kocha wa Pool na sasa tumeletewa kocha wa Netball.Bado kuletewa kocha wa basketball,kocha wa ndondi,kocha wa mdako.Kipindi cha pili cha uongozi wake lazima tutie timu katika mashindano ya nchi za Afrika na kubeba kombe.

    ReplyDelete
  8. Kocha toka nje wa kazi gani jamani?Yaani hao madada waliocheza netiboli huko nyuma wakafanya vizuri miaka hiyo hakuna mmoja wao anayeweza kuifundisha timu yetu?Wenzetu huko nje wanaajiri wachezaji wao wa zamani kufundisha...!Sisi na udunia wetu wa Tatu tunaenda kuleta wageni watulie hela huku viwanja bora,nk vinahitajika!NI AIBU KUBWA SANA!!!!

    ReplyDelete
  9. Huyo kocha amekuja vekesheni bongo. Akimaliza vekesheni yake ananza. Hakuna cha ukocha hapo. Toba!

    ReplyDelete
  10. kwa kweli nchi yetu inatutia aibu kocha wa netball wa nini.Huyu kocha atalala hotelini atakula hotelini na gharama hizo nani analipa na atapewa mshahara.Jamani kwa nini hizi nafasi hatupeani wenyewe hapo nchini kwa uhakika wapo wa TZ wana ujuzi na kuiongoza netball,kweli kuna kamati za bajeti hapa au kuna mtu anataka kula fungu la pesa na kusingizia tumelipa kocha.Haya ni mambo ya aibu kabisa.

    ReplyDelete
  11. poor Tanzania! is this what the country want? ask the salary this lady will be getting, its tones of money and that's all bullshit! millions have no access to water, health services, but we still spend a lot of money which doesn't make any sense. where are the new generation? we need to push this country forward and take off those people who do not think professional..politics kills this country

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...