Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Rais mtata sana huyu hana tofauti na dikteta

    ReplyDelete
  2. jamaa mkwara mpaka marisi wengine wacheki dege lake.

    mtama saana

    ReplyDelete
  3. alimpa tafu sana Amini, lakini Mchonga alimuonesha,kwa kweli si mkubali.Na jacket lake hilo la kutudanganya ndio kabisaaa

    ReplyDelete
  4. Maneno hayo hapo chini alisema gaddafi majuzi alipokuwa italia.

    "We don't know what will happen, what will be the reaction of the white and Christian Europeans faced with this influx of starving and ignorant Africans," Col Gaddafi said.
    chanzo BBC News

    ReplyDelete
  5. chuma hicho ingekuwa viongozi wote wa afrika wana msimamo kama wa huyu basi afrika isingechezewa

    lakini sio tu viongozi ukiangalia huko kwenye nchi zetu za afrika mpaka baadhi ya raia wana ujinga wa kubeba wazungu mpaka leo

    utaona mpaka kwenye hizi comment kuna watu wanafagilia wazungu na kuponda watu wa namna nyengine ukiona hivyo ujuwe bado tupo kwenye utumwa wa wazungu mpaka miaka 500 ijayo

    kubali msikubali gadafi ni chuma cha afrika na ndio asingekuwa na maana basi hao wazungu wenu wasingemuogopa na kumpa heshima mpaka leo

    kaeni kuwa vibaraka wa wazungu mtabakia mkiibiwa mali na kuachiwa mashimo matupu ni wakati wa kuamka umefika wacheni politiki za nyerere mtarudi kula ugali wa njano na sukari ya maji ya miwa na taa za mapira ya gari

    sasahivi mnaweza kula chips mayai basi mnajiona mnajuwa kuchonga na kuanza kufagilia wazungu kuliko waafrika wenzenu ooh gadafi dikteta sasa mnaanza kuwachagulia wenzenu viongozi kama dikteta hiyo ni kazi ya walibya wenyewe kuchagua, nyie kazi yenu chagueni kwenu sio kwa watu.

    ankal usiweke kapuni hii waache iwachome wapate kushtuka wapiga mayoe hao.

    mdau mahakama kuu ya dunia.

    ReplyDelete
  6. We mdau wa Wed Sep 15, 02:04:00 PM, ...chuma cha Afrika? Acha ulimbukeni. Just because mtu anawachamba Wazungu haimfanyi ni kiongozi bora. Basi hata Hitler naye alikuwa chuma, kwa sababu aliwachachafya Wazungu wengi tu.

    Nyie ndio watu mliokuwa mnamsifia Iddi Amin kwa sababu aliwalazaimisha Wazungu wambebe. Huo sio ujanja...mtu yoyote mwenye power au madaraka anaweza akalazimisha wenzake watimize matakwa yake. Nyie mnaojidai kuponda Wazungu mnavyopiga kelele mkinyimwa visa....

    ReplyDelete
  7. Gaddafi ni katili , ulishawahi kukaa libya we anonymous unayemsifia gaddafi? watu wanaongea na facts, basi kama ni hivyo Idd amini, mugabe ni wa maana na wakati ukiwa uingereza ukasema unatokea zimbabwe unadhihakiwa na wazungu. WAZUNGU WANA UJINGA WAO PIA MAJUNGU NA UMBEA WANAYAWEZA SANA, KAA NAO NDIO UTAJUA ILA WAMEPATA CIVILIZATION MIAKA MINGI SANA ILIYOPITA HATA WAARABU WANAFYATA KWA WAZUNGU PAMOJA NA UTAJIRI WAO WA MAFUTA. IN SHORT, GADDAFI ANA MAZURI YAKE LAKINI SI MALAIKA YULE HATA KIKWETE ANA MAZURI YAKE LAKINI SI MALAIKA HANA UWEZO WA KUMFURAHISHA KILA MTU.

    ReplyDelete
  8. tuondokee hapa, visa ni nini? weka bank statement iliyoshiba kama unaona issue. wazungu wako kama watu wengine wana ubaya wao vile vile, rangi na hali ya kiuchumi ndio tunatofautiana, mengine sawa , wananuka hawaogi, kucheka mtu akichemka , kusemana haya yote wanayo pamoja na unafiki, mwangalie gordon brown kwenye kampeni zake alivyomsema vibaya bibi mmoja, google bigot woman, UK utaona video yake. MICHUZI IWEKE HII

    ReplyDelete
  9. Wewe Wed Sep 15, 07:15:00 PM, visa ni ruhusa ya kuingia nchi za ugenini. Bank statement ndio ya nini, ya kuombea visa? Maana kwa mtu unayechukia Wazungu, naona ilibidi utujulishe uko Mahakama ya Dunia. Hiyo ni ya the Hague, au ya Arusha. Najua kama ni ya Arusha usingeona umuhimu wa kutujulisha wote.

    Mimi siwafagilii Wazungu, kwa sababu hata nao wana mambo uliyoyasema; ni binadamu kama mimi na wewe. Lakini mimi siwezi kumfagilia mtu kwa sababu anachemsha Wazungu. Inaonyesha inferiority complex na lack of maturity. Hayo mambo aliyofanya Gordon Brown Tanzania hayapo, au kwa Ghadafi? Sasa huyo Gordon Brown yuko wapi sasa, wakati Ghadafi anazeekea hapo tu.

    Kama wewe unaona kuwabwatukia Wazungu big deal, njoo huku. Utabwata hapo usiku utalala, hamna mtu anayekusumbua. Jaribu huko Libya, uone kama hutakuwa mke wa mtu jela

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...