Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Jan Poulsen

MASTAA wa Simba na Yanga wameachwa kwenye kikosi cha Mdenmark Jan Poulsen ambacho kitamenyana na Morocco Oktoba 9 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika 2012 zitakazoandaliwa na Guinea ya Ikweta na Gabon.

Nyota waliofungashiwa virago na Poulsen kutokana na kiwango duni ni viungo Athumani Iddi'Chuji' kutoka Yanga, Mabeki Salum Kanoni, Juma Jabu, Kelvin Yondani, mshambuliaji Uhuru Seleman, mlinda mlango wa Azam Jackson Chove na Abdi Kassim 'Babi' ambaye ameachwa kutokana na kuwa majeruhi.

Mbali na kuwatema mastaa hao pia amewaongeza wachezaji wapya ambao ni mlinda mlango wa Majimaji Said Mohamed beki wa Simba Haruna Shamte na kiungo Mohamed Banka,Salmin Kiss wa polisi Tanzania na Salum Machaku wa Mtibwa

Poulsem alisema kuwa ni dhairi mchezo dhidi ya Morocco Morocco utakuwa mgumu hivyo anahitaji maandalizi ya kutosha.

"Nimeteua wachezaji hawa kwanza kwa kuangalia mchezaji kuwa fiti kwa asimilia mia moja na hii ndiyo sababu iliyosababisha wengine nimewaacha kwakua ni majeruhi."Mchezo dhidi ya Morocco utakuwa mgumu pengine kuliko ule wa Algeria ni jana tu wachezaji wao wawili wamefunga magoli katika ligi ya mabingwa Ulaya hivyo hatuna budi kujiandaa kikamilifu,"alisisitiza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Maximo alipokuwa akiwaacha hawa wannabes, mlisema ana ugomvi binafsi, sasa huyu m-Denmark mtasemaje?

    ReplyDelete
  2. Hadj Drogba "mwana chelsea"September 29, 2010

    huyu kocha nampenda sana,atafanikiwa INSHALLAH maana wachezaji wa simba na yanga walizidi viburi

    ReplyDelete
  3. Safi sana maana hao Simba na Yanga
    ndio wanaodidimiza soka letu, wachezaji hawajitumi...sasa kama wanataka kuuzika huko Simba na Yanga..wajitahidi mashindano ya vilabu barani Afrika..
    Kuitwa STARS si kwa kigezo cha Usimba na Yanga..no uwezo wa kusakata kabumbu tu..
    Namna hii tutaendelea sana. Safi meneja Taifa stars..
    Mdau
    Kilimanjaro

    ReplyDelete
  4. Safi babu, bado mmoja anayewacheka wenzake wakifungwa eti kwa sababu ya kutopangwa, siku zake naye ni chache ile mbaya. Safi Maximo, safi Poulsen

    ReplyDelete
  5. tofauti ya huyu kocha anaweka wazi kila kitu na sababu zake za msingi sana!! maximo alijaa uswahili sana kuliko U Brazil !! kwa style ya huyu kocha labla TFF wamwangushe wenyewe !Pia ma kicha wazee mi nazani wanafaa sana kwa watanzania kwani kijana rahisi kudanganywa na vijana wenzake , maximo alikuwa anadanganywa kwa kupelekwa twanga pepeta na warembo !!

    ReplyDelete
  6. kwa match ya kwanza tu chini ya huyu kocha taifa staz hilionyesha mpira tofauti sana na wa maximo, naamini this time taifa starz kweli watafanya poa! hila msiwasaau wachezaji vitu kama lishe bora , poshu si adi akiitwa stars

    ReplyDelete
  7. wamewachwa wa Yanga na Simba wamebadilishwa Wengi Simba palepale sema huyu manager anaona tofauti ya wachezaji bora kawahi mapema. Wachezaji watapata kuelewana huu muda uliobaki. MZ

    ReplyDelete
  8. Namfurahia sana huyu kocha maana kwake soka si jina bali ni kipaji na ujuzi uliokuwa nao if you are the best to him automatically you will stand out of the crowd.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...