Helo Michuzi!
Habari za siku kidogo.
Ningependa kujua kama mdau anaingia kwenye soko/biashara ya mavazi kwenye aina ipi maana kuna wigo mpana kidogo kwenye textile industry toka nyuzi,ufumaji,vitambaa/majora n.k.Hivyo ni vema akafafanua kidogo ili tuweze kumsaidia na kisha tuangalie ukubwa wa soko na ushindani.
Pia kuna mambo kama ya kuwekeza kwenye EPZ n.k hayo yote tutamfahamisha.
Kwenye biashara ya vyakula vile vile kuna mambo mengi ya kuangalia maana hiyo ni sekta nyeti yenye vyombo vingi vya uangalizi kuanzia serikali kuu,TBS,n.k na kuna sheria chungu mzima kwenye bidhaa za vyakula ikiwemo Traceability,SPS n.k,lengo likiwa ni kulinda afya za walaji na usalama wa chakula (food security).Vyakula vikavu na vibichi,vilivyosindikwa na visivyosindikwa n.k.
Kwa hiyo ni vizuri kujua ni eneo gani huyu muwekezaji wa ndani anataka kuwekeza.Uzoefu katika biashara moja wapo na hata utaalamu kidogo pia ni muhimu sana hivyo naomba nipate majibu toka kwake ili tuweze kuendelea.
N.B.Biashara nyingi hushindwa kusimama kutokana na kutofanya utafiti wa ukubwa wa soko,mahitaji na washindani katika soko husika.
Pia kodi pamoja na sheria mbalimbali kwenye biashara husika.Mfano Uganda kuna sheria inayozuia uingizaji wa nguo aina fulani ambazo hazikidhi viwango ama ni za viwango vya chini (hapa kwetu baadhi huziita za "Kariakoo ama za Kichina),hivyo ni bora tukaelewa mdau ana fikiria eneo ama bidhaa zipi hasa za kushughulika nazo.
Aksante,
Samson L Buyamba

food security?
ReplyDelete