Mratibu wa kampuni ya Frontline,inayoratibu mchezo huu wa bahati nasibu wa SUPA PESA,Nancy Sumari akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mapema leo asubuhi kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Sea Cliff,Jijini Dar,na Mkurugenzi wa mchezo huo,Bw.Harm Forie na kushoto ni Muwakilishi wa kampuni ya Frontline,Irene Kiwia ambao ni waratibu wa mchezo huo.

====== ====== ===== =====

BAHATI NASIBU YA KUSISIMUA SUPA PESA YAZINDULIWA RASMI NCHINI!

Bahati nasibu ya kipekee inayojulikana kama SUPA PESA itakayowawezesha watumiaji wa simu kujishindia mamilioni ya pesa kila siku imezinduliwa rasmi nchini jana.

Akiongea kwenye uzinduzi wa bahati nasibu hiyo mkurugenzi wa Supa pesa Bwana Harm Fourie alisema “SUPA PESA ni bahati nasibu inayohusisha ujumbe mfupi wa simu ambayo ni kama mchezo utakaowawezesha wahusika kubahatisha kushinda zawadi za pesa, vocha na nyinginezo nyingi kirahisi tu kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu. Kutakuwa na droo na zawadi za kila siku na ya kila wiki itakayowawezesha wateja kushindania zaidi ya tshs milioni 25 kila wiki.

Supa Pesa inahusisha watumiaji wa simu wa mitandao yote ambayo ni Zain, Tigo, Vodacom na Zantel kwa gharama ya Tshs 500 tu. Baada ya kutuma ujumbe mfupi, mhusika atatumiwa ujumbe wa kumuidhinisha kushiriki kwenye droo. Baada ya hapo mitambo ya kisasa kabisa inachagua washindi bila mpangilio maalumu.

Mr Fourie aliongeza kusema “Supa Pesa itajikita kuisaidia jamiii haswa kwenye maswala ya elimu. Tunaelewa kwamba serikali ina changamoto kubwa sana kwenye hili swala na tunaamini kuwa elimu ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya jamii. Tunapenda kujihusisha moja kwa moja kwenye kutoa mchango utakaoleta mabadiliko katika maisha ya watanzania.

Msemaji mkuu wa Supa Pesa Nancy Sumari alinukuliwa akisema “kutakuwa na droo za kila siku kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa ambapo washindi watatu watajinyakulia Tshs milioni 1 kila siku. Washindi hao watajulishwa ushindi wao kupitia ujumbe mfupi wa simu na watatumiwa hela zao ndani ya masaa 24 kupitia huduma ya malipo ya Mpesa kutoka Vodacom. Pia kutakuwa na droo ya kila Ijumaa itakayohusisha wale wote waliotuma zaidi ya SMS nne (4) katika wiki hiyo,mshindi atajinyakulia Tshs. Milioni Kumi. Mshindi huyu wa wiki atapigiwa simu kupitia redio ya Clouds FM kujulishwa kuhusu ushindi wake. Dhumuni kubwa ni kuhakikisha tunawafurahisha wateja wetu kwa kutajirisha maisha ya watu wengi kwa kutoa washindi wengi kila wiki. Bahati nasibu hii ni rahisi sana kushiriki hivyo tunawahimiza watanzania wengi washiriki na kushinda na SUPA PESA!“

Supa pesa imepanga kwenda na wakati na kujumuisha mambo mbalimbali ya kufurahisha kwenye kuendesha mchezo huu ili kuhakikisha kuwa inawaridhisha wateja wake kwa kutajirisha na kubadilisha maisha yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Irene n Nancy ni wanawake live,.mnapambana dada zangu,hongereni sana.

    ReplyDelete
  2. muuza machungwaSeptember 20, 2010

    OOH! IT'S A PURE SCAM.NO ONE WILL EVER WIN A BIG MONEY.IT'S POPULAR IN EUROPE.MASWALI MARAHISI NDIO YATAKAYOKUWA YAKITOLEWA,KWAHIYO KILA MTU ATATUMA UJUMBE KWA MATUMAINI YA KUSHINDA.KWAHIYO MAMILIONI YA WATU WATUMA UJUMBE NA KUPOTEZA 400/=.HII KAMPUNI TARGET YAKE NI HIZO 400 ZETU.HII NI IDEA YA KUZIDI KUMFANYA MTANZANIA AZIDI KUWA MASIKINI SANA.

    ReplyDelete
  3. sijaelewa, hii baati nasibu itakuwa inafanyika live runingani au clouds fm..?? sasa kwasisi ambayo siyo wapenzi wa hiyo clouds fm ni wa RTD itakuwaje au ni mchezo wa vijana (bongo flava)?

    ReplyDelete
  4. Wajanja tutawaona yetu sisi ni macho kushiriki ni kusikia tuu kupitia mtadaoni

    ReplyDelete
  5. hamna ujanja wowote hii bahati nasibu ni ya ukweli kabisa mimi nimecheza na nimeshinda bila hata kutegemea jaribuni bahati zenu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...