TAARIFA YA MKUTANO WA MHE. MIZENGO PETER PINDA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UTAKAOFANYIKA TAREHE 26 SEPTEMBA 2010 SAA 9 MCHANA

Tafadhali rejeeni somo la hapo juu.

Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York, unapenda kuwaarifu ndugu Watanzania wote wanaoishi katika maeneo yaliyotajwa na pia ya jirani kuwa Mhe. Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda yupo mjini New York kwa shughuli za kikazi ambapo pamoja na mambo mengine atahudhuria mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa (UNGA) akimwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Wakati wa ziara hiyo angependa kukutana nanyi Watanzania siku ya Jumapili tarehe 26 Septemba, 2010. Mkutano huo utafanyika kuanzia saa 9 mchana hadi saa 11 jioni. Mnaombwa kuhudhuria.

MAHALI AMBAPO MKUTANO UTAFANYIKA NI:
Nyumba ya Balozi,
30 Overhill Road
MT. VERNON,
NY 10552

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ubalozi wenu unajua dhahiri Watanzania wachache sana wanaoishi upande huo... Hio sio UK kwamba London and mji wa kusoma is 30 mins apart.

    Pinda tunaomba aje down South kwenye miji ya Houston, Dallas, Oklahoma city and ATL. Hapa atakutana na Watanzania tulio na maswali mengi.

    Mwisho. Warning Tanzanians living in US are total different with Tanzanians of anywhere else. So, espect questions about EPA, Richmond and many more.

    GoodLuck....

    ReplyDelete
  2. Inatakiwa tupeleke nyama choma na makande au yatakuwepo? Mi ntawakilisha! Ahsante kwa taarifa.Tanzania itajengwa na wenye moyo.

    ReplyDelete
  3. "...wote wanaoishi katika maeneo yaliyotajwa . . . ."

    Siyaoni hayo maeneo-tajwa!

    ReplyDelete
  4. Wee hapo juu nani kakwambia huku hatupo wengi? hebu peleka huko zako. kama unauchungu na nchi yako njoo kwenye mkutano. Tutasafiri toka Virgina kuhudhuria huo mkutano...

    Na mnaotaka kujua maeneo yaliyokaribu na huyo mheshimiwa kama hujui ni eneo gani lipo karibu na mt vernon, NY basi huishi huku uwaachie wenyewe wanaoishi huko...East coast wote tutatinga ndani ya nyumba. Tunamaswali mengi sana tu natumaini atakua amejiandaa sio kama boss wake akija huku ni unajua bwana, unajua bwana...

    ReplyDelete
  5. HAPA SIO LONDON SHUGHULI HATUZIWEZI TUPO BUISY . AHSANTE KWA KUTUKARIBISHA ILA TUNATAFUTA MAISHA SASA

    ReplyDelete
  6. Kuna state kama 11 East Coast. Ukianzia South East Coast kuelekea Northeast Coast. Virginia, DC, MD,PA, NJ, DE, NY, CT, MA,NH, VT, ME, na RI. State zingine ziko umbali wa 1 hour to 2 hours by car na zingine 5 hours to 7 hours by car kutegemea na kitongoji unachotokea.Usafiri upo wa kila aina hadi boats zimo!! Hivyo mnaotokea mbali zaidi mnaweza kufly hadi hizo state za karibu na kujiunga na wenzenu katika msafara wa hiyo warsha kongamano mdahalo wa masaa 2.

    Is it worth it to come to the meeting or gathering and have a constructive dialogue with senior leaders, politicians, and diplomats??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...