Hi bro Michuzi,
Ningependa kujua kiutalamu ukomo wa uzazi kwa akina baba na akina mama
kwa maana ya umri. Baadhi ya watu wanadai kuwa akina baba waweza kupata watoto ktk umri mkubwa, na akina mama hawawezi kupata ktk umri mkubwa.
Wadau mwasemaje kuhusiana na hilo?
Wisdom itumike kujibu pls.
Mdau muungwana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. wanawake umri mzuri inasemekana isizidi 35 years, yaani ili uweze kupata yale mayai yenyewe yale haswa, japo baada ya hapo wapowengi tu waliojifungua, ila inasemekana wengi wao hupata matatizo ya uzazi, na wengineo hupata watoto wenye matatizo, japo pia kuna wengi tu waliojifungua after 35 attaining years of age na watoto wako wazima tu, mi nikiwa ni mmoja wapo, nilijifungua mtoto nikiwa 40 na ni mzima, na alikuwa ni mtoto wangu wa kwanza.

    Akina baba, sina uzoefu na hilo, ila nadhani inategemea na nguvu na nguvu za mtu, kuna vizee hadi vya miaka 80 na vina watoto wadogo na vinaendelea kutotoa.

    ReplyDelete
  2. kitaalamu inaitwa Menopause,ni kipindi ambacho mayai ya uzazi(oocyte) yanaachwa kuzalishwa toka katika nyumba ya uzazi(ovary) na matokeo yake hedhi(menstruation) inasimama na na uwezo wa kuzaa(fertilization) unakuwa umeisha.
    kipindi hiki huwapata wakina mama tu,kuanzia miaka 40 mpaka 50,wakina baba hawana hii phenomena,wana uwezo wa kuzalisha mpaka siku ya kuingia kaburini,kwa sababu utengezaji wa mbegu za kiume(spermatization) is going through out their life

    thanks mdau istanbul

    ReplyDelete
  3. kwa ufahamu wangu...wakina mama baada ya miaka 35 kwa ujumla kuzaa kunakuwa kugumu, na maranyingi haishauriwi kiafya. However, kila mtu yuko tofauti...wapo ambao afya zao at 35 ni sawa na binti wa miaka 21...so inategemea ha hali ya kiafya, ila kina mama mkishavuka 30 ni bora kutizama ushauri wa daktari, na kufanyiwa vipimo kabla kuamua kubeba mimba. Hii ni wa manufaa ya mama na mtoto.

    Kwa upande wa kina baba nao inashauriwa baada ya 45 wasizalishe, unless kama afya zao zimethibitishwa na daktari kuwa mtoto hatakuwa katika high risk. Again, si maajabu kusikia baba wa miaka 50 hata 60 kuweza kutia mimba inategemea na individual.

    Kwa kulinganisha, over 35 chance za kinamama kubeba mimba bila matatizo hupungua kwa kiwango kikubwa kuliko kinababa kuweza kutia mimba. Off course...akinababa hawabebi mimba miezi 9, kama nao wangekuwa wanabeba mimba probably at 35 wangekuwa at same risk.

    Teknolojia inaendelea sana siku hizi, hata kama umepita 35 na ungependa kuwa mama...kuna njia nyingi zinazokupa nafasi kuwa mama katika umri mkubwa; invitro fetilaizeshen, au hata kutumia tumbo la mama mwingine kubebea watoto waliotokana na yai lako na mbegu za mume wako inawezekana.

    Nimetumia 2nd person singular kwa kurahisisha mawasiliano tu...sijamaanisha WeWe binafsi.

    ReplyDelete
  4. Shule ni muhimu mdau. Kama umepita sekondari katika somo la biology utajua kuwa akina dada wakifika muda wa menopause, yaani , mayai hayatoki tena, basi hawawezi kupata watoto tena. Umri unategemea na afya lakini mara nyingi katika miaka ya 50-70. Wanaume mpaka miaka 90 anaweza kuzalisha lakini kama ana magonjwa kama kisukari au moyo, basi hawezi kuzalisha akiwa na umri mkubwa kutokana na matatizo ya ED (erectile dysfunction) yaani hawezi kusimamisha uume wake. Viagra inasaidia hapa.

    Jaribu ku google katika kiswahili utapata majibu yote, sioni sababu ya kuuliza maswala kama haya hapa wakati una mtandao.

    ReplyDelete
  5. semeni 40 au 50 nakuendelea ,wadau mnaposema kati ya 50 hadi 70 mnamaanisha nini,au mnataka kusema baada ya 70 atazaa

    ReplyDelete
  6. Uzazi unategemea na afya ya mtu, jirani yangu amejifunguwa mtoto mwenye afya njema miaka 48, ila tu alichoona tofauti ni kwamba ajisikia uchovu zaidi wakati wa ujauzito. Mtoto ni mzuri na hana tatizo lolote. Tunshauriwa kuwa na watoto kabla ya miaka 35 kwa akina mama. Wakina baba nia mpaka miaka 70 wanwatoto inategemea na afya yako. Tatizo linakuja kwa je unauwezo wa kumtunza huyo mtoto, kama huna nguvu za bega kwa bega za kuwa na mtoto inakuwa ni tatizo. Kingine ambacho nimegunduwa ni kwamba watoto wengi huwa hawapendi kuwa na baba ambao ni wazee sana kwani rafiki wanwauliza huyo ni bibi au babu yako, ukisema ni baba wanashangaa hata kukupa utani.

    ReplyDelete
  7. Go back to school

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...