Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni na Afisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air Alfonce Kioko kulia akimkabidhi zawadi ya mfano wa ndege ya mpya ya Kampuni hiyo aina ya ATR 72-500 mgeni rasmi Bw. Reginald Mengi mara baada ya kuizindua rasmi jana kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere, ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abilia 66.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi katikati, Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni na Afisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air Alfonce Kioko wa pili kutoka kulia wote kwa pamoja wakinyanyua glasi za mvinyo juu kuashiria uzinduzi rasmi wa ndege mpya ya shiriki hilo aina ya ATR 72-500 yenye uwezo wa kubeba abiria 66 jana kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere, kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Kenya Airways Lucy Malu na wengine kuanzia kushoto ni Claude Paulet Mwakilishi wa Ubalozi wa Ufaransa na Raberta Cocconi Mwakilishi wa Ubalozi wa Italia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Inasikitisha sana... kama mashirika binafsi yanafanikiwa kiasi cha kuwa wanaongeza ndege kila kukicha, tatizo ni nini kwa ATC? Sitaki kusema UCHAKACHUAJI........

    ReplyDelete
  2. KIOKO, na huku nyanda za juu kusini mwa Tanzania kuna mkoa (jiji) unaitwa MBEYA, tunatumia zaidi ya masaa 12 (kumi na mbili) kwenda Dar kwa barabara, tuokoeni na sisi jamani tunaumia!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...