Muendelezaji wa vipaji hapa nchini,Sammy Cool akionyesha umahiri wake wa kulisakata Salsa na mwanadada ambaye anashirikiana nae katika zoezi zima la ukuzaji wa vipaji kwa watoto na watu wazima pia.hii ilikuwa ni katika hafla fupi ya kuwatunuku vyeti baadi ya watoto waliofuzu awamu ya kwanza ya mafunzo ya kucheza,iliyofanyika katika ukumbi wa kituo cha utamaduni wa kirusi kilichopo upanga,jijini dar.
baadhi ya watoto wanaofunzwa na Sammy Cool wakionyesha umahiri wao wa kucheza baada ya kupata mafunzo ya takrubani miezi 6 kutoka kwa Sammy Cool.
Sammy Cool akiwa na watoto hao waliofuzu awamu ya kwanza ya kucheza ambao mkali huyo yupo nao kwa takriani miezi 6.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Halafu tukiachwa nyuma tutalalamika? Hebu angalia hiyo picha mwalimu mbantu lakini hamna hata mtoto moja wa kibantu. Kwanini? Sababu ya wazazi wengi hawatilii mkazo mambo ya sanaa kabisa. Hawajui kama usipofanikiwa kuwa DR, lawyer au engineer unaweza kumake a life out of arts...

    Mimi nilivyokua nasooma huku wala sikufuta vibibi kabisa ili niweze kulipa bills zangu. Nilifundisha piano watoto nikawa nalipwa vizuri sana tu. Piano yenyewe nilijifunzia kanisani na kuread piano note nimejifundisha mwenyewe na wala sio pro bado lakini niliweza kupull up na kufundisha watoto wadogo wanaoanza basic piano lesson..

    Itabidi wazazi wa new generation muamke na kuyapa kipaumbele haya mambo pia la sivyo tutapitwa kila siku na kuishia kuimport hata walimu wa dance. Kama mtu unaweza kwenda bar kila ukitoka kazini jioni sidhani kama utashindwa kumlipia mwanao course ya week 6 tu....Wala mtu asiniambie hela hamna, hela ipo sana bongo ila jinsi ya kuitumia ndio watu hawajui.

    ReplyDelete
  2. mzeee zumbweee.......marangu sec iyo 84,keep it up babu
    gugu

    ReplyDelete
  3. Ulikua umeanza kutoa point mpaka ulipoanza kusema kuwa huku hukufuta, nafikiri ulikuwa unamaanisha hukufuata vibibi kulipa bills. Kila mtu ana uelekeo wake maishani, kama wewe ulikuwa umefundishwa piano, basi poa; sio kila mtu alikuwa na fursa hio. Wengi wanafuata vibibi viwape makaratasi; that is their business!

    Sio kila mtu anakwenda kanisani. Mie mzee wangu alifundishwa music enzi za ukoloni akawa anapiga kinanda kanisani, lakini sikusikia akimponda mtu yoyote. Humility goes a long way! Unaweza ku-make a point without being obnoxious!

    ReplyDelete
  4. Hongera Sammy Cool kwa kuendeleza libeneke- but nakushauri uwe unachukua chako mapema toka kwa wazazi wa wanafunzi wako. Yasije yakakutokea yale yale ya TBC1..... nI MIMI Rafiki yako wa zamani; YCIC

    ReplyDelete
  5. Hongera sana Sammy Cool. Nimefarijika sana kuona unajituma. Big up you will get the reward

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...