Kwa niaba ya Familia ya Njaidi, mimi kaka wa marehemu Yusuf Njadi na mke wa marehemu Sarah Mirambo kwa moyo mkunjufu, tunapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru ndugu, jamaa, marafiki waliopo Tanzania, Jumuiya za Watanzania Cardiff, Cork, Leicester, Birmigham,Reading na London kwa kufanikisha shughuli zote za msiba wa Marehemu ndugu na rafiki yetu, Mnomba Njaidi.
Mnomba alifariki huko Cork City Ireland katika hospitali ya Cork University HospitaI tarehe 27/08/2010 na hatimaye kuzikwa tarehe 12/09/2010 kwenye makaburi ya Kisutu mjini Dar es salaam.
Asanteni kwa dua, maombi na kujitokeza kwenu katika kutufariji na kututia nguvu. Shukrani za pekee ziwaendee kamati nzima iliyoratibu na kufanikisha shughuli nzima ya kuusafirisha mwili wa Marehemu Mnomba kufika Tanzania.
Shukrani pia ziuendee Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Papa King na wanablogu wote waliolitoa tangazo la kifo kwenye Blogu zao.
Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mtu kipekee,tunaomba shukrani hizi mzipokee wote mliohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha shughuli nzima ya msiba huu wa ndugu yetu Mnomba. Hatuna cha kuwalipa bali tunamwomba Mwenyezi Mungu awajalie na kuwazidishia katika shughuli zenu za kila siku.
Asanteni sana

Pole sana kaka Yusufu nasi pia tunasikitika saaana ila usijali sana tuko pamoja.
ReplyDeleteR.I.P OUR BROTHER, POLE KWA FAMILIA NA MARAFIKI
ReplyDeletePoleni sana familia ya Njaidi popote mlipo...Oj kaka wa marehemu anatoka gerezani terehe 24/09/2010ni kweli? TEXAS
ReplyDeletepole sana kaka Yusuph, Mungu azidi kukupa nguvu
ReplyDeletepole kaka yusuph mi maka hapa nipe namba yako pse mpe pole pia adam
ReplyDelete