Align CenterMwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Kinondoni na Mwanaharakati wa kutetea haki za watoto nchini, Nimka Lameck (11)(mwenye kofia) akiwa na Ujumbe wake walipoenda kukiangalia jengo la ukumbi wa Luxery Pub,lililopo wilayani Temeke,jijini Dar.jengo hili ndilo lililotumika kwa disco toto na kusababiwa watoto watatu kupoteza maisha.
Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Kinondoni na Mwanaharakati wa kutetea haki za watoto nchini,Nimka Lameck (11) akitoa pole kwa wafiwa wa watoto waliopoteza maisha katika ukumbi wa disco huko Temeke.


Na Mwandishi Wetu.

Ujumbe maalum wa watoto nchini leo mapema umedhuru kwa ndugu na jamaa waliopatwa na msiba kufuatia hitilafu ya umeme kwenye ukumbi wa Luxery Pub Temeke na kusababisha vifo vya watoto watatu.

Ujumbe huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Kinondoni na Mwanaharakati wa kutetea haki za watoto nchini, Nimka Lameck (11), Salome Filbert (7),Monica Ntevi.Josephu Nzozi, na Maleo Lameck.

Waliweza kutembea familia ya Mtoto Fatuma Ramadhani (7) ambaye alifariki dunia papo hapo ukumbini humo ambapo mama yake Zaitun Chenja ambapo alionekana kuwa na huzuni huku akisema anamwachia Mungu.

Waliweza kutembelea kati ya familia mbili na kutoa rambirambi kwa wafiwa pamoja na kutoa ujumbe kwa wa wazazi hao kutokata tama, kwani yaliyotokea ni mapenzi ya Mungu.

“Sisi watoto tiliopo hapa na tukiwawakilisha na watoto wenzetu,tunatoa pole sana kwani tumeguswa sana na tatizo hili kwa ujumla na tunaomba sheria kali zichukuliwe dhidi ya wahusika” walisema watoto hao.

Aidha, ujumbe huo pia ulitembelea kutoa rambirambi zao kwa familia ya Lilian Rajabu (9) ambaye naye alizikwa juzi na walitoa pole kwa ndugu na jamaa sambamba na kutoa ubuni wao.

Hata hivyo pia ujumbe huo uliweza kutembelea ukumbi wa Luxery Pub na kujionea jinsi palivyo, ambapo walitoa sera yao na kukemea vikali kwa tukio hilo. Baadhi ya watoto ambao walishuhudia tukio hilo.

waliweza kutoa maoni yao na kuomba Serikali kuimalisha ulinzi siku za sikukuu kuweka ulinzi mkali ikiwemo kwenye baa na kumbi za starehe ilikupunguza matatizo kama haya yanayotokea kwa watoto.

“Tunakumbuka mwaka 2008, tukio kama ili lilitokea na kuweza kuuwa watoto 19, mkoani Tabora, hivyo hatutaki tena kushuhudi vifo vya watoto wenzetu vikiendelea kutokea kwani hawana hatia” walisema baadhi ya watoto waliokuwa na umri miaka 15/17 ambao ni wanafunzi wa kidato cha pili na tatu wakazi wa Temeke.

Mpaka sasa Serikali imeunda tume maalum kuchunguza Sakata hilo huku mmiliki wake akiwa anashikiliwa na jeshi la Polisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi bila kupendelea wala kusema lolote naomba nitoe hoja. Mbona Huyu dada sikuona mahali alokwenda kuhani kule Tabora mwaka jana au kuhani kwa watoto mazeruzeru au ukipenda kwa kimombo Albino walouawa???? Iweje ni mwezi huu na aende amevalia kihivyo?? Michuzi sisi wengine hatuna vyama ila it is too much please kama unataka blog yako iwe ya kila raia try to be impartial tumechoka kila kukicha hayo hayo. Kama si hayo ni mambo ya uzuri. Tupe kero au maendeleo ili tujue linalohitajika nyumbani siyo hao watoto wanaotumiwa na mafisadi kujijenga. Kwanini wasiwaweke wajukuu zao kufanya hizo kazi?

    ReplyDelete
  2. ni vile hii ni africa tu ingekuwa kama ni ulaya watu wangefungwa hapo mpaka basi tena.... yaani mnafanya toto disco? kwanini badala ya kuwapa moyo wajiendeleze shule, hayo mambo ya kutafuta kwao pesa wanatakiwa wafungwe milele.

    Poleni wafiwa

    ReplyDelete
  3. Eti nini?...................

    ReplyDelete
  4. This sound redicolous, Mwenyekiti chipukizi giving out rambi rambi to the family of the victims, sound like a comic script.

    Nahitaji mtu mzima, muhisika, na siyo some kid tell me "Pole sana ndio maisha, unajua I feel you I have two children myself !" LOL! Redicolous, let the little kid attend schools and concentrate what best for him/her and not giving him combat and start encourage everyone to be civil, thats not the way to do it, probably MUSEVENI was right giving arms to little kids, he would argue in the same case, we are all becoming mature at 12yrs old..WHAT A CIRCUS

    ReplyDelete
  5. Mwandishi ametumia neno "kudhuru" mahala sio pake. Neno halisi ni "zuru" ukinyanyambua unapata "ziara" kidogo kidogo tutafika

    ReplyDelete
  6. Howa watoto walitakiwa wawe darasani, wana fanya nini hapa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...