Naibu Khadhi Mkuu wa Zanzibar Shekhe Khamis Haji Khamis akiwakabidhi akiwakabidhi Mafuta ya kula watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu wa mjini Unguja Zanzibar mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Foundation kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation na kutoa misaada ya vyakula, mafuta ya kula,madafutari pamoja na mbuzi 12 kwa ajili ya sikukuu ya Eid el Fitr,Vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 2.
Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Foundation,Mwamvita Makamba (mwenye baibui) akikabidhi Mbuzi na vyakula kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu wa mjini Unguja Zanzibar kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation na kutoa misaada ya vyakula,madafutari pamoja na mbuzi 12 kwa ajili ya sikukuu ya Eid el Fitr,Vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 2.
Mtoto yatima Sharifa Khamis wakidato cha tatu(10) akimuonyesha uhodari wa kuandika Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa Unguja Zanzibar , Vodacom Foundation walitoa misaada ya vyakula,mafuta ya kula,madafutari pamoja na mbuzi 12 kwa ajili ya sikukuu ya Eid el Fitr,Vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 2.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. ni kidato cha tatu, au darasa la tatu?.

    ReplyDelete
  2. kidato cha tatu at 10 years?

    ReplyDelete
  3. its dat necessary?givin sadaqa and show off how much you spend?wrong absolutely wrong.

    ReplyDelete
  4. Sheikh Akbar Ibrahim.September 10, 2010

    Kwanza : nadhani ulimaanisha kusema darasa la tatu na sio kidato cha tatu sababu binti anaonekana ana miaka kato ya 9-11.

    Pili : kwa muislamu unapotoa sadaka hairuhusiwi kutangaza umetoa kiasi gani na ndio maana msikitini ikipita kofia au sanduku au kikapu cha sadaka sunnah ya mtume Mohamad (S.A.W) inasema jaribu kukizuia kile ulichonacho kiasi kwamba mkono wako wa kushoto usifahamu wa kulia umefanya nini, maana yake ifanye iwe siri yako na Mungu wako kwani Mwenyezi Mungu hakupi kwa wingi wa unachokitoa na badala yake anakupa kwa ile nia yako na uwezo wako.

    Eid Mubarak.

    Wabillahi Tawfiq.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...