Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh. Mwanaidi Maajar akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Marekani Barack Obama mara baada ya kukabidhi hati ya utambulisho wa Balozi wetu huyo nchini humo.
Rais Barack Obama wa Marekani akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wetu nchini humo Mh. Balozi Mwanaidi Maajar (katikati) pamoja na mume wake, Bw. Shariff Hassan Maajar pamoja na mjukuu wao Kai-Hassan katika Ikulu ya Marekani wakati alipokabidhi hati ya utambulisho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. MAMA WA KICHAGGA HONGERA SANA KWA KAZI YAKO NZURI ULIYOIFANYA UINGEREZA. WE ARE LOOKING FORWARD KUKUONA UNAENDELEA KUIWAKILISHA TANZANIA VIZURI. MUNGU AKULINDE AKUPE AFYA NZURI NA MAISHA MAREFU.

    ReplyDelete
  2. obama na balozi wetu wamefanana. balozi wetu amependeza kweli. huyu mama ni beautiful, anajua kujipamba na anavaa vizuri sana.

    ReplyDelete
  3. Karibu Amerika, Mama Balozi.

    Mdau Atlanta.

    ReplyDelete
  4. Beautiful moment caught on camera..!

    ReplyDelete
  5. CCM oyeeeeee OBAMA ahsante kwa kuitambua CCM kuwa ndiyo chama pekee bora Afrika nzima..

    ReplyDelete
  6. CCM oyeeeeee OBAMA ahsante kwa kuitambua CCM kuwa ndiyo chama pekee bora Afrika nzima..

    ReplyDelete
  7. yaani hawaonyeshi kama wana mjukuu haswa mumewe. kwa kweli nimefurahishwa sana na mheshimiwa maajar manake anatupa moyo sie wanawake kujiendeleza zaidi licha ya kwamba kuwa kiongozi ni ngumu na pia namwonea wivu mjukuu manake hata yeye kafanikiwa kumwona kaka obama tetete

    ReplyDelete
  8. Mdau wa pili hapo juu umeniwahi, ni kweli kabisa balozi majaar anafanana sana na obama, utadhani mtu na sister wake.

    ReplyDelete
  9. Mungu atusaidie tuwe na mabalozi kama wewe hamsini; kazi unayoifanya inatupa matumaini kwamba nchini mwetu kuna wazalendo wa kweli.

    ReplyDelete
  10. Wanameremeta!

    ReplyDelete
  11. The KaiondosOctober 04, 2010

    Baba na Mama Maajar, kwa kweli tuna wamiss sana, tunazidi kuwaombea kwa Mungu hata huko mlikokwenda mkaendeleze kazi nzuri kama ambayo mmeifanya hapa UK. Mungu azidi kuwabariki pamoja na familia yenu. Tunawapenda sana.

    ReplyDelete
  12. Wote hamjui kufananisha, wiki mbili zilizopita nilikuwa naelekea Tanzania nikiwa terminal 5 heathrow airport mule ndani tunasubiria kile kitrain kitupeleke kwenye gate letu kaja mama kasimama mbele yangu kumcheki nikasema Mama shikamoo kageuka kaniitikia,hapo mimi najua ni Mama Balozi kumwangalia vizuri kumbe ni MRS MANDELA, MAMA GRACIER MACHELL na kaitikia kabisa marahaba hujambo?. Nilistuka nikasema haiwezekani yuko mwenyewe haikupita mda bodyguard huyo na nahisi walikuwa zaidi ya mmoja. Michuzi weka picha ya balozi na mrs madiba ili wadau wajue naongelea nini, yaani ni mtu na dadake kabisaaaa!

    ReplyDelete
  13. Shemeji Balozi wetu marekani, hongera sana kwa kumshirikisha mjukuu wetu kwenye sherehe ya kujitambulisha kwa rais wa marekani. Hapa Norway sisi pamoja na dada yetu H. tumefurahi sana na kujisikia PROUD ya wewe na mmeo na mjukuu wenu kuingia White House. Hongera sana shemeji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...