Salam Ankal

Tanzania na nchi nyingine mbalimbali za kiafrika zinaweza kunufaika zaidi kama zitaweka kipaumbele utumiaji wa nishati endelevu

(Sustainable Energy) hususani vijiji ili kuleta maendeleo na kupunguza umasikini. Nishati endelevu hutoka kwenye mwangaza wa Jua, Maji, Takataka na Kinyesi cha binadamu na wanyama. Hizi nishati mbadala hutoa umeme na gesi ambazo hutumika majumbani kwa kupikia na kuwasha taa hivyo kusaidia kutunza mazingira yetu na kuondoa utumiaji wa mkaa unaosababisha uharibifu wa mazingira kwa ukataji ovyo wa miti

Urban Pulse inawaletea documentary sehemu ya Pili kwenye version ya kiswahili, Documentary hii mpya ambayo tayari imerushwa hewani kwenye vituo tofauti vya Televiseni za nchi mbalimbali za bara la Ulaya na Afrika na imetafsiriwa katika lugha saba mbalimbali.

Documentary hii ambayo Ashden wali wa kamishen URBAN PULSE kuizalisha inaonyesha na kuhamasisha wajasilimali, wananchi namna gani nchini za kiafrika zinavyonufaika na misaada hii kutoka shirika la hili la Ashden Awards For Sustainable Energy.

Shirika hili ambalo lina saidia kukuza utumiaji wa nishati endelevu, lina saidia uboreshaji na utunzaji wa mazingira duniani . Shirika hili liliundwa na duka maarufu la familia ya kitajiri ya Sainsbury. Mlezi wa shirika hili ni Mwana Mfalme wa Wales Charles Philip Arthur George

Asanteni,

Urban Pulse Creative

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hii ni habari ya kipumbavu sana,kwani hata sijui inasaidia nini Tanzania.Nchini Kenya ni wafinyu wa Natural resources.Kwa Tanzania kuna vyanzo vingi sana kwa maji amabavyo vina weza kuwapa wananchi umeme kwa 24/7 nchi nzima.Hii inaitwa bora liende habari.

    ReplyDelete
  2. mi hata sion mantiki ya hii habar sijui sinsbury sasa sie tufanye nin,kama mdau amesema haina manufaa kwetu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...