Shirika tanzu la taasisi ya misaada la Ufaransa, agence francaise de developpement,(AFD) leo limesaini makubaliano ya kuipatia benki ya Exim tawi la Comoro mkopo wa Euro milioni nne kusaidia wajasiriamali nchini Comoro.
Makubaliano hayo yamefanyika leo katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo ya Jijini Dar es Salaam katika hafla ambayo benki ya benki ya Exim iliwakilishwa na Mwenyekiti wake wa Bodi ya Wakurugenzi Bw.Yogesh Manek wakati Proparco iliwakilishwa na Mwakilishi wake Mkazi wa Kanda Bw Mr.Ghislain De Valon .
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo Bw. Manek alisema fedha hizo zitasaidia kuimarisha ujasiriamali visiwani humo na pia kuimarisha nafasi ya benki yake nchini Comoro.
“Mkataba huu ni wa miaka saba, kama ilivyo kwa Tanzania, fedha hizo zitatusaidia kuendesha mafunzo na mikopo kwa wajasiriamali nchini humo,” alisema Mwenyekiti huyo.
Bw. Manek alisema mkopo huu ni wa tatu tangu mwaka 2003 wakati taasisi hiyo ilipotoa fedha kwa mara ya kwanza kwa benki hiyo.
“Benki yetu imeshanufaika na mikopo ya Proparco ambayo iko katika viwango mbalimbali vilivyotuwezesha kutekeleza programu mbalimbali za kusaidia ujasiriamali kwa wajasiriamali wadogo na wa kati katika kukuza sekta ya kilimo.” Alisema.
Alisema fedha hizo zitasaidia kuwaendeleza wajasiriamali nchini Comoro.
Akizungumza katika hafla hiyo, Bw.De Valon, alisema taasisi yake inafarijika kufanya kazi kwa karibu na benki ya Exim ambayo mbali na kujitahidi kuboresha maisha ya Watanzania pia inafanya hivyo katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
“Uhusiano wetu na benki hii ulianza miaka saba iliyopita, kizuriu ziadi ni kwamba benki hii imekuwa ikikua kila mwaka na kuwa miongoni mwa benki kubwa hapa nchini na kwa kweli tunaipongeza kwa ubunifu inaoufanya kwa lengo la kutoa huduma bora,”
Alisema PROPARCO ilianzishwa mwaka 1977 lengo lake likiwa ni kutoa fedha kwa nchi zinazokua kwa kuisaidia sekta binafsi.
“Taasisi hii imeshatoa Euro bilioni moja kwa nchi zaidi ya hamsini lengo likiwa katika kukuza sekta ya ujasiriamali katika nchi katika uendelezaji mazingira na kukuza utawala bora,”
Alisema taasisi yake inaona faraja kuona kwamba fedha inazozitoa zinakwenda kuboresha maisha ya wananchi wa Comoro sanjari uchumi wao .
“Pia ni matumaini yetu kwamba fedha hizi zitauboresha uchumi wa Comoro na hatimaye iweze kujitegemea” alisema.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...