Je Wenzetu Wamasai wenye mila
imara (strong culture) wanaelekea wapi?
Koo zao zina ubunifu na akili nyingi kwani wamesambaa Afrika Mashariki, kaskazini na Afrika Kusini. Ni wapiganaji kimaisha. They have undoubtedily a strong socio-cultural values in Tanzania. Tunasikia wanauza miti shamba kuko Sudani na Misri na huishi au kufika huko bila passport.
Wanakuwa viongozi wazuri (good leders) wapatapo fursa na mifano hai kama Hayati Sokoine. Wa sasa ni Lowasa, Ole Sendeka, Kina Molel nk. Wengine wameoa wazungu na kwenda kuishi Ulaya na nimekutana nao Handeni wakiongea Ki-spanishi, Italiani na Kifaransa. They area also included in the culural tourism around nationalparks like Manyara.
Wakoloni walilitenga eneo la Maasai Lands kwa ufugaji (pastoralislism) tu na lilionekana halifai kwa Kilimo wala makazi. Sasa hivi kama sikosei ndio wilaya za Simanjiro, Monduli, Ngorongoro, Loliondo na Odeani?. Hizi hazikuonekana kuwa maskani ya watu bali ufugaji wa kuhama hama. Hivi karibuni madini ya thamani yameonekana huko. Pia wana raslimali nzuri za misitu na wanyama na hivyo utalli mkubwa.
Ndugu zetu hawa ambao walishawekwa picha zao kwenye noti ya Tanzania kutokana na utamaduni wao usiotetereka wanaonekana katika miji yote ya Tanzania Bara na visiwani wakifanya kazi za ulinzi wa maeneo ya biashara, mahoteli na makazi. Wengine wanauza urembo na dawa feki ajira isiyo ya uhakika. Wengine wamekuwa wasusi. Utashanga wanauza madawa ya miti shamba na kuyachanganya na ya kisasa na hivyo kuonekana yanafaa. Akili kubwa. Pia wanachezesha michezo ya pool na kuongoza watalli. Huko Zanzibar wamezushiwa jambo - kufanya michezo michafu ya n****. He wengi huishi upenuni na kwenye majengo/maghorofa yanayojengwa. Wengine wameshtakiwa kwa vitendo vya uvunjifu wa uhalifu ; wizi nk.
Najaribu kupata sababu ya mabadiliko yao hasi ya kiuchumi na kijamii. Je tuseme sababu ni zifuatazo??
- Matatizo ya hali ya hewa inayoleta ukame hivyo kuwakimbiza makwao??
- Ni udongo duni ,ukosefu wa maji na mvua za uhakika??.
- Uchukuaji wa ardhi (land excision and invasion) kwa hifadhi ya wanyama na misitu kama vile Ngorongoro Crater. Au
- Uchukuaji wa maeneo ya uwindaji kama Loliondo na Monduli.
- Ni sera zisoziwajali kama zile za Wawekezaji kuvamia maeneo yao na kuwasukumia mabonde ya Rufiji na Kilombero/ Mahenge au Mbarali hadi Ruvuma
- Ni uwekezaji wa madini au kutengwa maeneo ya miji kama Monduli nk
- Je wanahadaliwa na wanasiasa wajanja wasioweza kuwakilisha matakwa yao.
- Wameshindwa kwenda na technologia na uhitaji wa elimu kutokana na kufungwa na mila.
- Ni wao kukumbatia mila (kutobadili mfumo wa uchumi kama kuuza ngombe na kwekeza mijini?? Kutokubali wageni na kuchanganyika au kuozeana (intermarriage) has wake zao.
Hata hivyo kuna mabadiliko yameyakubali haraka kama televisheni, baiskeli, simu za mikononi nk. Pia akina mama wanaukubali ulokole (new evangelism) na kuhoji mila potofu kama za kuhalalisha ugoni.
Naomba maoni yenu jinsi ya kuwasaidia wenzetu hawa na kulinda mila zao. I am not trying to provoke them but challenging them so that they continue to stay a top as big culture ethnic group in Tanzania.
Thanks
Richard Mazingira

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Challenges(Changamoto) inazoikabili jamii hii, pia zinakabiliwa na jamii zingine mbalimbali kote Tanzania, iwe mijini au vijijini.

    Mfano
    Watanzania kutomilikishwa ardhi kisheria(hati za ardhi vijijini au viwanja mijini).

    Ardhi/viwanja vilivypopimwa na kupewa hati vingewawezesha Watanzania wa jamii zote kupata mikopo benki, kuingia ubia au kulipwa fidia.

    Elimu na Afya huduma ni ghali sana kwa Watanzania wote, hivyo huduma hizo zingetolewa bureee.

    Masuala ya mmomonyoko wa maadili wanasikika pande zote za Tanzania, jamii hizi za Watanzania zitaingiliwa na tamaduni ngeni toka nje ya Tanzania na Afrika kutokana na utandawazi.

    Mwisho, Tujifunze sote kuupenda utamaduni wetu wa kiafrika.

    ReplyDelete
  2. (Nje ya mada).. kuna uwezekano mechi ya Tanzania na Moroko kuonyeshwa hapa

    http://www.ilemi.com

    angalia link ya Tanzania Vs Morocco

    Kwa walio mbali na nyumbani inaweza kusaidia.

    ReplyDelete
  3. umesahau kusema hata kwenye miss TANZANIA utamaduni wao ndo unatawala.mamiss TANZANIA wote wanao kwenda ngambo au baadhi yao huwa wanavaa KIMASAI kama vazi la taifa.mpaka kitchen party za sikuhizi nyingi theme inakuwa kimasai.walinzi wa nyumba yani askari ni Masai.

    ReplyDelete
  4. hali ya maisha ndo yamechangia . binadamu wanabadilika kutokana na mazingira yanayo mzunguka . sasa wewe unazani tuachunhga mbuzi adi lini, pia viongozi wao wameshindwa ku revolve na hali ya maisha ya wakati.

    ReplyDelete
  5. Ndugu Mazingira kazi ya kupuyanga na mifugo siyo kazi ndogo. Unatembea kuanzia asubuhi mpaka usiku hiyo television utaiangalia saa ngapi?

    Wamasai nao wanakwenda na wakati, hivi sasa baadhi wamekuja mjini na wengine wamekwenda shule na wameona wenzao wanavyokula kuku kwa mrija kwa hivyo wakaamua kubadili katabia kidogo.

    Vile vile hiyo ardhi ya kupitapita huku na kule na hasa katika yale maeneo yao ya asili haipo tena kwa asilimia kubwa. Kwa hivyo ni lazima sasa wanunue ardhi na wakae kwa kituo ili wafuge vizuri. Mfano wale waliopo maeneo ya Dakawa.

    Idadi ya mifugo siyo issue tena bali quality ndiyo yenye thamani kwa sasa.

    ReplyDelete
  6. mijini tu watu wanalia njaa , je wewe uliye kuwepo porini service bora zitakuifikiaje.

    ReplyDelete
  7. Mimi naona thesis yako iko nje ya point. Umesema toka mwanzoni wanafanya hivyo vitu kwa vile wana akili sasa leo kama wanafanya the same things lakini in a high modern way..what's wrong with that? Toka mwanzoni wao ni nomads sasa ukimwpna leo kawa mlinzi kesho kaenda sijui kutengeneza dawa ni all the same as before ...Fighting to stand on this world. That is all about the power of survival. That has nothing to do with any of your arguments sababu kama nchi ingekua imeendelea na kuwaacha wao nyuma basi ningeanza kujiuliza why na ku pin point the answer but the whole country is in the same S**t..Do we really need to say more? Go figure

    ReplyDelete
  8. Mimi ni mmasai. Sijaona ubaya wa ulioyasema. Hii hali ya kuhifadhi mila na desturi za kabila fulani limekua changamoto sio tu kwa wamasai bali kwa jamii nyingi duniani. Baadhi ya sababu umeshazieleza kama ukuaji wa maendeleo ya watu, teknologia na mengine.
    Huwezi kubaki vile vile wakati hata nchi na viongozi waliopo madarakani wanauza makazi yako au wanaamua tu kufanya wanavyotaka bila kukushirikisha. Mfano kama ukiangalia maeneo yaliokua yanaitwa makazi ya masai(Masai land) sirikali au serikali inayabadilisha na kuhamisha makazi ya watu bila hata kuwafikiria wataishi wapi na wataenda wapi mfano halisi ni Ngorongoro na upitishaji wa njia ya usafiri Serengeti.
    Wamasai wameishi kwa muda mrefu pale na hawana alternative zaidi ya kubadilisha mfumo wa maisha.
    Nafikiri suluisho zuri la haya ni elimu na serikali kuweka vipao mbele watu, mila zao kwanza na sio faida za kutabirika.
    Bado mila yetu ina nguvu na itachukua muda kupotea maana tumewaambukiza na wengine wameiiga. Tuungeni mkono kudumisha mila sio tu yetu bali ya watanzania wote.
    http://www.savetheserengeti.org/issues/stop-the-serengeti-highway/#axzz11vsvLHtj
    Aircraft system engineer.

    ReplyDelete
  9. the world is changing and everything in it is changing as well. the masai are clever i mean we are smart..thank you for that!!!! but sorry you can not help us maintain our culture how dare can you say that..you have one of your own to take of, so why don't you shod off.... yes we move for the green pasture just like any other human being and we have always done so.

    "Najaribu kupata sababu ya mabadiliko yao hasA ya kiuchumi na kijamii. Je tuseme sababu ni zifuatazo??
    every single reason that you have listed does not make sense. every body is facing the same problems either from developed or underdeveloped countries whatever you want to put it. everyone is rolacating nowadays.... leave alone masai they have always done so even before anyone else..
    and for more information hatujashidwa kwenda na technologia,,, we are on top of our game..so watch your words... OLE SERE

    ReplyDelete
  10. zitto-kiaratuOctober 11, 2010

    sio wamasai peke yao pia kuna wabarbaig,wambulu n.k. hawa wote wanachukuliwa hifadhi zao na kuuzwa na mafisadi wa chama tawala, wakuria,wazanaki wamefaidika kwa kupitia mtakatifu nyerere, nakumbuka miaka ya sabini wamasai vijijini walikuwa wananyolewa nywele kwa nguvu na askari eti wanalazimishwa maendeleo, huu ulikuwa ujinga wa serikali tawala kunyanyasa watu hawa hadharani, makabila yote niliyotaja hapa sio wabantu kama sisi ambao tunadhani nchi hii ni ya wasukuma,wanyamwezi,wangoni n.k.

    ReplyDelete
  11. Nakubaliana na wengi waliochangia ila kingine kinachochangia hali hii ni SERIKALI KUANZISHA MIRADI ISIYO ENDELEVU mfano wamasai kwa muda mrefu wamekuwa watundu kwa kuwa na madawa yao asilia kuanzia mofugo mpaka binadamu, lakini kutokana na kuanzishwa kwa miradi mbalimbali kama majosho ya mifugo na chanjo za mifugo ambazo hazikudumu imepelekea mifugo ya wamasai kupoteza kinga asilia hivyo imeshindwa kuendana na mazingira yaliyopo na kuanza kufa hasa ukizingatia hata hizo chanjo na majosho ambayo serikali imeanzisha hayapo tena. Mifugo inapokufa imebidi wengine wajaribu kufanya kazi mbadala kama alieanzisha mada alivyosema, kwa kumalizia MILA ZA WAMASAI NI NZURI SANA ILA SERIKALI NDIO IMESABABISHA YOTE HAYA KWA KUWANYAMGÁNYA MAENEO YAO HASA UKIZINGATIA mfumo wa maisha wa wamasai ni rafiki wa mazingira tofauti na makabila mengine ambayo yakivamia sehemu lazima mazingira nayo yanaharibika, mie mdau Igwamanoni from Mwanza

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 14, 2012

    Wadau wa Michuzi Blog. Takribani miaka 2 ilopita nilianzisha hii mada. Nimefarijika sana kuona Jinsi wadau walivyochangia mawazo yenye rutuba na ya kuelimisha umma kuhusu mila na matumiza ya rasilimali zetu za ardhi. Naona hizi blogu zinatujenga sana.nking you a Million. Thanks Ankal
    Richard Mazingira
    14 May 2012

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...