Ankal salamaleko,
Siku nyingi yakhe sijatoa tamko kwenye Globu yetu hii ya Jamii. Basi leo kwa hishma na taadhima nipe nafasi japo kiduuuuchu nieleze dukuduku langu lililonikaba rohoni siku nyingi. Dukuduku lenyewe ankal ni kuhusu mfanano wa vipindi vya redio na TV zetu hapa nyumbani. Inakera kwa kweli - sasa sijui ni mtindio wa ubunifu kwa kisingizio cha ushindani ama basi tu bora liende. Wadau watanisaidia kwa hilo maana naomba msaada kwenye tuta la mwisho.
Ni hivi, mie ni msikilizaji mzuri sana wa redio (zote tu, sichagui wala sibagui) ilimradi napata ile kitu roho nataka. Tatizo ni huo mfanano wa vipindi kuanzia mawio hadi machweo. Yaani inakuwa kana kwamba unasikiliza kituo kimoja tu cha redio, hasa hasa vituo vya Dar es salaam. Huko kwengineko sifahamu maana masafa yao sipatagi.
Ukianzia na asubuhi karibu vituo vyote baada ya kufungua na kusoma taarifa za habari, hufuatia mapitio ya magazeti. Kisha zinaanza porojo za kupitisha asubuhi. Vituo vyote vya redio vinavaa sare hapo nikimaanisha ukisikiza huku na kule utakuta yale yale.
Haya; na tuje baada ya saa tatu asubuhi hadi mchana. Hapo utakutana na mipasho na mishauzi karibu katika vituo vyote, kuanzia Radio One, Clouds FM na huko Times FM, TBC Taifa. Magic FM na kadhalkika nako ndio usiseme. Vijembe na umbea kwa kwenda mbele. Inafurahisha kiasi, tatizo ni pale mfanano unapochukua nafasi yake.
Baada ya taarifa ya habari saa saba, kuna muziki mwororo eti wa mlo. Basi wote hupiga muziki huo na wengine kuzungumzia maakuli. Baada ya hapo Bongo Fleva kwa kwenda mbele - Vituo vyoooote hadi inaboa.
Kijua kikianza kutua balaa huzidi. Kila kituo kinaleta zile porojo kama za asubuhi pamoja na mapitio ya magazeti ya mchana. Jioni kwenye taarifa za habari na michezo, japo hapo kwa saa tafauti, lakini mambo ni yale yale. Sare sare maua hadi basi. Wakati Ijumaa usiku kila kituo hujikita na miondoko ya reggae, Jumapili jioni nako ni taarabu na mipasho.
Kwenye TV nako kadhalika. mambo ni hayo hayo. Juzi alhamisi ndio nilichoka kabisa kukuta Ze Comedy (akina Bambo na wenzie) ITV na TBC one kulikuwa na Orijino Komedi (ya akina Masanja na wenzie) na muda huo huo mmoja. Nikajiuliza sasa hii ni ushindani ama zogo tu. Hata hujui uangalie wapi. Kwa upande wangu muda huo wa alhamisi saa moja unusu hadi saa ngapi sijui naona nanihino bado wako juu. Hivyo wakina nanihino wengine sio tu wafanye 'homework' kuwapiku wenzao bali pia wangechagua muda mwingine maana nina hakika wanakosa watazamaji wa haja - japo nao ni wazuri kwa mitizamo tafauti.
Kwa leo ni hayo tu Ankal. Naomba wadau wachangie mada hii ili kama kuna mwenye macho na asikie na mwenye masikio aone ili kama kuna marekebisho yafanyike kwa mantiki ile ile ya 'Mteja ni Mfalme' na kwamba sie wateja tunaboreka kwa mifanano ya vipindi.
Hata sijui wamatumbi tumeitoa wapi tabia hii ya kuigana na kuwa sare sare maua kwa kila kitu. Yaani mtu ukifungua grosali basi ujue mtaa mzima nao watafungua. Ukianzisha show room ya magari, basi kila mtu zinayemuwasha anafungua yake...Najua ntapigwa madongo, sijali sana kwani kwenye ukweli uwongo hujitenga. Ila redio na TV za Bongo zinaboa kwa kuigana!!
Ndimi Mdau Mkere Ketwa,
Kigamboni, Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. hii yooote ni kutokana na kutokuwa wabunifu, kitabu kina saidia sana !

    ReplyDelete
  2. Duu!! Kweli mtoa mada nadhani tatizo hilo la kuigana ni kubwa kuliko unavyoliona. Ukiacha hivyo vituo unavyosema njoo kwenye bendi zinazotumbuiza huwezi kujua huu wimbo ni wa wazee wa masauti au wa academia gani sijui. Kwenye bongo fleva huko ndo funga kazi yaani ni kuigana kwa kwenda mbele...sijui kifanyike kitu gani mwe! Mtindo huo wa kuigana kwangu naona ni uchakachuaji tu wa ubunifu wa kazi za watu...haipendezi.
    Ben

    ReplyDelete
  3. kwa kukusaidia tu mtoa maoni.
    wanafanya hivyo kutoka na survey ya listeners. mfano asubuhi wanasoma habari na kuchambua magazeti na habari zilizo serious kidogo WHY? wanaosikiliza wanataka kupata habari kabla hawajaianza safari ya siku pia wengi kwenye magari wanasikiliza radio zao wakielekea makazini. saa 3 kati hivi vipindi vya kuelimishana mipasho etc ukiangalia sana kaka wana target % kubwa ya wakina mama wa majumbani, watu ambao kama elimu haijatolewa namna hii hawasikilizi radio mfano muda huo uwe na kipindi kinaitwa KUTOKA MASHAMBANI au DIRA YETU hamna atakae sikiliza ndio maana wanawaelimisha kiihivyo. ikifika mchana i tell you kama unaendesha gari unaumwa kichwa kama wanapiga sana miziki ya kuruka na majoka! ingawa sasa vijana wengi wametoka shule(wale wa shift) ndo hua wanasikiliza kufoka foka kama clouds but radio one labda wanajua saa hizi mlo wanawafundisha wanaopika mlo wanaongeza idadi ya kutumia restaurant na wanakupa mziki mlani coz that tym unakula and psychologically u need to have something softer to go with ur food. kisha after hapo mayb radio one wanakumbuka watoto wa sec wanatoka shule shift ya mchana ni wengi hivyo wanapigiwa kufoka foka wao na radio clouds wanafanya hivyo. then trafic jam, unasemaje, kutafutana na jahazi which is soft news. umekaa kwenye gari masaa mawili u need to listen to something. ndio maana wanatumia hivyo. nimechoka kuandika bwn i hope nimekujibu. about michezo ni muda huo ili watu wote wasikose kipindi hicho vile wote wanakua hometht tym. then habari then a bit of informative kipindi then unabembelezwa ulale need i say mo? hata mtoto ataona hili!!!! so ni culture ya wasikilizaji na aina ya listerners waliopo muda huo inawafanya wasikilize hilo! wewe mwenyewe honestly vipindi kibao vya radio tz husikilizi kiivyo viko so straight frwd yaani vimekaa kibunge bunge. lakini ukiangalia utakuta radio one wana chemsha bongo radio one dr vipindi vya watoto etc we check muda utajua hata clouds kile kipindi chao cha mchana jumapili hata hivyo vya mchana vinaelimisja!!! juzi nilisikia wanawake wakiambiwa waache kutukana mama wakwe zao! the way kina gea walivyokitangaza. kinafikisha ujumbe than wangetangaza RTD au ni TBC taifa

    ReplyDelete
  4. kaka wanahabari wanakimbia na wakati. na kila kizuri kinaigwa kibaya kinatupwa. ukibaki nyuma unaachwa na wanafuatwa walio mbele daima .

    ReplyDelete
  5. Habari za saa mbili usiku za ITV zinaanza na kibwagizo/tune ile ile tokea kituo hicho kianzishwe miaka 15 iliyopita. Tells you a lot.

    ReplyDelete
  6. Ndugu Mkereketwa, ungekuwa una kazi za kufanya na kukuweka bize, usingekuwa na muda wa kufuatilia matangazo ya kila kituo cha redio na TV na kujua wanarusha nini. Kujua ratiba ya kila redio na TV ni kazi sana, unless uwe huna kazi za kufanya. Ni mtazamo tu, wadau msijenge chuki.

    ReplyDelete
  7. Jamani Radio One Kabla hawajaanza kuiga walikuwa na vipindi vizuri sana kwa wiki nzima,sasahivi naona kama nao wamefulia tu,saa 3 mpaka 6 wanapiga makelele yasio na msingi wowote,unajua hata hizo porojo zao za saa3 si kila station zinavutia,nyingine ni makelele tu,mimi ni mama wa nyumbani na si kweli eti hivyo vipindi vinatulenga sisi,hata sisi pia tunataka kujua ya maana yaliyojiri duniani pamoja na kuburudika huku tukielimika,hebu RADIO ONE mjipange upya,tumechoka na makelele ya wale wadada,halafu wanabadilisha sauti zao za asili wanakuwa vichekesho,mfano Regina,una sauti nzuri sana,lakimi kwa yale makelele mmmmmhh una boa.

    ReplyDelete
  8. Hi Michuzi,
    Usibane hii. Toa maoni na usitukane.

    Mtoa mada naona naye ana matatizo ya kufikiri. Vipindi wanavyo rusha vingekuwa vibaya basi naamini hata TV au Redio asingeangalia. Ukweli ni kwamba vyombo vyetu vya habari vimejitaidi.

    Vipindi wanaviendesha kwa sababu ndo interest za watanzania, na nina ujakika wamefanya utafiti wa kutosha kabla hawajavirusha.

    Lkn pia ukitoa mawazo si lazima udharilishe watu kuwa wana mtindio wa ubongo, si lugha nzuri hiyo. Toa maoni na usitkane.

    ReplyDelete
  9. Mimi naona sio ukosefu wa ubunifu ila ni muamba ngozi huvutuia kwake..Wanaona wakieka vinavyofanana basi utakimbilia kule kwenye the best

    Huku tuliko radio siwezi kusema ila TV ni hivyo hivyo...Nazungumzia local tv za NY city sijui wengine niaje talk asubuhii zote ni news halafu zinakuja talk show yaani ni kila moja na style yake lakini mambo yale yale..the Drs, sijui Rachel ray, the view na yule kibabu na mjukuu wake sijui halafu wakimaliza hiyo zinaanza court shows mara the people's court, judge Mathias, judge judge , street judge, sijui judge yule, wakimaliza hapo ni jioni news tena halafu ndio zinaanza hizo reality shows zao...Kila kitu ni reality TV siku hizi...yaani local free channels ni taabu bora ulipie cable ..halafu ukidownload app zao ukaruhusu pushnews utakoma...wanakimbilia kurusha habari hata kama hawajawa na uhakika..Talking about I wanna be the first one to say this...

    ReplyDelete
  10. Ubunifu na kitabu ni vitu viwili tofauti, mtu anaweza awe na kitabu (Elimu) lakini asiwe na ubunifu, au anaweza kuwa na ubunifu mkubwa sana lakini asiwe na elimu.

    ReplyDelete
  11. mtoa hoja, nikuweke waki hapo..ni kupindi cha comedy cha ITV, yani wale kina bambo na wenzao wanaboa vibaya, ni heri wangetafuta muda mwingine watu waanze kuangalia kwa kupass time labda watapata wachache watakaoshow interest, hawawezi kuweka same time na origino comedy wakidhani wanacompate, wale wamesomea sanaa, si tu talent, talent na kisomo!yani ptu!

    ReplyDelete
  12. Kaka michuzi,mie naomba kujua taratibu za kumuona mkuu wa kaya(JK)inakuwaje,,ni personal na ni yeye aweza toa ufumbuzi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...