Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata keki wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuzaliwa kwake pembeni yake ni Mama salma Kikwete na mjukuu wao Karima wakishuhudia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlisha kipande cha keki mkewe Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya kuadhimisha kuzaliwa kwake miaka 60 iliyopita.Sherehe hizi zilifanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimlisha kipande cha keki Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherehe ya kumpongeza Rais Kikwete kwa kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake jana jioni.Sherehe hizo zilifanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam(picha na Freddy Maro)
kwa picha zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Hongera, sana Mista Prezida!

    ReplyDelete
  2. HONGERA RAISI KIKWETE KWA BIRTHDAY YAKO. JAMANI RAISI KIKWETE NA MKE WAKE WAMEPENDEZA SANA. WEWE RAISI NA MKE WAKO MNAPENDA SANA WATOTO NA HILO NI JAMBO ZURI SANA. KUNA WATOTO KWA BAHATI MBAYA WAMEPATA MIMBA NAJUA NI VIZURI WATOTO WAFUNDISHWE HAYO YASIWATOKEE LAKINI KWAKWELI SI VIZURI KUWAZUIA WASIFANYE MITIHANI. SISI WOTE TUNAJUA KUWAZUIA WASIENDELEE NA MASOMO NI KUWARUDISHA NYUMA KIMAENDELEO NA KUWAFANYA WAZIDI KUWA MASIKINI PAMOJA NA FAMILIA ZAO ZA BAADAE. HILI JAMBO NI LAZIMA SERIKALI LILI SHUHULIKIE. RAISI WETU KIKWETE NINAJUA UNAPENDA MAENDELEO NA UNAFANYA BIDII KUONDOA UMASIKINI AND NOT TO FORGET UNAPENDA WATOTO, PLEASE DO SOMETHING TO HELP THESE KIDS.

    ReplyDelete
  3. Daaah!.. Mr. Raisi ameachama!..

    ReplyDelete
  4. Hongera president but I didn't like the cake

    ReplyDelete
  5. Hongera!..(Plastic smile on me).....ndo kilichobaki ati!

    ReplyDelete
  6. Hongera Ndugu JK. Tunamwomba Mwenyezi Mungu awalinde wewe na wanafamilia wako wote na awape kila la heri.

    ReplyDelete
  7. ama kweli tanzania tambarare!!!!

    ReplyDelete
  8. Bradha,

    Mbona sijamuona REGINAD MENGI kwenye hiyo hafla?

    ReplyDelete
  9. Kila la heri MH JK.

    ReplyDelete
  10. Happy birthday to you Mr President and we wish you all the best. Ole Koila and family.

    ReplyDelete
  11. Hongera Mr President kwa Birthday yako.Una miaka 60 unaitwa Rais kijana!!!! je na mimi mwenye miaka 40 nitaitwa mtot? wabongo acheni uzushi ndiyo maana bado tuko nyuma.
    ama kweli ukipenda,chongo huita kengeza!!

    ReplyDelete
  12. NATOA PONGEZI ZA DHATI KWA MH RAISI, WEWE ANON WA HAPO JUU,KWANI UKIKUBALI KWAMBA ANONEKANA KIJANA HASA UKIZINGATIA UGUMU WA KAZI YAKE NA MASTRESS YANAYOAMBATANA NAYO,HAINA MAANA ANAONEKANA MTOTO (KUONEKANA KIJANA MAANA YAKE KUONEKANA YOUNGER THAN HIS AGE 60) BADO ANA NGUVU KIAKILI NA KIMWILI ILI KUENDELEA KUMUDU YANAYOMKABILI, IKIWA JK NI SIXTY, HAONEKANI KAMA AMEMTANGULIA OBAMA KWA ALMOST 12 YRS.... HONGERA MH JK NA KEEP IT UP, MAMA SALMA UPO JUU
    MDAU NUTRO , KANADA

    ReplyDelete
  13. MTU WA WATU USIYE NA MAKUU. MUNGU AKUBARIKI MR PUREZIDENTI.

    ReplyDelete
  14. Jamani , hongera sana Raisi wetu!! kwa kweli unaonekana kijana ukilinganisha na umri wako!!!!!!!!!
    Jamani kula vizuri, fanya mazoezi na upumzike ndio unakuwa kijana kama baba yetu JK.Hongera mama first lady mwaya kwa kumtunza mumeo, ndio mwanamke mwema huyo hutunza familia yake kuwa yenye afya njema!!!!!! tukutane Octoba 31, pamoja tunaweza!!
    Msemakweli

    ReplyDelete
  15. Kazi na dawa jamani! Si kazi tuuu kazi tuuu! but ndugu wangeizunguka keki!!! au mliila hiyo keki watatu tu? MMEPENDEZA!! UONGO SI KAZI!!

    ReplyDelete
  16. Mama Salma anajua kuvaa. She real look beautiful. But I am sorry, this time I am going to be First Lady. Of course with Dr. Slaa!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...