Tunaomba ushirikiano wako

Kwa yeyote mwenye taarifa, au mwenye uwezo wa kutusaidia, asubuhi ya leo, Jumapili, Oktoba 3, 2010, kwenye eneo la maegesho ya magari nje ya Kigango cha Mt. Thomas Moore, Ally Sykes Close, Mbezi Beach, takriban saa 4 za asubuhi, wakati misa ikiendelea, gari aina ya Suzuki Swift iliyokuwa kwenye eneo hilo ilivunjwa kioo cha nyuma na mlango wa nyuma kufunguliwa, hatimaye kuwezesha baadhi ya vitu vilivyokuwamo ndani yake kuchukuliwa na mtu au watu
wasiojulikana.

Tunajua utadhani kwamba huu ni mtego. La hasha. Tunachotaka ni vitu hivyo kurejeshwa kwani ni hasara kubwa sana kwetu. Tupo tayari kukuzawadia kwa ushirikiano wako, kwani hatuna muda wa kwenda kufungua kesi Polisi au Mahakamani, kwani tuna uhakika kwamba kwa njia hii HATUTAFANIKIWA. Tunachokuomba ni uaminifu wako na imani yako, kwamba, hatutachukua hatua zozote za kisheria.

Tafadhali turejeshee vitu vyote vilivyokuwamo ndani ya gari, tuko tayari kukupa kiasi kizuri cha pesa kama shukrani yetu kwako. Muda wa kuomba upya kadi ya benki ya CRDB, kutafuta kitambulisho kipya cha kazi, kutafuta kadi ya mpiga-kura huku zikiwa imebaki siku chache sana kabla ya Uchaguzi Mkuu, na hii ni muhimu zaidi, kumbukumbu za namba za simu na picha zilizopo kwenye simu za mkononi (ambazo thamani yake haihesabiki), vyote hatuna muda wa
kufuatilia, ni hasara kwetu.

Tunajua kwamba ni dhiki ndiyo inayokusumbua, na kwamba, unaona kwamba hiyo ndiyo njia sahihi kwako kujipatia chochote. Hatuwezi kukuhukumu kwa kuwa maskini!

Tafadhali wasiliana nasi kwa namba za simu
0715-019119
au 0786-019019
ili tuweze kukutana nawe na kurejeshewa vitu hivyo.

Asante.

Familia ya Bw. na Bibi Aziz Losika Mongi

P.S. Ni bora tukayamaliza kati yetu kuliko kupelekana Polisi, ambapo hatutapata muafaka!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. Serikali na Wanakijiji wa Mitaa hasa hasa wanatakiwa waweke sungusungu kama Serikali hawafanyi kitu.

    Mie nashangaa Hasa maeneo ya huko Mbezi Kuna Kambi kibao za Wanajeshi na Kazi hawana kwanini hawapewi kazi za kulinda? au wao ndio Wezi? na wengi wakazi wa huko wanaibia mchana au usiku mida ya watu wanajirusha wengi watu wa kazi mjini wanasomwa.

    MZ.

    ReplyDelete
  2. KWA KWELI HALI HII INATISHA,MAMBO YA AINA HII YATAISHA LINI NCHINI KWETU?HASA HAPO DAR?WATU HAWANA HATA UHURU WA KWENDA SEHEMU WAKATOKA SALAMA,LAZIMA HASARA HATA VIFO VITOKEE,IMEKUWA KAMA NDIYO STAILI YA MAISHA YA MTANZANIA.HATUJUI HATA WA KUMLAUMU.
    POLENI SANA NDUGU MLIOIBIWA MALI ZENU,INASIKITISHA SANA KWANI PAMOJA NA UMASKINI ULIOKITHIRI KATIKA NCHI YETU,HUU SIYO USTAARABU HATA KIDOGO.
    MDAU, LONDON

    ReplyDelete
  3. HIIKALI YAKE,KULINGANA NA MAELEZO YA MLETA MADA YAELELKEA WANAWAJUA WEZI WAO SASA HAWATAKI KUWAPELEKA POLISI KWA KUWA NI KUPOTEZEANA MUDA,SASA KAMA UNAWAJUA SI UWAPELEKE KWA PILATO TU,SASA HAPA HUPUNGUZI WEZI UNAONGEZA VIBAKA,

    ReplyDelete
  4. dah!poleni sana.ila sidhani kama wezi /vibaka wa tanzania wameelimika kiasi cha kutumia teknologia ya matandao wa intanet.muhimu tangazeni redion au kwenye runinga, huo ni ushauri wa bure.

    ReplyDelete
  5. Hii ni approach nzuri iliyotumika ila neno dhiki nikama kashfa!
    Nahawa vibaka hawana access na mtandao.Ni vizuri ukawatangazia vijana wanaofanya shughuli zao jirani na tukio lilipotokea au vijiwe vya wahuni viliopo jirani.
    Pole sana.Usikate tamaa utavipata tu.

    ReplyDelete
  6. UNBELIEVABLE!!! Be carefull what you say,it mighty come back and HAUNT YOU!!

    ReplyDelete
  7. MIMI inaonekana nimekaa nje sana,hivyo vibaka wa bongo siku hizi wanasoma internet,maana sielewi huu ujumbe utamfikia vipi

    ReplyDelete
  8. KWELI BONGO AMANI HAKUNA KABISA.SASA ONA WATU HAWANA AMANI NA MALI ZAO,PIA HATA WATAFUTA HAKI NAO HAWANA IMANI NA VYOMBO VYA DOLA.......KWAKWELI HALI INASIKITISHA KILA NIKIONA MATUKIO YA AINA HII, HALAFU TUNAJIVUNIA AMANI, AMANI GANI HUKU WATU HAWANA AMANI NA MALI ZAO?????

    ReplyDelete
  9. Poleni sana Bw na Bi Mongi kwa upotevu wa mali zenu.Mimi nakaa Mbezi na eneo hilo nalifahamu.
    Hata hivyo ushauri wangu ni huu:
    -sidhani kama mhalifu aliyetenda hili anauwezo wa kupitia blog kama hizi
    -nimepita hapo na naona mnajenga fence, je mna walinzi hapo?
    =kama walinzi wapo, uzoefu unaniambia wanahusika sana
    -kanisani kwetu KKKT Mbezi huwa walinzi wanakuwa liable kwa loss yoyote ya mali ya msharika wakati wa ibada,losses zikawa minimized baada ya walinzi kutozwa upotevu.

    ReplyDelete
  10. Siwaungi mkono hao vibaka, lakini kwani uache au utembee na vitu vyote kwenye gari wakati unajua kabisa vikiibiwa ni viguu kuvi-replace? Hata kadi ya benki unaacha kwenye gari? Kwa kweli hapo unategemea nini? Kama gari ilikuwa tupu sidhani kama wangevunja. Hata huku Ulaya ukiacha hivyo vitu kwenye gari unavunjiwa. Sembuse bongo.

    ReplyDelete
  11. duh,poleni sana,serikali ipo busy na kampeni,mda wa kuwalinda raia haupo.jaribu kuongea na watoto wa vijiweni unaweza kuvipata,Tanzania amani hakuna kabisa,mungu aturehemu tu.

    ReplyDelete
  12. duh,poleni sana,serikali ipo busy na kampeni,mda wa kuwalinda raia haupo.jaribu kuongea na watoto wa vijiweni unaweza kuvipata,Tanzania amani hakuna kabisa,mungu aturehemu tu.

    ReplyDelete
  13. HUWEZI KUHUKUMU KWA KUWA MASKINI!!!?? WEE UNAONEKANA UNA DHARAU SANA. JUST BECAUSE MUNGU AMEKUJALIA KWA KUWA NA KIJIUWEZO!? KWANZA TAMBUA ONLY GOD CAN JUDGE! wee huna uwezo wa kumhukumu mtu, na kumwita mtu MASKINI!!! jifunze vizuri tafsiri ya maskini kabla ya kutumia.
    pamoja na kuwa umechukuliwa vitu, polite approach ingesaidia. kuliko kashfa hizo ulizotumia. hata ningekuwa mimi nimeiba nisingerudisha. maana unajidai sana wewe. Wabongo bwana! kiji uwezo kidogo tu basi madharau kibao!

    ReplyDelete
  14. Kama alivosema mdau hapo juu tangaza dau nono vijiwe vya hapo karibu utapata vitu vyako mi niliibiwa hivyo laptop mbili,documents na vingine kadhaa na nikavipata kwa kotoa elfu hamsini tu sidhani tumefika wadokozi kusoma michuziblog.

    ReplyDelete
  15. Halafu CCM wanazunguza kuuliza wananchi "Tuna amani hatuna?" na wananchi wanajibu "tunayo!!!!" Haya ni masikitiko makubwa ndugu zangu, ukweli ni kwamba hatuwezi tukawa kwenye amani kama idadi kubwa na wanachi wamegubikwa na umaskini mkubwa!!!!! Michuzi najua unabana sana maoni kama haya yanayofichua chanzo cha matatizo....ukweli wa mambo hapa ni kwamba CCM tuwamwage tu, ili tusonge mbele na kujenga nchi yetu na hatimaye kupata amani ya kweli. Michuzi bana tu, lakini ujumbe unakufikia na lazima ujue kuwa unaangamiza nchi yako, kwa kuendelea kufagilia CCM na serikali yake kwa maslahi yako binafsi!! Mimi sina shida hata kidogo, na ningekuwa ni mbinafsi kama wewe, basi ningekuwa sina sababu yeyote ya kuipinga CCM, kwani kuwepo kwao madarakani au kutokuwepo mimi napeta tu. Tatizo ni ndugu zangu waTanzania waliowengi ambao wamegubikwa na umaskini mkubwa na CCM imeshidwa dhahiri kuondoa umaskini huo.
    Ni mimi Muungwana
    USA

    ReplyDelete
  16. BONGO BALAA MWEZI ULIOPITA NILIKUWA HUKO MZEE NIMEFUNGA VIOO VIBAKA WALICHUKUA SIGHT MIRRORS ZOTE KAMA KUPANGUSA SIKUAMINI UTADHANI WAMESOMEA.

    ReplyDelete
  17. Pole sana unaweza kufanikiwa kwa njia hii, ila kejeli kwamba dhiki zisumbua zinaweza kutafsiriwa vengine na hawa vibaka, kuna vibaka ni High tech na wala hawana dhiki ivo, rekebisha usemi ili mlengwa/walengwa wakuonee huruma, kwa kusema ni dhiki kibaka atakuona ni arrogant na una madharau.

    ReplyDelete
  18. Jamani kabla hujatuma maoni tufikiri kwanza, wewe Anony Sun Oct 03,06:17:00pm. Internet haisomwi ila habari zinasomwa kwenye Internet. Jamani hata kiswahili kinatushinda? Ni hayo tu.

    ReplyDelete
  19. ACHA ZARAU WEWE UNANIITA NAZIKI THEN UNATAKA NIKURUDISHIE , LOL UNACHEKESHA .

    ReplyDelete
  20. HALAFU BADO MNA WACHAGUA VIONGOZI BOMU , UKIONA VITENDO KAMA HIVI HINA MAANA HALI NGUMU SANA! ALAFU WEWE MTOA TANGAZO HINAONEKANA JAMAA WAMEAMUA TU KUKU KOMESHA KWANI UNAONEKANA WEWE NI MTU WA ZARAU SANA UTAWAHITAJI BINADAMU WENZAKO WANA ZIKI WEWE UNA NINI SASA ? KAMA WEWE UMEVIMBIWA BASI TULIA WENYE ZIKI WALE


    MDAU FROM PARIS
    AKUNA VIBAKA WENYE ZIKI UKU !!

    ReplyDelete
  21. lazima kujifunza kutokuweka vitu garini vitapoonekana, ni kuacha gari kama vile hakuna kitu hata ukificha chini ya kiti angalia isionekane na hii tunafanya miaka mingi sio hapo tu dar hata ulaya ni hivyo watu wanafanya.

    pia ukijua unaenda sehemu anza ficha kabla ujafika kupaki gati as wezi watakuwa lazima wanavizia kuona ukichelewa au kujionyesha unaweka vitu vizuri unalo.

    ila kama kuna wanaokaa maeneo hayo wauzaji walinzi kama wapo lazima anayejua kilichoendelea.

    ni kweli inaonekana unawajua nani kaiba, basi wafate waambie wakurudishie, au hii ni matatizo ya kifamilia au boy/girlfriend kufanyiziana, maana ni kama unaona umechaguliwa wewe kwa makusudi.

    ReplyDelete
  22. WENGI WANAWAJUWA WANAFANYIANA U MAFIA BONGO SIKU HIZI MTU ANAMPOTEZA MWENZAKE VIBAYA KIMAFIA NI DEAL ZAO ZIKIENDA VIBAYA AU WAKICHUKULIANA MADEMU BASI STORI TU HAPO JUU UTAONA NA WENGI WANAOKAA MITAA HIYO.

    JE KUNA MDAU ANANIUNGA MKONO? MAKIZINGA.

    ReplyDelete
  23. Pole sana , but I think vibaka hawasomi humu.tumia akili nyingine.

    ReplyDelete
  24. Hatuwezi kukuhukumu kwa kuwa maskini! - DUH HILO TUSI SASA....

    ReplyDelete
  25. Idle threat aka mkwara mbuzi hata ningekua mimi ndo mwizi nisingerudisha, my advise to you just go tanga mkatafute sangoma labda mtafanikiwa but your approach on this is unattainable!!

    ReplyDelete
  26. Pole sana ndugu kwa kuibiwa! huo uamuzi wako wa kutokwenda polisi mimi nauunga mkono, kwani utapoteza muda wako bure!! polisi wetu ni bomu! tena wanakula nao hao vibaka!! nakuombea tu upate vitu vyako muhimu!

    ReplyDelete
  27. Is this for real or is just an indirect message? Hao vibaka kweli wanasoma blog ya jamii siku hizi au ni vibaka wengine (Mafisaid) ...

    Kuita mtu ana dhiki sio vyema kabisa kwa vile hujui yaliyomsibu hyo mwizi. Niishi na vibaka wengi tu ambao ni watoto wa matajiri sana Tanzania. Hivi mafisadi wakichukua hela unadhania ni dhiki?

    usiie watuw anadhiki kwa vile kuiba sio dhiki..

    ReplyDelete
  28. TvzkicartoonOctober 04, 2010

    kutokana na sifa njema ulizomwagia, za udhiki na umasikini wake,
    akirudisha "FALA".

    ReplyDelete
  29. hahahaha!!! Jamaa ana mikwara duuh!!! hayo maneno tu baba hata kwenye Khanga yapo,Cha kukushauri hapa zama maskani ya karibu na tukio tangaza dau wana watakurudishia.Na upunguze ukali kwenye ishu kama hizi Simba mwenyewe na ukali wake wote bado watu wanamnywesha chai

    ReplyDelete
  30. oya mwana ngoja nikuhabarishe,unajua nini bro?sie juzi hatukuwa na mapene si ndo tukaona tulianzishe?kupita kitaa tu tukaona mkoko wako,sema nini bro una mazarau kwa sana tu,wewe na demu wako hapa kitaa mmekuwa watu wa ngendengwe kwa sana tukaona tutafte shavubhumo garini so tukalianzisha!sasa humu ndani tumelamba laputopu yako,vilongalonga vya kiukweli na hizi kadi zako pia kuna mapene sasa sie kama vp mwana tunakuletea kiuzushi hapo mjengoni haya mazagazaga kama kadi za benki,za kura na wanja wa bidada na mkoba wake sie tunajisevia kiuzushi mpango mzima ila usijaribu kuwaabia hawa mastono wa kova noma mwana japo samtaime tunashirikiana nao huku kitaa kwa sana ila umetuzalilisha hapa mtandaoni,lakini aliamudulilai hii lapatopu yako inatutoa kwani leo tumeweza kusafu mtandaoni,nasi tunatesa kama vp nikong`otee kilongalonga changu namba 0718 12 341
    AHSANTE BY KIBAKA MSOMI
    MBEZI BEACH.

    ReplyDelete
  31. ahahahaha mm nimefurahi ulivyoibiwa wajua kwanini?dharau imekuwa kubwa sana eti maskini unaijua tafsiri ya masikini wewe?yaani bora walivyokuibia dharau ikuishe

    ReplyDelete
  32. najua ume-post hapa ukijua kabisa si sehemu husika kutangaza hizi habari na pia approach uliyotumia hakuna kibaka yoyote duniani anayeweza kuthubutu kupiga simu wakati siku hizi simu zimesajiriwa

    kingine umeonesha dharau kwa kumwita kibaka kuwa ni masikini na pia ana dhiki, kumbuka kuwa hata gari yako uliyotaja ni ya kimasikini pia elewa kuwa nchi yetu ni masikini hivyo wananchi wake nao ni masikini pia kwa hiyo na ww ni masikini wa mali na roho maana kanisani ulitakiwa kwenda na vogue sio Suzuki Swift gari ya bei rahisi

    Ushauri:
    weka alarm kwenye gari yako, pia usipende kutembea na vitu kwenye gari ambavyo una matumizi navyo kwa wakati huo kama kitambulisho cha kupigia kura, cha ofisini n.k au kama vinabebeka tembea navyo sio unaweka kwenye gari matokeo yake ndio hayo, tafuta njia nyingine za kidiplomasia za kutafuta hivyo vitu na pia unapopiga picha kwenye simu uwe unazitoa na kuhifadhi kwenye CD au kuzisafisha kama ni muhimu sana, kuhusu uchaguzi pole kura yako haitakuwepo (hapo ndio issue kwa taifa)

    Ushauri mwingine: Muache dharau kwa watu hata kibaka nae ni mtu tena huyo ni bora zaidi ya fisadi

    ReplyDelete
  33. Aliyekuambia kuwa vibaka wa siku hizi ni maskini amekuongopea... Nenda Slipway, CocoBeach, Makabirini wakati wa Kuzika, Mlimani City, na hata Diamond Jubilee uone vibaka wanaokuja na Magari mazuri na wanapaki jirani na gari yako ndipo wanavunja vioo na kuiba. Tena kuna watoto wa Kiarabu na wahindi ambao kutokana na imani zetu kuwa ni matajiri na sio wezi, basi wakiegemea gari yako wapita njia wanajua yao, hivyo wanakuibia kirahisi sana...

    Pole kwa yaliyo kukuta, kawahi kufunga acount zako maana siku hizi watu wanahitaji kujua akaunti namba yako tu bila password...

    ReplyDelete
  34. Allo wewe KIBAKA MSOMI wa Mbezi Beach,

    Mbona namba yako ya simu haijatimia herufi zote? Au walikufundisha tu kusoma lakini sio kuhesabu?

    Kama kweli unayo nia ya kusaidia, basi uitimize hiyo nia ipasavyo, au sio?

    ReplyDelete
  35. aisee yani awa jamaa wana adi funguo malaya automatic wakibonya tu magari zaidi ya 1 yanaungua na wanabeba vitu kiulaini

    tanzania tuiombee tunakoelekea siko,na ivi shilingi inazidi kuzama

    ReplyDelete
  36. Mtoa mada ameleta kilio chake kwa wanalibeneke akiamini yamefika mmojawetu hivyo ajaribu kutoa maelekezo alichukua hatua gani hadi kupata vitu alivyoibiwa. tatizo ni kwamba, badala ya kutoa ushauri baadhi ya watu wanatoa maoni yanayoprovoke badala ya kumconfort mtoa mada. Ni bora kukaa kimya kuliko kufanya ambayo wengi wetu hufanya, kuandika hata kama ni utumbo. Au wengi wa waandikaji ni vijana wa skuli waliochoropoka kutoka maskulini buguruni kwa madenge, mburahati mianzini au tandale kwa mfuga mbwa? shiiiiiiiiiiit!

    ReplyDelete
  37. "Tunajua kwamba ni dhiki ndiyo inayokusumbua, na kwamba, unaona kwamba hiyo ndiyo njia sahihi kwako kujipatia chochote. Hatuwezi kukuhukumu kwa kuwa maskini!" nimechoka na hilo nimeona ni nunukuu kama ilivyo...hizi jeuri??????

    ReplyDelete
  38. Kwa mtindo huu uliokuja nao utaendelea kuibiwa kila siku, kwanza kashfa kuwaita wenzio maskini,na kutumia lugha ya kutisha..sema umeishiwa cha kusema ndo maana usema hutaki kwenda polisi. Jifunze kutumia lugha ya kistaarabu ili usaidiwe..acha ulimbukeni!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...