Hello Uncle Michuzi....
Habari za kwako na pole kwa shughuli. Natanguliza shukrani kwa juhudi zako kwenye hii blog. Inatusaidia sana Mungu akuzidishie.. Naomba ukipata muda uniwekee hii. Najua maswali ni mengi lakini labda kuna wadau wanaelewa zaidi. Tumegoogle lakini hatukufika popote na nilikopata tuliandika email lakini ni week sasa hatujajibiwa...
Kuna mama mmoja ana mtoto wake yupo college na anasomea uandishi wa habari. Lakini huyo mtoto anataka akimaliza masomo akafanye kazi nchi kama Somalia, Sudani etc. Sasa mama yake amemwambia atamlipia gharama zote akiamua kuchukua mwaka mmoja off aende kusihi kwanza Africa kwenye nchi yeyote ili apate uzoefu kuliko aje aende akiwa amemaliza shule akishindwa itakua amepoteza muda wake wote.
Kuna mama mmoja ana mtoto wake yupo college na anasomea uandishi wa habari. Lakini huyo mtoto anataka akimaliza masomo akafanye kazi nchi kama Somalia, Sudani etc. Sasa mama yake amemwambia atamlipia gharama zote akiamua kuchukua mwaka mmoja off aende kusihi kwanza Africa kwenye nchi yeyote ili apate uzoefu kuliko aje aende akiwa amemaliza shule akishindwa itakua amepoteza muda wake wote.
Bahati alivyooongea na chuo wamemwambia kama akienda na kufanya kazi au kuonyesha vitu alivyofanya akiwa huko basi watampa credits kwa huo mwaka. To make a story short mama yake alikua anataka kumpeleka South Africa ila kwa vile aanajua ninatoka Tanznaia na nilivyomweleza nchi yetu amekua na hamu sana. Nimemwambia asifurahi sana asubiri niulizie mambo haya kwanza...
A) Hivi Tanzania kuna freelance journalists/reporters siku hizi au bado lazima mtu aajiriwe ndio apeleke habari? Anasema sio lazima alipwe bali hata akipewa credentials tu inafaa kabisa. Mimi nikamwambia sijui kuwa kuna mashirika ya habari yanayoochukua habari nje ya wafanyakazi wao. Nimegoogle lakini sioni kama wanaelezea haya.
B) Naombeni majina na contact za magazeti, TV stations au radio zinazotoa huduma kwa nchi nzima (national tv stations, newspapers, radio stations) na kama kuna local stations, newspapers au hata TV stations zinazohudumia mikoani au kwenye miji. Hii ingemrahisishia kazi
C) Je kuna magazeti au jarida zozote yanayotolewa ya bure kweli nchini siku hizi. Yawe ya aina yeyote. Kama yapo naomba contact zake pia au radio na Tv station ambazo ni not for profit.
D) Na kama akitaka kuwasiliana kwa simu hivi kweli kuna toll free numbers kwenye mashirika yeyote Tanzania?
E) Na kama mwanae akiwa huko yeye anaweza kununua number ya simu ya Tanzania akakaa nayo huku na akiongea na mwanae charges ziwe kama wanawasiliana local? Au kwa wale wanaosafiri na simu mkifika nje ya nchi unaweza kutumia simu yako?
F) Hivi kuna digital printing services kama ya FedEx vile au ni mpaka viwandani mtu akitaka kuprint presentations au articles nyingi? Kama kuna mwenye number ya mahali popote pa kuprint iwe kiwanda cha kumprint magazeti au mahali popote wanapo print basi naomba number nimpatie.
Asante
Mdau Mdau
kama anakuja south africa List ya vitu vote vipo ispokuwa kadi ya simu ila zipo njia nyengine cheap za mawasiliano kama hatafanikiwa huko nitampa Data zote za ha na namba zote nipo cape town
ReplyDeleteTabu ya nchi yetu ni kupata VISA, tuko makini sana na haturuhusu kuingia ovyoovyo kwa vijisababu kama hicho cha freelance journalist. Namshauri ampeleke Msumbiji wao hawana noma kabisa.
ReplyDeleteIngia kwenye website ya Daraja, kisha andikia hao watu wa Daraja ni NGO ya masuala ya jamii na wana gazeti lao linaitwa Kwanza Jamii. huko kwa kuwa ni wazungu mtaelewana lugha. Hapa watakulostisha wabongo hawajui wala hawajozea mambo hayo ya kuvolunteer. Na wapo wengi tu vijana wanakuja GAP year kuvolunteer nimeishakutana nao wengi wanaenda Arusha na Moshi lakini hata huko Njombe patamfaa huyo kijana wenu, ni pazuri na salama, na asikudanganye mtu visa atapewa bila shida kama wenziwe wengi tu walioko huko vijijini wakijitolea!
ReplyDeletemaswali yako yote uliyouliza unaweza kupata majibu kwa dk 10 ktk internet, if you have a reasonable IQ!
ReplyDeleteHuyo mama Yupo wapi? kila kitu kitamalizwa na Skype.com is free unahitaji tu kuwa na computer yenye internet. Mwambie apige simu ubalozini aone kama watmpatia visa I natumaini ni pesa yako tu.
ReplyDeleteKaka, Tanzania imebadilika sana. Hivyo vitu vyote Tanzania vinapatikana isipokuwa sijui kama kuna gazeti la bure.Hata mh. Michuzi anaweza kukusaidia kabisa maana ndiyo fani yake na anajua kila kinachoendelea. Wewe mkamate uongee naye vizuri atakusaidia hasa kwa Tanzania.
ReplyDeleteUncle Michuzi asante asante sana kwa kupost hii hapa. Natumaini nitapata general ideas …Asante sana...I owe you one….
ReplyDeleteKwa anayesema kuhusu SA hata mimi nilikua nafikiri hivyo hivyo lakini nilijaribu kumshawishi ajaribu kwetu nikijua kama akienda kwetu hela takayoitumia kuishi huko itaingia katika uchumi wetu. Japo ni mmoja lakini kidogo kidogo hujaza kibaba na huwezi jua akipapenda kesho atawaambia watu wangapi nao waje waspend hela yao kwenye uchumi wetu? Ndio maana nilimwambia huko SA the cost of living ni nyingi kuliko kwetu…
Kuhusu visa sidhani kuwa hiyo ni tatizo kabisa.
Na wewe mwenye harsh comment hapo juu spare you comment for some other juicy good stuff. I really don’t have time for that now. Hunijui sikujui lets leave like that...If my IQ is less than you think good for you. I am not here to judge people and as they always say ukipigana/kujibishana na kichaa/mjinga na wewe utaonekana ni mjinga/kichaa.
@ 12:02 AM kama vinapatikana nawezaje kupata contact number? Hicho ndio nacho hitaji sana. Hata majina na contact kama zipo kama hamna nitagoogle zaidi. Nilijaribu kusearch wizara mabalimabali lakini hamna maelezo mengi kabisa.
Thanks again for those who took their time to post some useful information
Kiswahili chako kizuri sana na unaonekana ni Mtanzania unayeuliza hayo maswali lakini unaonekana kutoijua Tanzania at all! Please visit our local websites... ukigoogle kila kitu kipo majibu wazi kabisa, everythingindar.com...
ReplyDelete