================
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza kukamilisha mipango yote ya kuipeleka timu ya taifa ya Pool katika mashindano ya dunia yatakayofanyika katika jiji la Paris, nchini Ufaransa mwezi Novemba.
Akitangaza kukamilika kwa maandalizi ya safari hiyo muhimu kwa timu yetu ya Taifa ya Pool, meneja wa Bia ya Safari Lager, Fimbo Butallah alisema; “timu yetu ya Taifa imekuwa ikionesha mafanikio makubwa na kupanda kwa kiwango cha mchezo mwaka hadi mwaka. Nafasi hii ya kushiriki mashindano ya Dunia imetokana na matokeo mazuri ambayo timu yetu ilionesha katika mashindano ya Afrika yaliyofanyika mwaka jana nchini Afrika ya Kusini na kuibuka namba tano, hivyo kupata nafasi ya kuwa moja ya nchi zitakazowakilisha bara la Afrika katika mashindano hayo makubwa”
Bia ya Safari Lager inaungana na watanzania wote katika kufurahia matokeo na mafanikio haya mazuri ya timu yetu ya Taifa, na hii ndio sababu kubwa iliyopelekea tuhakikishe kuwa safari hii ya kwenda Paris inafanikiwa. Pia tunaahidi kuendelea kuudhamini mchezo huu wa Pool na kuuendeleza ili tutimize ahadi zetu, ambazo ni kuufanya mchezo huu kuwa ajira ya kutegemewa kwa vijana na pia kulitangaza Taifa letu kote ulimwenguni kupitia ushiriki wa mashindano kama haya ya kimataifa.
Nachukua nafasi hii pia kuipongeza kampuni ya Integrated Communication kwa ufanisi mkubwa wanaouonesha katika kuendesha mashindano yetu ya mchezo wa Pool, kampuni hii imetusaidia sana sisi wadhamini na chama cha pool kuhakikisha tunafikia malengo yetu.
Akizungumzia Safari hiyo, Katibu wa Chama cha Pool Taifa Amos Kafwinga alisema “timu itaondoka tarehe 6 Novemba na kuwasili Paris tarehe 7, itaelekea katika mji wa LIMOGES, ambako mashindano hayo yatafanyika na timu inategemea kurudi tarehe 15. Mashindano haya yanashirikisha jumla ya nchi 32 toka katika mabara matano, na bara la Afrika linawakilishwa na timu tano ikiwemo Tanzania.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa Isaac Togocho alitoa shukrani nyingi kwa Safari Lager kwa jinsi wanavyoendeleza mchezo huu wa Pool hapa nchini, hususani kufanikisha safari hii muhimu zaidi kwa timu yetu na Taifa kwa ujumla, pia alisisitiza suala zima la nidhamu kwa vijana na ujumbe wote unaoelekea Ufaransa ili kulitangaza jina la nchi yetu vizuri na kuleta sifa hapa nyumbani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...