UMOJA WA WANAFUNZI WA KITANZANIA
HYDERABAD-INDIA (TSAH)

Tunapenda kuwataarifu wanafunzi wote wa Kitanzania, wanaosoma katika vyuo vikuu na taasisi mbalimbali za kitaaluma hapa Hyderabad India, kuwa kutakuwa na uchaguzi mkuu wa viongozi wa Umoja kwa mujibu wa katiba yetu.

Wale wote wenye sifa za kuongoza jumuiya yetu, mnakaribishwa kuchukua fomu kwa wajumbe wa tume waliotajwa hapo chini.

Ratiba kamili ya zoezi zima ni kama ifuatavyo.

1. Kuchukua fomu na kuzijaza 5/09/2010 mwisho wa kurudisha ni 24/10/2010
2. Kukutana na Kamati ya uchaguzi ili kukubaliana kanuni za uchaguzi 24/10/2010
3. Kampeni na maandalizi tarehe 25/10/2010 hadi 31/10/2010
4. Tarehe ya uchaguzi ni 31/10/2010 eneo la Sainikpuri-Ukumbi mtajulishwa baadaye.


Wajumbe

Tabagi A: wenyekiti +918897943864 Tolichowki

Majinge, D, Mjumbe +919966954555 Sainikpuri

Simbo, Mjumbe +919948460883 Sainikpuri

Lipina, Mjumbe +919885186905 Singapore city

Kulwa, K. Mjumbe +919618477357 Alwal

Makwinya, J: Katibu +919618477428 Tolichowki

Imetolewa na Tabagi, Abel
Mwenyekiti wa kamati maalum ya uchaguzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. kura yngu itaenda kwa yle atakaetetea maslahi ya w'funzi wa nizam college tunaoteseka na telangana maana viongozi mnakaa kimya tu

    ReplyDelete
  2. Sasa huu hujumbe una wahusu nini wengine . kwani ungewatumia kwenye simu zao si ingetosha . vitu vingine bana. dah

    ReplyDelete
  3. wewe mtowa maoni wa pili na wewe imekuhusu nini kwali hii blog yako? kama hupendi awekayo michuzi nawe fanya blog yako halafu uweke utakacho, hujalazimishwa kufungua blog hii kabisa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...