Bwana Michuzi, assalaam aleykum.

Naomba unirushie ujumbe wangu huu, hasa kwa wanahabari wetu. Nimewasikia mara kadhaa wakisema kuwa serikali hii ya Rais Kikwete ni Awamu ya Tano! Nani kawaambia? Ninachofahamu mimi ni kuwa hii bado ni serikali ya awamu ya nne, au kuwa sahihi zaidi, hiki ni kipindi cha pili cha Serikali ya Awamu ya NNe.


Wasitupotoshe kwa kuwa wao wanaaminiwa na jamii sasa inapotokezea wanazungumza jambo kimakosa na wanafanya hivyo kupitia runinga, inakuwa mtihani zaidi.

HII NI AWAMU YA NNE
MDAU MAKINI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. ASAVALI BANA MDAU TALUMA YA HABARI HATA MIMI NAONA INAKWEDA KUSHOTO AMA IMEINGILIWA KUTOKANA NA HALI YA MAISHA SIKU HIZI ATA WEWE UKITAKA KUWA MWANAHABARI WA TANZANIA BILA KUFAUTA VIEGEZO VYA TALUMA YENYEWE INWEZEKANA.KUNA MWANDISHI ALIANDIKA HISTORIA YA MARIJANI RAJABU,YEYE AKAMWITA MARIJANI SHABANI,SIOJINA TU NENDA KATIKA HISTORIA YENYEWE UNAJIULIZA KAIPATA WAPI?WANASHINDWA ATA KWENDA MAELEZO WAKAPEWA HABARI SAHIHI ALAFU WAKAITOA.ALAFU KUNA WANDISHI WA UDAKU HAO NDIO CHICHEMI.

    ReplyDelete
  2. Awamu ya saba.

    ReplyDelete
  3. Achilia mbali kutokujua mambo, jamani kiswahili kinavyomomonyolewa siku hizi sijui watu wengine wamesoma shule gani! au ndiyo matunda ya 'english medium schools'. Maana utakuta mtu anakuambia ni mwandishi wa habari, anasema ''katika kipindi hiki tulichokuwepo'' badala ya ''katika kipindi hiki tulichopo'' Mwingene utamkuta anakuandikia 'ata' badala ya 'hata'. Sijui tatizo ni lugha za asili. Waandishi kama huna uhakika na unachotaka kuandika au kusema uliza uelishwe.

    ReplyDelete
  4. hata habari nazo mna-chakachua! hii kali wadau waandishi wa habari.
    mdau.

    ReplyDelete
  5. Sawa, ninakubaliana na mawazo yenu. Tatizo jingine ni kutokuwa na muda wa kuyachambua makosa kabla ya kurusha habari.

    Kwa mfano wewe mtoa mawazo wa pili kwani wewe una maana gan na kuandika ''uelishwe'' ni rahisi kulalamika bila kuangalia ni kitu gani kina sababisha makosa kama hayo.
    Ahsanteni sana!

    ReplyDelete
  6. Hii kali: "...katika kipindi hiki tulichokuwepo'' badala ya ''katika kipindi hiki tulichopo..."

    Je, labda wanatafsiri kutoka katika mukadha wa Kiingereza:

    Kwa mfano: This past week...

    Juma hili lililopita/Wiki hii iliyopita...

    Au ni:

    Juma lililopita/Wiki iliyopita...

    ReplyDelete
  7. Mdau wa kwanza umeona mbali sana , basi usiombe hawa wanahabari wetu akaisoma habari ya nje ya nchi iliyoandikwa kwa kiingereza halafu akaiandika kwenye magazeti yao utaona mtu anaandika mfano mchezaji wa Villareal wa spain wakati hiyo ni jina la timu mojawapo nchini spain au anaandika timu ya Galatasary ya Ugiriki wakati hiyo ni timu ya Uturuki. au akaandika Mchezaji Karem Benzema wa Barcelona wakati huyo ni mchezaji wa Real Madrid. ilimradi wao kazi zao ni bora liende . wakati hawajui kuwa wanapotosha watu na ukitaka kuhakikisha wadau jaribuni kusoma gazeti la Habari leo au Majira kila siku mtatoa makosa. wanahabari njaa zitawaua kwa kuingilia kazi za watu.
    mdau Paka la jikoni UK.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...