Bondia kutoka Makambako wilaya ya Njombe mkoani Iringa mwakilishi wa Tanzania Chupack Chipindu akionyesha juu makanda wake mara baada ya kumwadhibu vikali bondia kutoka Kenya Josephat Odihambo. Chupaki amemwadhibu bondia huyo katika pambano lisilo na ubingwa lililomalizika hivi punde katika uwanja wa Samora katika tamasha la Mtikisiko 2010 na Redio Ebony Fm
Mashabiki wakimpongeza Chipindu baada ya kushinda pambano

Mpambano ukiendelea
Josephat Odhiambo toka Kenya akijiuliza nini kimempiga

Gemu lilikuwa kali toka mwanzo. Picha zote na Francis Godwin





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Michuzi namna gani sasa? bondia wa iringa amshinda bondia wa kenya? kwani iringa ni nchi gani? kuwa muangalifu bwana unavunja hadhi ya uandishi wa habari.

    ReplyDelete
  2. hivi kweli huyo bondia wa kenya alifaa kwa pambano hilo! mbona naona kama hana lishe ya kutosha! au macho yangu!!

    ReplyDelete
  3. YANI NYIE MAPROTA MTAUWA SIKU MMOJA KWA KUKURUPUKA ILI MRADI MPATE GAT COLLECTION YENU YANI HUYU ODHIAMBO CHANG'AA UBONDIA KANZA LINI,PAMBANO HILI LA UZITO GANI NA MKANDA GANI.

    ReplyDelete
  4. Hahaha kweli Iringa nchi au Mkoa? Bondia wa Tanzania kutoka Mkoa wa Iringa amtwanga Bondia wa Kenya. Huyo mbona Kama Kibabu yani Mzee huyo wa Kenya au ndio anatafuta pesa kwa nguvu?. Hongera Bondia wetu wa Tanzania. MZ

    ReplyDelete
  5. Hebu angalia hapo juu jinsi alvyokaa,yaani mbendembende,ana shepu ya mgema, si bondia.

    ReplyDelete
  6. mtakuja kuua watu buree. Huyu Bondia wa Kenya mzee na afya yake ina mgogoro yaani hafai kupigana.

    ReplyDelete
  7. Duh! yaani nimetoka kubeba box niko hoi na stress kibao za utility bills halafu nikaiingia blogu ya ankal na kumkuta bondia wa kenya alivyokaa nimecheka yaani now stress level very low. yaani we acha tu.

    ReplyDelete
  8. Chpack oyee!!!!! Lakini Francis na Ankal msingelitoa hiyo picha ya nne kwa kuwa nahisi itawadhalilisha watoto [na wajukuu?] wa mzee Odhiambo. I hope Mzee Odhiambo atapewa hela za kutosha ili asiendelee kunyanyaswa na maboxer vijana.

    ReplyDelete
  9. Jamani hao waandaaji watakuja kuua! Ankal eh, chondechonde waambie hao jamaa kuwa huyo Odhiambo alishawahi kupigana ndondi kweli jamani. Bondia gani unapigwa halafu unatoka machozi? Mi naungana na mdau hapo juu kuwa huyo Odhiambo anaonekana kama mgema vile. Samahani kama nitakuwa nimekosea ankle lakini hili suala ni serious. Na huyu jamaa wa Iringa asiwe na kichwa kikubwa kwani hakupigana na bondia bali mgema wa Lamu anayejiita Odhiambo.
    Nawakilisha

    ReplyDelete
  10. Huyu Odhiambo utafikiri kibaka aliyepokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira na kuponea chuchupu kuchomwa moto, na sasa anavuta pumzi baada ya kuokolewa na wajomba....hahahaaaa!

    ReplyDelete
  11. Ni wazi kuwa mtoa habari hajui anachofanya. Kwanza kama ni mchezo wa ndondi ni lazima kuelimisha watu ni uzito gani. Je ilikuwa mashindano ya kimataifa au kwa kuwa mmoja wa "mwanandondi" anatoka Kenya basi unakuwa mpambano wa kimataifa? Habari zinafaa kuhakikiwa vinginevyo ni upotofu wa uma.

    ReplyDelete
  12. DUH !! MBONA HAWA MABONDIA WAMECHOKA HIVYO????

    MDAU PARIS

    ReplyDelete
  13. Na uhakika Odhiambo ni agemate wa Mwai Kibaki, Njja mbaya mweee, lilifanyika ukumbi gani hilo pambano na alipigwa raundi ya ngapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...