Mh. Mizengo Kayanda Pinda "Mtoto wa Mkulima"

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE AMEMTEUA MH. MIZENGO KAYANDA PINDA, MBUNGE WA JIMBO LA KATAVI, KUWA WAZIRI MKUU, KWA MUJIBU WA TANGAZO LILILOSOMWA BUNGENI SASA HIVI NA SPIKA WA BUNGE MH. ANNE MAKINDA.

ZOEZI LINALOFUATA SASA NI WABUNGE KUMTHIBITISHA WAZIRI MKUUAMBAPO MWANASHERIA MKUU MH. FREDERICK WEREMA ANATOA HOJA YA KUWAOMBA WAHESHIMIWA WABUNGE WAMTHIBITISHE AMBAPO ITAPIGWA KURA YA PAPO KWA PAPO NA BAADAYE UTAFUATIA UCHAGUZI WA NAIBU SPIKA AMBAYE ATAJULIKANA LEO PIA.

WAZIRI MKUU ANATARAJIWA KUAPISHWA KESHO IKULU NDOGO YA CHAMWINO, IKIWA NI HATUA YA KWANZA KABLA YA KUTANGAZWA KWA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI. HATUA HII INAKAMILIKA BAADA YA RAIS KUKAA NA KUSHAURIANA NA MAKAMU WA RAIS NA WAZIRI MKUU.

BARAZA HILO JIPYA LINATARAJIWA KUTANGAZWA IJUMAA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. kwahiyo sasa ataachia ubunge ama ndio atakuwa na vyeo viwili kwa wakati mmoja?

    ReplyDelete
  2. Hatukutegemea mabadiliko yeyote hata hivyo. Hatutegemei mabadiliko yeyote pia katika baraza la mawaziri, labda kuziba mapengo yaliyoachwa na akina Masha. Chonde chonde JK, Safari hii jikakamue na kuwatupilia mbali wateuliwa wasio na uwezo, au wenye kutetea tu maslahi yao badala ya maslahi ya nchi! Vinginevyo, hilo CCM litakufia hilo 2015!

    ReplyDelete
  3. Kwa anon wa kwanza: KULINGANA NA KATIBA YA TANZANIA, Waziri mkuu lazima awe mbunge.

    51.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
    atakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii na
    ambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais
    kwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa
    na Bunge.
    (2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku
    kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua
    Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi
    anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi
    Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge
    wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio
    wengi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika
    madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa
    na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge
    walio wengi.
    (3) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, Waziri
    Mkuu atashika kiti cha Waziri Mkuu hadi-
    (a) siku ambapo Rais mteule ataapa kushika kiti chake;
    au
    (b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka; au
    (c) siku atakapojiuzulu; au
    (d) siku Rais atakapomteua Mbunge mwingine kuwa
    Waziri Mkuu; au
    (e) atakapoacha kushika kiti cha Waziri Mkuu kwa mujibu
    wa masharti mengineyo ya Katiba hii. (IIFUNGU NAMBA 51 KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KAMA ILIVYOREKEBISHWA 2008 =AS AMEENDED IN 2008)


    Mdau

    ReplyDelete
  4. Jk mpe MREMA MAMBO YA NDANI

    ReplyDelete
  5. Wewe mtoa maoni wa kwanza hujui kama lazima awe mbunge ili kuwa waziri mkuu? watoto kama nyie zamani mlikuwa mnaitwa manunda hamjui a wala be...vile vile huitwa mbumbumbu..

    ReplyDelete
  6. Wewe ulieniita mbumbumbu mbona sio kweli. Mimi nilikuwa bright sana enzi zangu wakati nikisoma mpaka nilivyomaliza elo-wai nilikuwa nachukua namba moja mpaka tatu darasani. Swali langu hamjalielewa, ngoja niwafafanulie kidogo, namaanisha Je kuanzia sasa hivi huyo Pinda ataendelea kuwa waziri mkuu and at the same time kuendelea kuwa mbunge ama itabidi aachie kofia ya ubunge kwavile ameteuliwa kuwa w.mkuu? bado hakuna alienijibu,ingawa anon mmoja amejaribu kuniwekea vifungu vya katiba nimevielewa ila havijajibu swali langu. Nisaidieni tafadhali kwa wanaofahamu jibu sahihi. Mdau mwenye mbongo, UK

    ReplyDelete
  7. Mh SAMAHANI HIVI KIGUMU NI KIPI?

    UWAZIR MKUU NA UBUNGE NI KAMA MWILI NA ROHO. KIKIONDOKA KIMOJA KINGINE HAKIFANYI KAZI.

    Inamaana Pinda akiachia Ubunge, hawezi kuwa waziri mkuu ndio ufafanuzi wa kipengele hicho hapo n.51

    Need I say more

    ReplyDelete
  8. Kwa kumsaidia mdau aliyeuliza kuhusu Waziri mkuu. jibu ni kuwa ataendelea kuwa mbunge wa jimbo lake kama mawaziri wengine watakavyokuwa wabunge wa majimbo yao.na atawakilisha jimbo lake bungeni kama wengine .
    mdau aliyefeli Elowai.

    ReplyDelete
  9. Mdau wa kwanza mwenye bongolala uliye UK-Ukara Ukerewe ... kwa kifupi ataendelea kuwa mbunge na waziri mkuu. Hawezi kuacha Ubunge. Kumbuka waziri mkuu lazima awe mbunge kwanza hawezi kuacha ubunge. Nafikiri nimejibu swali lako.

    Mdau Tandika sokoni

    ReplyDelete
  10. Nashukuru kwa majibu yenu na sasa nimeelewa. Swali langu jipya ni je inawezekana vipi muheshimiwa ashikilie viti viwili at the same time, jukumu la ubunge pekee ni zito na sasa ukiongezea na u'mkuu si itakuwa jukumu zito zaidi? Nimestaajabishwa sana kusikia kumbe mawaziri nao wana vyeo viwili vya uwaziri na ubunge at the same time? sikuwa najua hili, ARE YOU KIDDING ME!!!! inakuwaje mtu mmoja ashikilie vyeo muhimu namna hii vyenye majukumu na kuhitaji muda kuvitumikia? Kwanini sheria isizuie hili? Juu ya w'mkuu, kama sheria inasema lazima awe mbunge ni sawa lakini naona akishachaguliwa basi avue kofia hiyo ya ubunge ili aweze kuhudumia vyema nafasi ya u'mkuu. Na ingekuwa vyema zaidi hao wabunge wawe wakiishi majimboni mwao na sio Dar. sasa hao mawaziri-wabunge je wanaishi majimboni mwao ama Dar? Ndugu naomba mnifafanulie zaidi hili maana leo nimejifunza mambo niliyokuwa siyajui kabla. Ni hayo tu. Does my theory make any sense to anybody at all? -Mdau mbongo, UK

    ReplyDelete
  11. Wee Mkerewe, unajua gharama ya kuandaa uchanguzi wa mbunge mmoja pindi waziri mkuu akiachia Ubunge? Jibu ni gharama kubwa sana. Gharama yake ni kubwa kuliko gharama ya kuvitumikia vyeo vyote hivyo viwili kwa wakati mmoja. Yaani Uwaziri mkubwa na Ubunge. Over.

    Mdau,
    Kibanda Maiti.

    ReplyDelete
  12. Inasikitisha kuona jamii bado inaupeo finyu juu ya katiba ya taifa lao ila taratibu tutafika Inshaalah. Hivi ww uliyesema "UWAZIRI MKUU NA UBUNGE NI KAMA MWILI NA ROHO. KIKIONDOKA KIMOJA KINGINE HAKIFANYI KAZI". Hiyo theory yako ni mbovu mno maana unaweza ukaachia UWAZIRI MKUU na bado ukawa Mbunge, mfano mzuri yaliyo mkuta Lowassa baada ya kuacha UWAZIRI MKUU aliendelea kuwa Mbunge kama kawaida.
    Kuhusu mdau anaye uliza Waziri Mkuu baada ya kuchaguliwa kwanini bado awe na nyadhifa mbili Uwaziri na Ubunge??? bila shaka wasiwasi wako utakuwa katika swala zima la utendaji. kibinaadam huo ni ukweli ila katiba inasema hivyo, njia pekee ya kubadili hayo ni marekebisho katika katiba.

    ReplyDelete
  13. Mdau Tue Nov 16, 11:56:00 PM huko Ukerewe nafikri una point. Sioni umuhimu wa waziri yoyote kuwa mbunge vile vile. Kama ni waziri atawahudumia wananchi jimboni kwake saa ngapi? Pia si ataweza kutumia uwaziri wake kuwanufaisha jimbo lake zaidi?

    Ingekuwa poa sana kama mtu asingeweza kuwa waziri kama tayari ni mbunge. Hapo ndio tungeona wale wenye uroho na madaraka kama wengegombea ubunge. Yaani hapo ndio tungekuwa na wabunge asilia.

    ReplyDelete
  14. He, sawa ndo hayo ya Philosopher Plato kuwasha tochi mchana katikati ya mji na watu wakaanza kumkimbia na wengine kumcheka kwamba kadata. Ukweli ni kwamba tunatakiwa kuwa makini sana na pia kilichopo ktk katiba kinaweza kubadilishwa kulingana na mazingira.Swali kuogopa gharama za kutenganisha hivyo viti viwili ni msingi wa maana kweli? Je hatujawahi kuwahi kuwaza kwamba hiyo ni technic kubwa ya CCM kuwa na potential figures against wapinzani. haya kazi bado ipo wandugu.

    ReplyDelete
  15. Anon wa 14:00hr unayependekeza Mrema kupewa wadhifa wa wizara ya mambo ya ndani huijui katiba ya jamhuri ya muungano na unamjua mrema wa mwanzoni mwa miaka ya 1990. Mrema wa sasa amechoka kwa mzee na ugonjwa, usilete ukabila kwenye ishu nyeti kama uteuzi wa baraza la mawaziri. Kiswahili chako kinaonesha wewe unatoka north, kweli si kweli?

    Baba Ochu, Jang'ombe kwa maharuki.

    ReplyDelete
  16. Ndugu ningependa kumaliza mada hii kwa kuuliza swali moja zaidi, Je hao mawaziri-wabunge hulipwa mshahara mmoja ama miwili? Maana kama wana nyadhifa mbili ina maana wanalipwa kwa kila nyadhifa waliyonayo? Watanzania tunachekesha sana. -Mbongo, UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...