Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya usafirishaji wa vifurushi Duniani ya DHL hapa nchini Bw. Blaise DeSouza (kushoto) akiwa amembeba mtoto Sara James wa kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha SOS cha Jijini wakati akikabidhi mmoja ya vyandarua vilivyotolewa na kampuni yake kwa kituo hicho, anayepokea ni Mkurugenzi Mkuu wa SOS hapa nchini Bi.Rita Kahurananga hafla hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika Ofisi za SOS Kinondoni Jijini Dare s Salaam, katikati ni Bw. Shreekesh Karia, Meneja wa DHL hapa nchini.


DHL, Kampuni inayoongoza kwa usafirishaji wa vifurushi nchini na duniani kote imetoa vyandarua 1500 vilivyotiwa dawa vyenye thamani ya shilingi milioni12 kwa lengo kupambana na ugonjwa huo hapa nchini.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa DHL Ukanda wa Afrika na Asia Kusini ya Pasifiki , Bw. Amadou Diallo,alisema msaada huo ni sehemu ya uwajibikaji wa kampuni yake kwa jamii katika maeneo ambayo DHL inatoa huduma na kwamba msaada huo una lenga kujenga jamii yenye afya bora.

Kwa sasa hapa nchini kuna kampeni mbalimbali za kupambana na ugonjwa huo ikiwamo ile ya Malaria Haikubaliki ambayo ilizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete mapema mwaka huu.

“Mbali na athari zake kwa jamii, gharama za kuutibu ugonjwa huo ni mzigo kwa taifa kwa kuwa unarudisha nyuma maendeleo pia unashusha uzalishaji mali, ugonjwa wa Malaria unasababisha vifo kwa asilimia 30 kati ya magonjwa yote.” alifafanua.

Kupambana na Malaria kutaiwezesha nchi yetu kuwa sehemu salama ya makuzi kwa watoto wetu”,alisema Rita Kahurananga, Mkurugenzi wa Taifa wa Taasisi ya SOS Children’s VillageTanzania.

Kati ya hivyo, vyandarua 1000 vimekwenda kwa taasisi ya kimataifa ya kulea watoto ya SOS wakati vyandarua 500 vitakwenda kwa vyama visivyo vya kiserikali (NGO) ambayo vinahitahi vyandarua hivyo.

Alisema kwa kuwa eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara ndilo kitovu cha mapambano dhidi ya Malaria Duniani huku likiwa na asilimia 90 ya vifo vinavyotokea katika bara la Afrika kutokana na malaria, ndiyo maana kampuni yake imeamua kujiunga katika vita hiyo dhidi ya Malaria.

Bw. Diallo alisema kwa mujibu wa takwimu za Mpango wa Taifa ya Kupambana na Malaria, watu milioni 16 mpaka 18 huugua malaria kila mwaka wakati vifo vikiwa ni wastani wa watu 100,000 kwa Tanzania na kuongeza kuwa aslimia 93 ya Watanzania wako katika hatari ya kuugua ugonjwa huo.

Alisema malaria husababisha kifo cha mtoto mmoja kati ya watano wenye umri wa chini ya miaka mitano pamoja na kuwaathiri wanawake wajawazito.

Naye Bw. Shreekesh Karia, Meneja wa DHL kwa Tanzania, alisema DHL inatambua umuhimu wa kupambana na ugonjwa huo hapa nchini na ndiyo maana imejitokeza kupambana nao ili kupunguza idadi ya vifo.

“Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) vyandarua vilivyotiwa dawa, ndiyo njia sahihi ya kupambana na ugonjwa huo kwa kuwa vimeonyesha uwezo wa kupunguza malaria kwa asilimia hamsini,” alisema.

Mbali na shughuli nyingine, Taasisi ya SOS Children’s Village inasaidia watoto 1500 nchini ya mpango wake wa kusaidia watoto katika jamii (FSP), kupitia mpango huo taasisi hiyo imepanga kuwafikia watoto wengi wanaoishi kwenye mazingira magumu na kuisaidia jamii kuwatunza watoto wanaoishi katika mazingira hayo tarishi.

Alifafanua kuwa asilimia 95 ya vyandarua vilivyotolewa na DHL vitasaidia kuutekeleza mpango wa FSP kwa kuwafikia watoto 1500 wenye mahitaji ya vyandarua katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hivi jamani naomba kuuliza africa ndo tunaumwa maralia peke yetu sioni mabara mengine yanapewa misaada. mimi nakasirika sana kwa nini watu wasipewe semina jinsi ya kuindoa maralia eti jikinge na maralia sielewi. wanatwambia hivyo harafu wanatengeneza dawa feki. sasa tufumbuke macho kama watu wanaweza kupewa semina za HIV na maralia je?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...