Katibu Mkuu wa CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akimpongeza Rais Mteule wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein, Baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC kumtangaza rasmi kuwa Mshindi wa Urais wa Zanzibar katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010-2015, hafla hiyo ilifanyika jana usiku katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani.
Katibu Mkuu wa CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa na Rais Mteule wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein, wakifurahi pamoja na Mama Mwanamema Shein na Mzee Hassan Nassoro Moyo baada ya matokeo jana usiku. Wote wameafiki kuunda Zanzibar mpya ya upendo na amani.
Wananchi, Wanachama na Wapenzi wa Vyama vya CCM na CUF wakiwa katika harakati za kusherehekea Ushindi wa Chama cha Mapinduzi CCM katika mitaa mbalimbali ya mji wa Zanzibar kufuatia kupata Ushindi wa CCM katika kinyang’anyiro hicho cha kihistoria cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010
Wananchi, Wanachama na Wapenzi wa Vyama
vya CCM na CUF wakiserebuka pamoja
Wananchi, Wanachama na Wapenzi wa Vyama vya CCM na CUF wakiwa katika harakati za kusherehekea Ushindi wa Chama cha Mapinduzi CCM katika mitaa mbalimbali ya mji wa Zanzibar kufuatia kupata Ushindi katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010
Wananchi, Wanachama na Wapenzi wa Vyama vya CCM na CUF pamoja. Uwanja wa Amaan Stadium unatarajiwa kufurika kesho wakati wa kuapishwa kwa Rais mteule Dk. Ali Mohamed Shein. Picha na Amour Nassor


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hii ndio Zanzibar tunayoitaka,Speech zilikua ni za kusisimua sana,Na wakati huu tumepata viongozi kutoka Pemba ni uwiano mzuri nahistoria ya kusisimua kabisa ambayo si rahisi kufutika kwa sasa.
    Hata hivyo Maalim Seif ni Baba wa Taifa la Zanzibar,Misuko suko aliyoipata katika historia yake na hapa alipofika anastahili zaidi ya urais.Mungu ibariki ZANZIBAR TANZANIA NA AFRIKA KWA UJUMLA.

    ReplyDelete
  2. Hali hii ya maelewano inapendeza sana na kutia moyo. Panapo maelewano na maridhiano huwepo pia baraka na maendeleo kwa sababu hakuna chuki na wote lenu moja. Kwa Zanzibar huo ni mfano wa kuigwa na ni jukumu letu sote tuilinde na kuiendeleza hali hii ya maelewano kwa maslahi ya Zanzibar na wananchi wake na pia kwa maslahi ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania.

    ReplyDelete
  3. MUNGU IBARIKI ZANZIBAR,TANZANIA NA AFRIKA.UPENDO NA AMANI MLIYOIONYESHA WAZANZIBAR UDUMU MILELE DAIMA.ONGERA DR.SHEIN KWA KUCHAGULIWA KUWA RAIS WA ZANZIBAR,ONGERA MAALIMU SEIF KWA KUTUONYESHA UPENDO NA AMANI.M/MUNGU AWABALIKI KATKA KUIONGOZA ZANZIMA.AMANI NA UPENDO VIDUMU DAIMA MILELE.ALL THE BEST

    ReplyDelete
  4. naHISI KULIA KWA furaha iliyojaa tele moyoni mwangu....hongera seif..wewe ni shujaa anastahili kuigwa ...amenusuru damu za wazaznibari wengi sana kumwagika... Mungu ibariki Zanzibar Mungu ibariki TAnganyika

    ReplyDelete
  5. sasa wazanzibar wameamua kuungana na kuwa kitu kimoja, sasa waachieni wazanzibar na zanzibar yao na nyinyi wa tanganyika angalieni tanganyika yenu waacheni na wenzenu wajiongoze kimataifa na walete maendeleo kwenye nchi yao ya zanzibar

    mungu ibariki zanzibar na wabariki watu wake....mungu ibariki tanganyika na watu wake dumisha umoja na amani.

    ReplyDelete
  6. Nchi sasa itakuwa kwani ukiziangalia nyuso zao tu utapata jibu kuwa hawa wote wawli wanaubinaadamu
    na iwe isiwe mpemba hatomtupa mpemba mwenzake,zimwi likujualo halikuli likakwisha........, maendeleo yatakuja sasa zanzibar na watu watafaidika na uongozi huu mzuri sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...