MBUNGE KUTEULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS

Mh. Seif Ali Iddi, MB, aliteuliwa kuwa Makamu wa pili wa rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar il hali ni Mbunge aliyeshinda uchaguzi uliopita katika jimbo la kitope, wilaya ya magharibi.

Kwa wadhifa huu mpya, pamoja na mambo mengine Balozi Seif atakuwa mkuu wa shughuli za serikali ndani ya baraza la wawakilishi kama alivyokuwa waziri kiongozi na mara nyingi baraza hukaa sambamba na bunge la jamhuri ya muungano ambapo atatakiwa kuhudhuria kama mbunge.

Kwa kuwa katiba ya Zanzibar ilirekebishwa mara baada ya kikao cha mwisho cha baraza la wawakilishi ili kuendana na serikali ya umoja wa kitaifa, suala hili halijawekwa bayana endapo mwakilishi au mbunge wa kuchaguliwa atachukuliwa vipi endapo atapata wadhifa wa makamu wa kwanza au wa pili wa rais. Utaitishwa uchaguzi mwingine na tume ya uchaguzi Zanzibar kwa kuwa makamu wa rais wa nchi atakosa muda wa kuitumikia nchi, jimbo lake, kuhudhuria vikao vya bunge na hapo hapo baraza la wawakilishi?

Wataalamu wa sheria na katiba ya Zanzibar tu mnakaribishwa, si vema kuleta longolongo katika ishu hii nyeti.

Baba ochu
Jang'ombe kwa maharukui.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. kujua taratibu za nchi hakuhitaji kuwa mwanasheria, kimsingi kisheria hadi sasa hakuna sheria au kanuni inayomzuia mtu kushika nafasi hizo zote, na ndio maana kwa mujibu wa sheria za zanzibar kuna wawakilishi huteuliwa kuliwakilisha baraza la wawakilishi katika bunge la muungano, kinachojitokeza hapo ni mgongano wa kiutendaji namna ya kutekeleza majukumu hayo. nimefungua mlango karibuni wadau mchangie uwe mwanasheria au mbumbumbu kama mie

    ReplyDelete
  2. Mimi ni mbu mbu mbu lakini nivayoona yaliyofanyika huko kwetu Zenj ni matakwa ya watu wawili, Alhaj Karume na Maalim Seif, kama ilivyokuwa mwaka 1964 kati ya Sheikh Karume na Mwalimu Nyerere na matunda yake (matamu na machungu) ndio tunatafuna leo!!! Utamaduni wetu sisi Waafrika ni kufanya mambo kienyeji na inapozuka suala la kisheria tunabaki kushangaa kwa nini watu wanashangaa!!

    ReplyDelete
  3. @ anony # 2
    haya sio matakwa ya karume na seif kwani ilipigwa kura ya maoni kuuliza jambo hili na watu wengi walilitaka tofauti na muungano wa zanzibar na tanganyika hakukuwa na kura ya maoni,jaribu kufatilia mambo vizuri ..usikubali kuongozwa na mapenzi yako ya kisiasa bali ongozwa na ukweli.pia jambo hili limefanyika ili damu isimwagike zanzibar kama ilivyokuwa kabla ya uhuru wa zanzibar na baada ya kurejeshwa tena mfumo wa vyama vingi hapo visiwani.sasa je lipi bora kati ya amani na kuuwana?

    ReplyDelete
  4. jamani hebu tujaribu kujadili nafasi ya sheria katika hili swala si vyenginevye mi naona kuna utata hapa mh seif ali iddi now ana post tatu makamo wa pili wa rais mbunge na mwakilishi so kisheria hapo inakuwaje hebu waungwana tuwekeeni wazi hapa hayo malumbano hayana msingi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...